Utafiti: wanasayansi wanachunguza jinsi saratani 'inavyozaliwa'

Breast cancer cell Haki miliki ya picha Francis Crick Institute

Wanasayansi wa Uingereza na Marekani wameungana kutafuta dalili za mapema za ugonjwa wa saratani katika juhudi za kugundua na kutibu kabla ijitokeze.

Wanapanga "kuzalisha" saratani katika maabara ili kubaini muonekano wake "siku ya kwanza".

Hii ni moja wa tafiti zinazopewa kipaumbele na muungano huo wa kimataifa wa wanasaya wanaofanya shughuli za ugunduzi wa mapema wa saratani.

Kufanya kazi pamoja katika mradi huo kunamaanisha watu wanaougua saratani watafaidika zaidi, unasema muungano huo.

Kupiga hatua

Kwa pamoja wanasayansi hao wanalenga kufanya uchunguzi kama vile wa damu, pumzi na kupima mkojo ili kuwabaini wagonjwa walio katika hatari zaidi, kuimarisha mbinu ya ugunduzi wa mapema wa saratani na kuangazia kwa jumla dalili zisizonekana za ugonjwa huo.

Lakini wamekiri kuwa hatua hiyo "ni kama kutafuta sindani gizani" na huenda ikachukua miaka 30.

"Tatizo la msingi ni kwamba hatujawahi kuona jinsi saratani inavyozaliwa katika mwili wa binadamu," anasema Dkt David Crosby, Mkuu wa kitengo cha ugunduzi wa mapema wa magonjwa katika taasisi ya utafiti wa saratani nchini Uingereza.

"Wakati inapogunduliwa, huwa tayari imejiimarisha."

Haki miliki ya picha Patrick Harrison, Cancer Research UK
Image caption Uchunguzi wa saratani kupitia vipimo vya damu umependekezwa kwa muda mrefu na wanasayansi

Watafiti kutoka Manchester, kwa mfano wanakuza tishu za matiti ya binadamu kwenye maabara na seli za kinga za synthetic ili kuona ikiwa wanaweza kuona mabadiliko ya mapema kabisa, ambayo yanaweza kusababisha saratani.

Prof Rob Bristow anasema ni sawa na "kuwa na tishu hai inayoishi nje ya mwili wa mgonjwa ".

Ukwili ni kwamba kuna hatari ya utambuzi zaidi a magonjwa, kwa sababu seli zote zilizo chungunzwa mapema zinaweza kubadilika na kuwa chanzo cha saratani.

Kwa hivyo wanasayansi wanazingatia hilo kwa kuangazia zaidi jeni watu walizozaliwa nazo na mazingira waliokulia ilikutathmini hatari inaowakabili linapokuja suala la ugunduzi wa mapema wa ugonjwa wa saratani kwa mtu binafsi.

Haki miliki ya picha Rafat Chowdhury
Image caption Uchunguzi wa kina wa MRI huenda ukawa mbinu ya mapema ya ugunduzi wa saratani tezi dume

Ni kupitia njia hiyo wataweza kukabiliana ka ugonjwa huo.

'gharama ya kuzima moto'

Hadi wa leo wanasayansi wanasema, utafiti kuhusu ugunduzi wa mapema wa ugonjwa huo umefanywa kwa kiwango kidogo na kwamba changamoto inayotokana na ukosefu wa kufanyia majaribio matokeo ya utafiti kwa watu wengi imerudisha nyuma juhudi za kufikia tiba kamili.

Dr Crosby anasema ushirikiano huu "utachangia kuleta mabadiliko katika mifumo ya afya na kuondokana na hali ya kukabiliana na saratani ikiwa katika kiwango ambacho gharama ya tiba iko juu na badala yake kubuni mbinu ya ugunduzi wa mapema ambayo pia gharama ya matibabu ni bei nafuu".

Takwimu zinaonesha kuwa 98% ya wagonjwa wa saratani ya matiti huishi kwa miaka mitano au zaidi ikiwa ugonjwa uligunduliwa mapema- katika daraja la kwanza,ikilinganishwa na 26% ya watu wanaogunduliwa kuwa na ugonjwa huo ikiwa katika daraja la nne.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii