Mwanaharakati wa walemavu India aambiwa 'avue suruali ' na maafisa usalama

Disability activists Kuhu Das (standing left) and Jeeja Ghosh (seated) at Kolkata airport Haki miliki ya picha Courtesy: Kuhu Das
Image caption Wanaharakati wa walemavu Kuhu Das (aliyesimama kulia) na Jeeja Ghosh (aliyekaa) wamesema walihisi " wametukanwa na kudhalilishwa " katika uwanja wa kalkata

Maafisa wa uwanja wa ndege wa India wa Kolkata wamewaomba msamaha wanaharakati walemavu wawili, ambao mmoja kati yao anasema aliambiwa avue suruali yake.

Kuhu Das ambaye alipata ulemavu kutokana na ugonjwa wa kupooza (polio) aliambiwa atoe chuma kilichokua mguuni kwake , licha ya kwamba alimwambia afisa wa usalama mwanamke kuwa asingeliweza kukitoa bila kuvua suruari.

Jeeja Ghosh ambaye ni mwanaharakati wa pilii ambaye anaulemavu wa shingo , aliambiwa kuwa hawezi kusafiri bila mtu wa kumsindikiza.

Walikuwa wakisafiri kuelekea mjini kwa ajili ya mkutano uliokuwa ukijadili juu ya haki za wanawake walemavu.

Unaweza pia kusoma:

Baada ya kugoma waliruhusiwa kusafiri, lakini wanaharakati hao wanasema kuwa walihisi "wametusiwa na kudhalilishwa".

Bi Das, ambaye alipatikana na ugonjwa wa kupooza akiwa na umri wa miaka mitatu, amaeambia BBC kuwa amekuwa akivaa chuma hicho kwenye mwili wake kwa miaka mingi.

Jumapili mchana alipokwenda katika uwanja wa ndege , afisa wa polisi alimtaka atoe chuma chake ili aweze kuwekwa kwenye kifaa cha uchunguzi wa usalama (skan) .

Unaweza pia kusikiliza:

Huwezi kusikiliza tena
Wazazi waliyo na watoto walemavu Zanzibar washauriwa kutowaficha majumbani

"Nilipokataa , alimuita afisa mwingine na mbele yangu , akamwambia mwenzake kwamba hajawahi kuona mtu yeyote kama mimi . Ni kama nilikuwa nimetoka sayari nyingine. Hiyo ilikuwa ni kauli ya kutojali hali yangu ?"

Bi Das anasema hajawahi kukabiliana na tatizo la aina hiyo katika viwanja vya ndege nje ya India.

"Haikubaliki kwamba kila wakati nchini India , wanataka nitoe gurudumu nayomaanisha kuwa nitoe suruari yangu ," alisema.

Amesema kuwa mhudumu wa kampuni ya ndege ya GoAir, ambayo ni ya kibinafsi waliyokuwa wakisafiria alimwambia mwenzake aliyekua akisukuma baiskeli yake ya walemavu Jeeja Ghosh kuwa hawezi kusafiri kama hana mtu wa kumsindikiza.

"Jeeja ni mtu mzima" ambaye anasafiri maeneo mbali mbali kote duniani peke yake na anahisi "ametusiwa sanba " na ndege, alisema Bi Das.

"Tulipinga , tulisema huu ni ubaguzi, kwa hiyo mtu aliyekuwa akituhudumia akaomba msamaha. Lakini tulikasirika sana. Sio tatizo la mtu mmoja. Hivyo ndio kampuni ya ndege inavyowachukulia watu wenye ulemavu " aliongeza.

Baada ya taarifa kuhusu kisa chao kutangazwa kwenye vyombo vya habari vya India. maafisa wa uwanja wa ndege wa Kolkata Jumatatu iliytuma ujumbe wa twitter wa kuomba msamaha kwa wanaharakati hao wawili.

Miama miwili iliyopita, maafisa walisema kuwa wasafiri wenye ulemavu hawatalazimika tena kutoa magurudumu au vyuma walivyonavyo mwilini kwa ajili ya uchunguzi wa kiusalama katika viwanja vya ndege , lakini miaka miwili baadae, inaonekana agizo hilo bado haijawafikia maafisa wa usalama.

India ina watu takriban milioni 26 wanaoishi na ulemavu wa mwili, lakini kuna uhaba wa miundombinu ya kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Wanaharakati wanasema watu wenye ulemavu pia hukabiliana mara kwa mara na unyanyapaa , ubaguzi na udhalilishwaji.

Mwaka 2016 mwanaharakati ambaye alitumia kiti cha magurudumu cha walemavu alipigwa kwa kutosimama wakati wimbo wa taifa ukiimbwa katika ukumbi wa sinema.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii