Mzozo wa Syria: Erdogan atishia kufufua mashambulizi muda wa usitishaji mapigano ukimalizika

Mkutano wa Erdogan na Putin umefuatia mazungumzo ya simu baina ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Putin juu ya kurefusha muda wa kusitisha mapigano uliosainiwa pia na Marekani Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkutano wa Erdogan na Putin umefuatia mazungumzo ya simu baina ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Putin juu ya kurefusha muda wa kusitisha mapigano

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema kuwa ataendelea na operesheni ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Syria "akiwa na azma kuu " ikiwa wapiganaji wa Kikurdi watashindwa kutekeleza wajibu wao katika makubaliani ya usitishaji mapigano na Marekani.

Unaweza pia kusoma:

Akizungumza alipokuwa akitoka mjini Ankara kwa ajili ya mkutano wa Oktoba 22 na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, kwenye mwambao wa bahari nyeusi wa Sochi, Erdogan amesema kuwa kikosi cha ulinzi cha Wakurdi (YPG) lazima kiondoke "eneo salama" Uturuki inataka kubuni eneo refu la mpaka wake na Syria.

" Kama ahadi zilizotolewa na Marekani kwa nchi yetu hazitaheshimiwa, tutaendeleza operesheni zetu kuanzia pale tulipoachia kwa azma kuu ," alisema.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan wanaunga mkono pande zinazopingana katika vita vya Syria

Makubaliano ya usitishaji mapigano ya siku tano mjini Washington yanamalizika siku hiyo katika eneo ambalo Uturuki inajaribu kuweka ''eneo salama'' la kilomita 120 karibu na mpaka wake na nchi hiyo inayotawaliwa na mizozo na ambako inataka kuwaweka wakimbizi wapatao milioni 2 ambao inawahifadhi.

Msemaji wa vikosi vinavyoongozwa na Wakurdi nchini Syria amethibitisha kuwa wanawahamisha wapiganaji wao kutoka mji muhimu wa Ras Al Ayn, ili kufungua njia kwa ajili ya wapiganaji wa Kikurdi kuondoka kutoka maeneo ya mpaka wa Uturuki na Syria.

Chini ya mkataba uliofikiwa na Marekani, Uturuki ilikubali kusitisha mashambulio yake katika eneo ili kuzuwia Wakurdi kurudi nyuma.

Huwezi kusikiliza tena
Raia wa Uturuki wakipiga viazi gari la Marekani

Viongozi wa Kikurdi wamekwishasema kwamba baada ya kuondoa Ras al Ayn wataondoa majeshi yao kutoka eneo salama lililopo kwenye mpaka wa Uturuki na Syria kulingana na makubaliano ya usitishaji mapigano. Wana hadi kufikia Jumanne kufanya hivyo.

Wavuti wa Kremlin umeeleza kuwa mkutano baina yao katika hoteli ya kifahari iliyoko kwenye mji uliopo kando ya Bahari nyekundu wa Sochi utaaangazia pia masuala yanayohusiana na " kukabialiana na makundi ya ugaidi ya kimataifa pamoja na mchakato wa kutatua matatizo ya kisiasa " nchini Syria.

Ziara ya Erdogan imekuja baada ya mazungumzo ya simu baina ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Putin, ambapo ombi lilitolewa la kurefusha muda wa kusitisha mapigano.

Image caption Ramani inayoonyesha hali halisi ya mzozo wa Syria

Macron alimsisitizia Putin, ambaye amewaagiza askari wake kufanya doria katika maeneo ya kaskazini mwa Syria juu ya " Umuhimu wa kurefusha kipindi cha sasa cha kusitisha mapigano na kumaliza mzozo kwa njia za kidiplomasia ."

Uturuki ilianzisha mashambulizi dhidi ya vikosi vinavyoongozwa na Wakurdi tarehe 9 Oktoba baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa anaondoa vikosi vya Marekani vilivyosalia kutoka kaskazini magharibi mwa Syria.

Uturuki inawaona wanamgambo wa Kikurdi wa Syria YPG kama magaidi , ingawa Wakurdi walitumiwa katika vita vya kuwashinda wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS) nchini Syria mapema mwaka huu pamoja na vikosi vya Marekani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii