Sochi 2019: Mkutano wa kwanza unaidhinisha kurudi kwa ushawishi wa Urusi Afrika

The leaders of Russia and Egypt have been accused of cracking down on the opposition Haki miliki ya picha Getty Images

Katika miaka michache iliyopita, Urusi imerudi upya kama nguvu ya kutambuliwa katika bara la Afrika.

Ushirikiano mwingi uliokuwepo katika enzi za uliokuwa muungano wa Sovieti ulikatizwa baada ya kuanguka kwa Muungano huo, lakini wakati uhusiano na magharibi ukififia kwa mara nyingine, Kremlin imeidhinisha uhusiano wa kutosha kiuchumi, kiusalama na kisiasa na Afrika.

Moscow itajaribu kuimarisha zaidi uhusiano huu wakati wa mkutano wa kwanza baina ya Urusi na Afrika unaofanyika mjini Sochi kuanzia leo tarehe 23 hadi kesho Oktoba 24. ratiba ya mkutano huo ni kujadili nishati, madini na ushirikiano wa kijeshi.

Kufikia 2018, biashara ya Urusi na bara la Afrika ilikuwa na thamani ya dola bilioni 20.4, iliyoongezeka mara nne zaidi ya ilivyokuwa 2010.

Kumekuwa na tuhuma nyingi kuhusu Urusi kupanua kwa siri uwepo wake kijeshi kwa kuwatumia mamluki katika baadhi ya mataifa ya Afrika na pia kuwatuma wawakilishi na kusambaza taarifa zisizo sahihi katika kampeni ya kushawishi siasa za dai ya nchi.

Moscow imeshuhudia ziara rasmi zinazoongezeka, huku viongozi 12 wa mataifa ya Afrika wakifika katika mji mkuu Moscow tangu 2015.

Mkutano huo unafanyika chini ya uenyekiti wa rais Vladimir Putin na kiongozi mwenzake wa Misri ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, Abdel Fattah el-Sisi.

Biashara ya silaha

Mkutano huo unatoa fursa kwa Urusi kujadili mikataba ya silaha na ushirkiano wa kijeshi.

Licha ya kwamba soko la silaha za Urusi ni Asia, Moscow imefanikiwa kujikita Afrika pia. Kwa mujibu wa taasisi ya utafiti - Stockholm International Peace Research Institute (SIPRI), Asia hununua kiasi ya nusu ya silaha zote zinazosafirishwa kutoka Urusi, huku Afrika ikinunua 30% mnamo 2018, huku wateja wakuu wakitoka Afrika kaskazini - yaani Algeria na Misri - ikijumuisha 95% ya mauzo yote ya silaha za Urusi barani Afrika mnamo 2018.

Urusi pia imeziuzia silaha Angola, Burkina Faso, Cameroon, Equatorial Guinea, Mali, Nigeria, Sudan kusini na hata Sudan.

Mnamo Septemba 2018, mkuu wa idara ya huduma kwa jeshi Dmitry Shugayev amesema mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara yaliagiza silaha zenye thamania ya zaidi ya dola bilioni 3.

Nigeria imeeleza kutaka kusaini ushirkiano wa kijeshi mwezi huu Oktoba, gazeti la Urusi Izvestia limeeleza. Rais Muhammadu Buhari anatarajiwa kukutana na Putin kando kando mwa mutano huo kukamilisha makubaliano yatakayoisaidia serikali kupambana na wanamgambo wa Boko Haram, Balozi wa Nigeria mjini Moscow amesema.

Mnamo Agosti mwaka huu, wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema mazungumzo yanaendelea kuanzisha utaratibu katika bandari Eritrea " kuidhinisha biashara ya pande mbili". Mradi huo pia utaiweka Urusi karibu na kambi ya kijeshi ya Marekani katika nchi jirani ya Djibouti.

Mamluki

Haki miliki ya picha ROSSIYA 1
Image caption Televisheni nchini Urusi ilikana uwepo wa mamluki wa Kirusi barani Afrika

Suala moja ambalo litasalia kimya kima ni taarifa za uwepo wa mamluki wa Urusi barani Afrika.

Waandishi watatu wa Urusi waliuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka mmoja uliopita wakiwa wanachunguza ripoti kuwa kampuni binafsi ya kijeshi inayoitwa Wagner ipo nchini humo.

Inaarifiwa kuwa Wagner ina uhusiano na mfanyabiashara anayehusishwa na Kremlin Yevgeny Prigozhin.

Kwa mujibu wa Bloomberg, Wagner ipo katika mataifa mengine kadhaa zikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Sudan, Libya, Madagascar, Angola, Guinea, Guinea-Bissau, Msumbiji, na Zimbabwe.

Hivi karibuni, mwezi huu Oktoba, The Times iliripoti kuwa mamluki wapatao 200 wa Urusi waliwasii Msumbiji kuisaidia serikali kupambana na wapiganaji jihadi. Kremlin ilikana uwepo wa wanajeshi wa Urusi katika taifa hilo.

Kampeni za ushawishi wa kisiasa

Kumekuwa na taarifa pia kwamba Urusi imekuwa ikijaribu kushawishi siasa katika baadhi ya mataifa ya Afrika kupitia operesheni za mfanyabiashara huyo Prigozhin.

Mfano, Kremlin inatuhumiwa kujaribu kushawishi uchaguzi wa urais wa Malagasy mwishoni mwa 2018.

Mnamo Mei mwaka huu Urusi ilituhumiwa kuwahiribia jina viongozi wa upinzani Afrika kusini Julius Malema na Mmusi Maimane.

Duru za kutoka Kremlin zimetoa taarifa mwezi huu zikipuuzilia mbali kuwa Prigozhin aliuawa katika ajali ya ndege huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mradi wa uchunguzi - The Dossier Centre, unaofadhiliwa na mkosoaji wa serikali ya Urusi, Mikhail Khodorkovsky, umedai kuwa mfanyabiashara huyo Prigozhin alihusika pia katika mipango ya Urusi kumuunga mkono kiongozi wa Sudan wa zamani Omar al-Bashir.

Mnamo Desemba 2018, Al-Bashir alikuwa kiongozi wa kwanza wa jumuiya ya nchi za kiarabu kuizuru Syria tangu kuzuka vita nchini humo.

Alipigwa picha akisalimiana na rais Assad mbele ya ndege ua Urusi ambayo inaarifiwa ndio iliomsafirisha kwenda Damascus.

Mafuta na Gesi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alifanya ziara kwenda Moscow mnamo Agosti

Kampuni kubwa za mafuta Urusi Rosneft na Lukoil zimehusika katika uchimbaji wa mafuta na gesi barani Afrika.

Rosneft imehusika katika utafutaji gesi nchini Msumbiji na inashikilia 20% ya hisa katika mradi huo. Inamiliki hisa pia katika miradi kama hiyo nchini Misri na Algeria, licha ywa kwamba kumekuwana taarifa kwamba Urusi inatazamai kuuza hisa zake hapo baadaye.

Lukoil ina miradi nchini Cameroon, Ghana, Nigeria, kwa mujibu wa gazeti la biashara la kila siku Kommersant.

Mnamo Juni mwaka huu, iliarifiwa kuwa Lukoil inaelekea kukamilisha ununuzi wa 25% ya hisa ya mradi wa mafuta Marine XII katika Jamhuri ya Congo, gazeti la Urusi Vedomosti limeandika.

Nyuklia

Nishati ya nyuklia inatarajiwa kuwa mada kuu katika mkutano huu wa Sochi.

Imeripotiwa kuwa Putin huenda akajadili ujenzi wa rusi wa kinu cha kwanza cha nyuklia huko El Dabaa nchini Misri.

Ujenzi huo unatarajiwa kuanza mwakani, huku Urusi ikijitolea mkopo wa dola bilioni 25 kwa Misri kufadhili mradi huo.

Katika mahojiano na shirika la habari Urusi RIA Novosti, balozi wa Nigeria mjini Moscow Steve Ugbah amesema rais Muhammadu Buhari alinuia kujadili uwezekano wa Urusi kuhusika katika ujenzi wa vinu viwili vya nyuklia nchini mwake.

Kwa mujibu wa RIA Novosti, Ethiopia pia inatumai kutumia mkutano huu leo kusaini makubaliano na Urusi kuhusu ujenzi wa kinu cha nyuklia.

Haki miliki ya picha Valery Sharifulin

Kwa sasa Urusi ina ushirkiano wa miradi ya nyuklia na Rwanda, Uganda na Sudan.

Bwawa Ethiopia

Mkutano wa Sochi pia unatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo yanayolenga masuala matupu kuhusu Afrika.

Mfano Misri na Ethiopia zinatarajiwa kutafuta azimio la mkwamo kuhusu mradi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance katika mto wa Blue Nile nchini Ethiopia.

Cairo inasema linaweza kusababisha uhaba wa maji nchini Misri.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii