Namna ya kuyatamka sawa majina ya wanamichezo nyota wa Afrika

Liverpool star and Senegalese player Sadio Mané

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Unalitamkaje jina la nyota huyu wa Liverpool

Katika msururu wa barua za kutoka kwa waandishi wa Afrika, mwandishi wa Sierra Leone Ade Daramy anafafanuwa kwanini anakerwa anapoona Waafrika wanafanikiwa katika michezo.

Nilipotazama mashindano ya ubingwa wa riadha duniani huko Qatar, kama Muafrika mwingine, ilikuwa ni mshtuko kila aliposhinda mwanamichezo kutoka bara la Afrika.

Sio kwamba ni kuchukizwa na matokeo yao bali kilichonikera namna majina yao yalivyotamkwa na kukosewa yanapotajwa na watangazaji wa michezo.

Chukua mfano wa mwanaidha mshindi wa medali kadhaa Nafissatou Thiam kutoka Ubelgiji. Jina lake la pili bado linatamkwa kama "tee-am".

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nafissatou Thiam, ambaye babake anatoka Senegal, alishinda medali ya fedha katika mashindano ya wanawake ya heptathlon huko Doha mapema mwezi huu

Babake ni raia wa Senegal na jina lake linatamkwa "cham".

Baada ya ushindi wa mara kadhaa wa medali ungedhani mtu angejiuliza: "Hili sio jina la kawaida, je linatamkwaje?"

Lakini imekuwa kila mtu analitamka namna yeye anavyohisi ni sawa.

Lakini sio kwamba Waafrika hawakerwi.

Katika siku za kabla ya mitandao ya kijamii, watu walikuwa wakipigiana simu na kuambiana: "Umeskia amelitamka vipi lile jina?"

Siku hizi, huenda tukasambaza kanda ya sauti au video sekundi kadhaa baada ya kutamkwa kimakosa.

"Foul" hiyo ni kawaida pia katika ulimwengu wa soka ambapo watangazaji wanakunguwaa ulimi wanapoyataja majina makubwa ya nyota wa kutoka Afrika wanaozichezea klabu kubwa za Ulaya.

Kidokezo kikuu

Watangazaji soka hawana shida kulitamka jina la pili la mlinzi wa Uhispania Cesar Azpilicueta lakini wakashindwa kulitamka jina la pili lenye silabi mbili la Mohamed Diamé, aliyekuwa mchezaji wa timu yatifa ya Senegal anayeichezea Qatar hivi sasa.

Chanzo cha picha, Fifa via Getty

Maelezo ya picha,

Jina la Mame Biram Diouf linapaswa kutamkwa "Mam Biram Joof"

Basi huu hapa muongozo kwa watangazaji michezo:

  • Diamé - halitamkwi "dee-ah-may", badala yake "Jammeh" kama jina la aliyekuwa rais wa Gambia Yahyah Jammeh
  • Jina la kwanza la nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal - Sadio Mané' halitamkwi "sah-dee-oh", badala yake "sah-jaw"
  • Jina la kwanza la mchezaji wa England Dele Alli limefupishwa kutoka jina la KiNigeria "Bamidele"
  • Jina la pili la mchezaji wa Stoke City Mame Biram Diouf, kutoka Senegal, halitamkwi "dee-oof", badaa yake "joof"
  • Badou Ndiaye pia ni mchezaji wa Stoke na jina lake la pili hutamkwa "nj-eye"
  • Aboubakar Kamara wa Fulham ambaye ana asili ya Mauritania - jina lake hutamkwa kama lilivyo "ka-ma-ra"
  • Jina la mwisho la Moussa Wagué wa Senegal, anayeichezea Barcelona, hutamkwa "wah-geh"

' Funika masikio'

Na haitoshi kwa mchezaji kama Pape Bouba Diop kufunga goli lililochangia kushindwa mabingwa watetezi Ufaransa katika mechi ya kwanza ya kombe la dunia mnamo 2202 au kwamba amecheza soka England kwa miaka minane, jina lake bado linakoseka.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Papa Bouba Diop aliifungwa Ufaransa katika kombe la dunia mnamo 2002

Aliitwa "Papa Bouba Dee-op" - kwanza jina lake la awali linatamkwa "pap", na la pili linapotamkwa husikika kama "robe" neno la kizungu.

Ni jambo la kuiskitisha kwamba tunaliangazia hili leo miaka 17 baada ya kumalizika muda wake katika mchezo wa kulipwa kwasababu ingelikuwa vizuri kuiskia jina lake likitamkwa sawasawa angalau mara moja katika muda aliocheza.

Ushauri kwa waafrika ni kuhakikisha kwamba wana vitu viwili muhimu kila wanapofuatilia mashindano makubwa ya michezo: Televisheni kubwa na viziba masikio.

Kwahivyo iwapo watangazaji hawatoshughulika au hawatobadili namna wanavyoyatamka majina haya, itabidi tuvumilie tu katika mashindano yajayo ya kombe la dunia Qatar 2022.

Tazama Pia:

Maelezo ya video,

David Luiz wa Arsenal azuru Rwanda