Nusrat Jahan Rafi: Hukumu ya kifo kwa watu 16 waliomchoma moto mwanafunzi Bangladesh

Picha ya Nusrat Jahan Rafi

Chanzo cha picha, family handout

Maelezo ya picha,

Nusrat alimwagiliwa mafuta ya taa na kuchomwa moto juu ya paa

Mahakama nchini Bangladesh imewahukumu kifo watu 16 waliomchoma moto hadi kufa mwanafunzi kwa kuripoti kuwa mwalimu mkuu amenyanyasa kingono.

Nusrat Jahan Rafi, 19, alifariki mwezi Aprili katika mji wa Feni, uliopo kilo mita 160 nje ya mji mkuu wa Dhaka.

Mwalimu mkuu aliyetuhumiwa na Nusrat kwa unyanyasaji na wanafunzi wawili wa kike ni miongoni mwa waliohukumiwa kifo.

Kifo chake kilishangaza nchi nzima na kusababisha msururu wa maandamano kushinikiza Nusrat apate haki.

Kesi hiyo ni ya kwanza kuamuliwa haraka nchini ikilinganishwa na nyingine kama hizo ambazo huchukua miaka kadhaa kabla ya kuamuliwa. Mwendesha mashtaka Hafez Ahmed aliwaambia wanahabari kuwa "wauaji sharti wachukuliwe hatua Bangladesh".

Mawakili wa washtakiwa wanasema watakata rufaa.

Maelezo ya picha,

Polisi wakishika dori nche ya mahakama Machi 24

Uchunguzi wa mauaji ya Nusrat ulionesha njama ya kutaka kumnyamazisha ambayo pia ilihusisha wanafunzi katika darasa lake pamoja na wanaume walio na ushawishi mkubwa katika jamii.

Walimu watatu wakiwemo mwalimu mkuu, Siraj Ud Doula, ambaye polisi inasema alitoa amri ya kuuwa kwa mwanafunzi huyo kutoka jela, walipatikana na hatia ya mauaji siku ya Alhamisi.

Wengine wawili waliopatikana na hatia ni Ruhul Amin na Maksud Alam, kiongozi wa chama tawala cha Awami League party.

Maofisa kadhaa wa polisi pia walipatikana na hatia ya kushirikiana na wale waliokamatwa kueneza taarifa za uwongo kwamba Nusrat alijitoa uhai.

Familia ya Nusrat, ambayo iliunga mkono hatua yake kwenda polisi mwezi machi, imepewa ulinzi, vyombo vya habari viliripoti.

hukumu hiyo imepokelewa vyema na kutoa wito itekelezwe haraka iwezekanavyo.

Maelezo ya picha,

Wanawake wakiandamana nje ya mahakama siku ya Alhamisi

Nini kilichomtokea Nusrat?

Kwa mujibu wa taarifa ya mashtaka iliyotolewa na Nusrat, mwanafunzi mwenzake wa kike alimpeleka kwenye paa la shule, alisema mmoja wa marafiki zake alikuwa amechapwa.

Wakati Nusrat alipofika juu ya paa watu wanne au watano, waliokuwa wamevalia burqa, walimzingira na kumshinikiza aachane na kesi dhidi ya mwalimu mkuu.

Alipokataa ndipo walipommwagia mafuta ya taa na kumchoma kwa moto.

Mkuu wa Idara ya upelelezi ya polisi Banaj Kumar Majumder alisema kuwa wauaji wanaotafutwa "walitaka kufanya mauaji hayo yaonekane kama Nusrat alijiua mwenyewe ".

mpango wao uliharibika wakati Nusrat alipookolewa baada baada ya kutoroka eneo la tukio. Aliweza kutoa taarifa kabla ya kufa.

" Mmoja wa wauaji wake alishindilia kichwa chake chini kwa kutumia mikono yake, kwa hiyo mafuta ya taa hayakumwagika pale na ndio maana kichwa chake hakikuungua ," Bwana Majumder aliiambia BBC mjini Bengali.

Lakini wakati Nusrat alipopelekwa katika hospitali iliyopo karibu asilimia 80% ya mwili wake ulikuwa na majeraha. Hawakuweza kutibu vidonda , na kuamua kutuma katika hosptali ya chuo cha tiba cha Dhaka.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mashirika tofauti yameshiriki maandamano y akupinga mauaji ya Nusrat Rafi, mwanafunzi aliyechomwa moto kwa kulalamikia unyanyasaji wa kingono

Unyanyasaji wa kingono ni mbaya kiasi gani Bangladesh?

Wasichana wengi na wanawake wenye umri mdogo nchini Bangladesh huamua kunyamaza kimya wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono au kubakwa kwa kuhofia kudhalilisha na jamii au familia zao.

Unyanyasaji wa kingono umekithiri sana nchini Bangladesh: ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na shirika misaada la ActionAid mapema mwaka huu ilibaini kuwa 80% ya wanawake wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza nguo huenda wamekumbana na visa vya unyanyasaji wakiwa kazini au kudhulumiwa kingono .