Upasuaji wa kuongeza makalio: Kwa nini nataka kuondoa makalio yangu 'bandia'

Picha za Sophie Elise

Chanzo cha picha, Sophie Elise

Sophie Elise alikuwa na umri wa miaka 20 wakati alipoamua kwamba anataka kuongeza makalio yake ili kuwa makubwa.

Mwanablogu wa Norway na mtu maarufu katika runinga, ambaye alidai kuwa mwembamba sana anasema kwamba alitaka kuongeza kidogo eneo lake hilo la mwili wake.

Haikuwa vigumu kuanza kufanya utafiti wa upasuaji huo. Washawishi katika akaunti yake ya instagram waliwasilisha majina ya maeneo na madaktari ambao wangefanya upasuaji wa kuongeza makalio unaojulikana kama BBL.

Alipata eneo moja nchini Uturuki.

Na bei yake je? Hatutafichua gharama yake lakini anasema kwamba ilikuwa bei ya majadiliano.

Kweli ilikuwa rahisi zaidi ya ilivyotarajiwa. Ingemgharimu fedha zaidi, Sophie aliambia radio 1 Newsbeat.

Chanzo cha picha, Sophie Elise

Maelezo ya picha,

Sophie alifanyiwa upasuaji miaka mitano iliopita

"Waliniuzia ndoto yangu''.

''Katika kifurushi cha mahitaji kulikuwa na uangalizi wa baada ya upasuaji , walikupatia dereva wa kibinafsi, unapewa afisa wa afya atakayekutembelea nyumbani, hospitali yenyewe ilikuwa safi sana''.

Kweli nilihisi kwambal ilikuwa chaguo zuri sana. Hivyobasi ni kwa nini baada ya miaka mitano anataka kuondoa makalio hayo? Tatizo lilianza wakati alipofika nyumbani.

Kama mtu maarufu sana nchini Norway, akiwa na vipindi viwili vya runinga mbali na wafuasi 500,000 katika Instagram , anasema kwamba maoni kuhusu upasuaji huo yalianza kumwagika.

''Watu walisema kwamba makalio hayo hayakuingiliana na umbo la mwili wangu. Sasa naweza kubaini kwamba hicho sio kitu ambacho ningefanya''.

''Kila kitu kiliharakishwa. Na naweza kusema kwamba sikufikiria sana kabla ya kufanya''.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 alichagua kufanyiwa upasuaji wa silicone badala ya ule wa BBL - ambapo mafuta hutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya mwili na kudungwa katika makalio.

Uingizaji wa Silicone ni chaguo bora kwa watu wasio na mafuta mengi katika miili yao na huongeza eneo linalokusudiwa kuwa kubwa zaidi ya BBL na mara nyengine inaweza kufanya mtu kuonekana tofauti na upasuaji aliofanya, kulingana na madakatari kadhaa wa upasuaji.

Sophie anasema kwamba hawakuwa na wasiwasi awali licha ya onyo kuhusu kuelekea ughabibuni ili kufanyiwa upasuaji wa kuongeza urembo.

Upasuaji wa kuongeza ukubwa wa makalio umepokea hisia mbaya katika miaka ya hivi karibuni , hususan kufuatia vifo vya wanawake wawili wa Uingereza waliosafiri hadi Uturuki ili kuongezwa makalio yao mwaka uliopita.

Wagonjwa huwa hatarini kukabiliwa na matatizo na hata kifo kwa kusafiri hadi ughaibuni ili kufanyiwa upasuaji kulingana na Muugano wa madaktari wa upasuaji nchini Uingereza Baaps.

Ni lazima wakuuzie huo uhondo.

Sophie anasema kwamba alikumbwa na uchungu mwingi badaa ya upasuaji huo - kama alivyotarajia - na kwamba ni sasa tu ambapo anakabiliwa na athari kufuatia uamuzi wake.

Anasema kwamba amegundua kwamba ana mwili mzuri na sasa anataka makalio hayo kuondolewa.

Sophie alipata daktari mwengine wa upasuaji kupitia utafiti katika tovuti maarufu badala ya watu wanaokuzwa na washawishi katika mtandao wa instagram.

''Lakini kumekuwa na tatizo. Siwezi kutoa kifaa cha silicone nahitajika kubadilisha na silicon nyengine ndogo'', anasema.

''Madaktari wapya niliokutana nao wanasema kwamba wanashuku kwamba upandikizaji niliofanyiwa ulikuwa ule wa matiti. Kwa kweli hicho sio kitu kizuri''.

Pia alifikiri kuhusu bei ya chini na mahitaji aliyopata baada ya upasuaji wake aliofanyiwa Uturuki.

''Unapokutana na daktari unapaswa kumuona mara kwa mara mbali na wewe mwenyewe kujiangalia''.

Hawawezi kukupatia uhondo wote. Sophie anasema kwamba alifanyiwa upasuaji mwengine na dakatari mwengine bora zaidi.

Lakini kwa sasa anaangazia kile ambacho tayari kipo ili kukipunguza kuwa kitu kidogo ili kuonekana kulingana na mwili wake.

''Sijuti kufanyiwa upasuaji'' , anasema Ni kwamba upasuaji niliofanyiwa na kuwekwa katika makalio yangu hakuingiliana na mwili wangu''.

''Hivyobasi sio upasuaji bali kiwango cha silicon kilichowekwa, nadhani''.

Anasema kwamba anajutia kutofanya utafiti zaidi.

''Ni vyema kuwa wazi kuihusu ili watu wengine wasipatikane na mtego kama huo. Sitaki kumuonya mtu yeyote asifanye chochote''.

Watu ni lazima wafanya kile wanachotaka. Lakini iwapo naweza kuwasaidia akina dada hilo litakuwa jambo jema.

''Na ushauri mzuri zaidi nilionao ni wewe kufanya utafiti wako. Usikimbilie chochote. Na iwapo upasuaji huo ni wa bei ya chini , basi hauna thamani''.

Rais wa Baaps Simon Withey awali amesema kwamba wagonjwa walio hatarini wanalengwa wazi kupitia mitandao ya kijamii na intaneti ili kusafiri ughaibuni kwa upasuaji wa bei ya chini na kwamba tatizo hilo ni rahisi kuongezeka.