Afrika inavyoweza kunufaika katika uhusiano wake wa kiuchumi na Urusi

Afrika inavyoweza kunufaika katika uhusiano wake wa kiuchumi na Urusi

Urusi inafanya mkutano wa siku mbili na Afrika katika mji wa Sochi kujaribu kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, kiusalama na kisiasa unaomalizika leo.

Ushirikiano mwingi uliokuwepo katika enzi za uliokuwa muungano wa Sovieti ulikatizwa baada ya kuanguka kwa Muungano huo, lakini wakati uhusiano na magharibi ukififia kwa mara nyingine, Kremlin imeidhinisha uhusiano wa kutosha na Afrika.

Kufikia 2018, biashara ya Urusi na bara la Afrika ilikuwa na thamani ya dola bilioni 20.4, iliyoongezeka mara nne zaidi ya ilivyokuwa 2010.

Lakini je Waafrika wanaweza kunufaika vipi na mkutano huu?. Gachau Kiuna Mwanzilishi wa Aqua power ametoa ushauri.