Jinsi ukoloni ulivyopalilia aibu dhidi ya watu wanene

A plus-size woman helps another to dress

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kwa mujibu wa watafiti, kuchukizwa na unene kumehusishwa kwa muda mrefu na fikra za kibaguzi kuhusu urembo

Zamani tangu hata kabla ya matangazo ya mitindo kushabikia watu wembamba, kuchukizwa na umbo la unene ni jambo lililotokana na fikra za kikoloni.

Wakati huo wa ukoloni, kuliibuka fikra nyingi kama kigezo cha kuwazidi nguvu watu wengine, na mojawapo ilikuwa ni imani iliyokuwepo kuhusu watu wanene and jamii ndogo zisizo za watu weupe.

Sabrina Strings ni naibu mhadhiri wa masuala ya kijamii katika chuo kikuu cha California, Irvine, na mwandishi wa kitabu "Fearing the Black Body: The Racial Origins of Fat Phobia".

Anaeleza kuwa waandishi na wanahabari pamoja na watangazaji katika enzi za ukoloni walifananisha unene katika koloni na kutisha, uvivu na udhaifu wa tabia.

Kinyume na hayo, unene katika jamii za magharibi mara nyingi uhusishwa na tabia za upole, katika wakati ambapo viuno katika nchi za kifalme vilizidi kuwa vikubwa.

Hamu zisizo za kiungwana

Kwa mujibu wa mwanahistoria wa Marekani Christopher E. Forth, muda wa mageuzi wa kuchukizwa na unene ulianza mapema mwishoni mwa karne ya ya 18 na 19 - wakati unene ulizidi kuhusishwa na hamu na starehe zisizo za kiungwana.

Waandishi katika ufalme wa Uingereza na Ufaransa walichukulia kuwa tamaduni zisizo za magharibi "zilivutiwa na walichokiona kuwa raia yoyote wa Ulaya angelikichukulia kuwa ni watu wanaotisha wasio na afya na wanaosababisha kichefuchefu," anasema Forth.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wasafiri waliotoka Ulaya kwenda Afrika kaskazini na magharibi wameeleza namna wanawake walivyonenepeshwa tayari kuozeshwa kiasi cha wao kushindwa kutembea.

Waturuki, jamii ya Eskimo, Aborigine kutoka Australia pamoja na Wachina na Wahindi walichukulia kuwa wanene kwa namna tofuati.

Ilihofiwa kwamba raia wa Ulaya wanaozuru maeneo hayo walikuwa katika hatari ya kuwa wanene pia.

Ishara ya kustawi

Kupanuka kwa ufalme wa Uingereza na Ufaransa kulichangia watu kuongeza kula. Biashara duniani ilipanuka na pia viuno au ukipenda matumbo.

Wanaume wa Uingereza wakapata umaarufu wa kuwana vitambi, na wageni waliofika Uingereza kutalii walitumai "kuona mwanamume wa Kiingereza aliye mnene akitembea mitaani," anasema Forth.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini katika miaka ya 1850, miili ya watu walio wastani na wenye nguvu kama wanamichezo ndio iliovutia nchini Ufaransa na Uingereza.

Fikra iliyokuwepo katika jamii za Ulaya ilikuwa ni kwamba watu katika jamii hizo walikuwa " ni wenye busara, walioweza kujizuia na kwahivyo walikula chakula kidogo na kuwana miili ya wastani," Strings anasema.

"Halafu tulikuwa na jamii za rangi tofauti na hususan Waafrika ambao walipenda ngono, chakula na kutokana na hilo walinenepa."

'Mzigo mzito'

"Ni mpaka wakati wa kuanza biashara ya utumwa na kuzua kwa sayansi ya rangi ndipo jamii ya watu wasiotoka mataifa ya magharibi walipochukuliwa kuwa na utofuati katika jamii kwa misingi ya utofauti wa miili na tabia zao ikilinganishwa na watu wa rangi nyingine," Strings anasema.

Na wakati mataifa ya magharibi yalipoanza kuziona jamii za watu wenye ragi tofuati kama suala la utafiti, walianza kuwaona kama kiburudisho - au pia kuwakejeli

Mojawapo ya mifano mizuri ya kuabishwa kwa watu wanene ni jamii ya Khoikhoi kutoka kusini mwa Afrika - waliosemekana kuheshimu makalio makubwa ya wanawake wao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sarah Baartman alitoka Kusini mwa Afrika na alizungushwa hadharani katika maonyesho mjini London na Paris katika karne ya 18

Sarah Baartman, alipata umaarufu duniani mwishoni mwa karne ya 18.

Alipelekwa Ulaya kwa kudanganywa na daktari wa Uingereza na alizungushwa katika maonyesho mjini Londona na Paris huku umati wa watu ukikaribishwa kumtazama na pia kumgusa makalio yake.

Baartman alifariki mnamo 1815 lakini ubongo, mifupa ya mwili wake na sehemu zake za siri zilionyeshwa katika jumba la ukumbusho Paris hadi mwaka 1974, makumbusho ya unyanyasaji wa kikoloni na ubaguzi wa rangi.

'Kipendacho roho'

Strings anaamini kuwa unene 'haupongezwi au haushutumiwi' lakini maana yake umeshikana na 'rangi ya mmiliki wake'.

Rangi sio suala la pekee kuhusu kupalilia aibu dhidi ya unene. Mengine ni dini na tabaka.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rangi dini na tabaka ndio mambo yaliyopalilia aibu dhidi ya unene

Kadri muda ulivyosogea, unene ulihusishwa na weusi na kutisha, na wembamba ukapendelewa na wanawake wenye asili ya Ujerumani na England.

Kwahivyo wakati aibu dhidi ya unene imekuwepo kabla ya utawala wa matiafa ya Ulaya, ilisaidia kushinikiza fikra na ubaguzi wa rangi.

Aibu ya kuwa mnene

Fikra hizo hazikuwa na umaarufu siku hizo, lakini ziliacha kovu anasema Strings. Wanawake weusi zaidi wanaendelea kuabishwa kwa ukubwa wa miili yao.

Nchini Marekani Strings anasema watu wengi hawaendi kumuona daktari kwasababu wanahisi kupuuzwa na wanaamini kuwa tatizo lolote la afya litahusishwa na uzito wa miili yao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Huenda ukawa mojawapo ya wachezaji tenisi waliofanikiwa katika historia na bado wakakabiliwa na aibu au chuki dhidi ya umbo lako

Hata Serena Williams - mmoja wa wachezaji tenisi waliofanikiwa katika historia - amelizungumzia suala hilo, na kuwahi kuwaambia wakosoaji wake kuwa: "Ninaweza kupunguza kilo 9 na bado nitaendelea kuwa na matiti makubwa na nitaendelea kuwa na makalio haya na hivyo ndivyo ilivyo."

Wakati ni kweli kuna sababu ya kuwepo wasiwasi kuhusu ukubwa wa kupindukia, Strings anakosoa kipimo cha body mass index (BMI) kama njia ya kubaini uzito wenye afya, akifafanua kuwa inachangia unyanyapaa dhidi ya watu wanene.

Anaamini masuala halisi - ikiwemo upatikanaji wa lishe bora kwa kila mtu - hayajashughulikiwa.