Vifo Essex: Je kuna ulinzi wa kutosha katika bandari za Uingereza?

Afisa mbele ya Lori

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Polisi akiwa amesimama mbele ya Lori

Polisi wanafanya kazi ya kutambua miili ya watu 39 waliokutwa kwenye Lorry Essex.

Inaelezwa Lori hilo liliingia nchini Uingereza likitokea bandari ya Zeebrugge, njia inayofahamika ya kupitisha magendo.

Kwa nini baadhi ya bandari hazidhibitiwi?

Ni moja kati ya bandari kadhaa ''ambazo hazina pilika pilika nyingi'' ambayo kwa mujibu wa shirika la kupambana na uhalifu, watu wanaofanya biashara ya magendo wamekuwa wakitumia mara nyingi. Bandari nyingine zilizobainishwa ni pamoja na Tilbury ambayo iko Essex na Hull.

Bandari nyingine ndogo ndogo na maeneo ya kutua ndege kwa kawaida hayalindwi.

Wataalamu wa maswala ya doria kwenye maeneo ya mipaka wanasema idadi ndogo ya rasilimali watu ikiwemo wanaokagua magari pia ni sababu inayochangia.

Namna gani watu huingia Uingereza kinyume cha utaratibu?

Tangu kufungwa kwa kambi ya wahamiaji nchini Ufaransa, mwaka 2016-2017, kumekuwa na majaribio yanayofanywa na watu kuingia Uingereza

Lakini majaribio hayo huratibiwa na watu wanaoongoza makundi ya uhalifu, kwa mujibu wa Taasisi inayopambana na uhalifu Uingereza (NCA)

Vitendo hivyo huhusisha kusafirisha watu kwenye makontena na magari kama ilivyokuwa kwenye Lori lililopatikana Essex.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Afisa wa kikosi kinacholinda mpakani

Jinsi gani watu huingia kinyume cha sheria?

Idadi kamili ya watu wanaoingia Uingereza kinyume cha sheria, ni vigimu kutambua kutokana na hali halisi ya mazingira.

Vikosi vya polisi hukusanya idadi ya watu wanaowakamata kwa kuingia nchini humo, lakini sio mara zote ripoti zao huwekwa hadharani .

Hata hivyo, uchunguzi wa BBC umebaini kuwa kulikuwa na watu 27,860 waliokamatwa kwa makosa ya kuingia nchini Uingereza kinyume cha sheria kati ya mwaka 2013 na Aprili 2016.

Katika kipindi hicho hicho, kulikuwa na visa 2,482 vya kukamatwa kwa watu waliokuwa wakiwasaidia watu wengine kuingia nchini humo kinyume cha sheria.

Watu 300,000 mpaka 900,000 walikadiriwa kuishi Uingereza kinyume cha sheria.

Kutokana na changamoto za kupata takwimu za kuaminika serikali haijatoa takwimu mpya tangu katikati ya miaka ya 2000, Ofisi ya taifa ya takwimu ilieleza mwezi Juni.

Maelezo ya video,

Wahamiaji wa Afrika wanaosafiri katika msitu hatari kujaribu kuingia Marekani.

Wahamiaji wangapi wamepoteza maisha wakiwa safarini Uingereza?

Kabla ya tukio hili, watu watano walikutwa wamekufa kwenye kontena au kwenye malori nchini Uingereza, tangu takwimu zilipoanza kukusanywa mwaka 2014.

Inadhaniwa kuwa walikufa walipokuwa wakiingia Uingereza kinyume cha sheria.

  • 2014: Raia wa Afghanistan alikutwa amekufa kwenye gati ya Tilbury, huko Essex. Alikua kwenye kontena ya mizigo sambamba na raia wengine 34 wa Afghanistan ambao walikuwa hai.
  • 2015: Wahamiaji wawili walikutwa wamekufa kwenye kasha lilitengenezwa kwa mbao katika bohari moja mjini Staffordshire.Kasha hilo lilisafirishwa kwenye kontena kutoka Italia.
  • 2016: Mwili wa mtu mmoja ulikutwa kwenye Lori lililokuwa limesafiri kutoka Ufaransa.

Umoja wa Mataifa unakisia kuwa watu 491 wamepoteza maisha au kupotea walipokua wakielekea ulaya mwanzoni mwa mwaka 2014.

Sababu ya vifo hivyo mara nyingi ni ajali za barabarani na kwenye treni. karibu watu 10 wamepoteza maisha kwenye maeneo ya kuingilia kwenye njia za Treni.

Idadi hiyo ilikusanywa na taasisi zisizo za kiserikali, mashirika ya kimataifa na ripoti za vyombo vya habari. Lakini hawajumuishi vifo kwenye kambi za wahamiaji au vituo wanavyowashikilia, na wala hawajajumuisha idadi ya watu inayokadiriwa kuwa 18,500 waliopoteza maisha au kupotea, wakivuka bahari ya Mediterania.