Ripoti ya Mueller: Uchunguzi wa madai ya jinai yanayomuhusisha Trump na Urusi waanza

William Barr

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Tathmini ya William Bar ya uchunguzi wa Muller imegeuka kuwa uchunguzi wa ugalifu

Mahakama nchini Marekani imeanzisha uchunguzi wa uhalifu juu ya uchunguzi wa awali wa Mueller, vimeripoti vyombo vya habari vya Marekani.

Tathmini ya kiutawala juu ya uchunguzi wa baraza maalumu juu ya uingiliaji wa uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 ulianza mwezi Mei.

Lakini uchunguzi wa awali kugeuzwa na kuwa uchunguzi wa jinai inamaanisha kwamba wachunguzi wanaweza kuagiza watu wafike mahakamani kutoa ushahidi na kutolewa kwa nyaraka kwa ajili ya kesi.

Rais Trump kwa muda mrefu amekuwa akidai ripoti za uchunguzi za Robert Mueller za kula njama na Urusi ni za 'hila' ".

Unaweza pia kusoma:

Uchunguzi kuhusu uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016 wa Marekani haikubaini kuwepo kwa njama zozote za kiuhalifu baina ya utawala wa Moscow na kampeni ya Donald Trump mwaka huo. Lakini haikumuondolea Trump kosa la kukwamisha sheria kuchukua mkondo wake.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Kwa muda mrefu Trump amekuwa akidai kwamba baraza maalum la uchunguzi huo ni "hila".

Ripoti juu ya uchunguzi wa uhalifu kwa mara ya kwanza ulichapishwa katika gazeti la New York Times.

Haijawa wazi juu ya uhalifu unaoweza kujitokeza chini ya uchunguzi huo, lilisema gazeti hilo.

Ni kwanini ripoti ya Mueller inachunguzwa?

Tathmini ya kiutawala kuhusu uchunguzi uliofanywa na Mueller ulianza mwezi May. Tathmini hiyo inasimamiwa na Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr na kuendeshwa na Mwendesha-mashtaka mkuu wa Marekani John Durham.

Bwana Durha alipewa jukumu la kubaini ikiwa ukusanyaji wa taarifa za kijasusi kuhusu kampeni ya mwaka 2016 ya Bwana Trump ilikuwa ni ya kisheria. Anaheshimiwa na wengi na anatambuliwa kwa kuwa na uhusiano wa kiuchunguzi na maafisa wa FBI , uhalifu uliopangwa na kuchunguza kuingiliwa kwa video za upelelezi wa mahojiano za CIA.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uchunguzi wa Robert Mueller umechukua takribani miaka miwili

Mwezi Aprili mwaka huu , Bwana Barr aliwaambia wajumbe wa baraza la Congress kwamba anaamini "upelelezi ulifanyika " juu ya kampeni ya Trump mwaka 2016, akiongeza kuwa: "Swali ni ikiwa ulipangwa vya kutosha . Na sisemi kwamba haukupangwa vya kutosha . Lakini ninahitaji kuchunguza hilo ."

Wakosoaji wanamtuhumu Bwana Barr kuanzisha tathmini ya kiutawala hasa zaidi kwa malengo ya kumtafuta rais kuliko kwa ajili ya maslahi ya kisheria.

Katika taarifa ya pamoja , wenyekiti wa mahakama na kamati za uhasusi walisema taarifa za uchunguzi wa uhalifu "ziliibua hofu mpya kwamba idara ya mahakama chini ya Mwanasheria Mkuu Barr imepoteza uhuru wake na inatumika kama chombo cha kulipiza kisasi kisiasa dhidi ya rais Trump ".

Wabunge wa Democrats, Jerry Nadler na Adam Schiff, amesema kuwa hatua hiyo inaweza kuleta "matatizo mapya ambayo hayawezi kusahihishwa " kwa utawala wa sheria.

Rais Trump anasema wakati huo hakumuagiza Bwana Barr kuanzisha tathmini ya uchunguzi wa kiutawala , lakini aliongeza kuwa "nilijivunia sana mwanasheria wetu mkuu " na ilikuwa ni "kitu kizuri sana ambacho alikifanya ".

Awali Bwana Trump aliwashutumu wapelelezi wa FBI ambao wao ndio walikuwa wakwanza kuanzisha uchunguzi juu ya uhaini katika kampeni za uchaguzi.

Ni nini tunachokifahamu?

Hadi sasa, idara ya mahakama, haijaweka wazi ni uhalifu gani unachunguzwa.

Pia haijawa wazi ni kwanini uchunguzi huu umeanza sasa, au umesababishwa na nini.

Na kwa kuwa idara yenyewe ya mahakama ndiyo iliyomchagua Robert Mueller kuchunguza uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016, uchunguzi huu wa uhalifu unamaanisha kuwa idara hiyo inaweza kuwa inajichunguza yenyewe.

Je riport ya Mueller ni nini?

Ripoti ya Muller kurasa 448- haijasema kuwa kulikuwa na njama za uhalifu baina ya Moscow na kampeni ya Trump zilizolenga kushawishi uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 2016

Hata hivyo ilielezea mifano 10 ambapo kulikuwa na uwezekano wa Bwana Trump kujaribu kuvuruga uchunguzi.

Ripoti hiyo ilisema kwamba Urusi iliingilia katika uchaguzi kwa mtindo wa "uliopangwa na haraka".

Uingiliaji huo ulifanyika kwa mtindo wa kampeni ya kando iliyopitia mitandao ya kijamii na udukuzi wa faili za kompyuta za chama cha Democrat uliofanywa na idara ya ujasusi ya jeshi la Urusi ilisema ripoti hiyo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Trump mara kwa mara amekana kuwa ushirikiano wowote na Urusi.

Nyakati za matukio muhimu katika uchunguzi wa Mueller

  • Septemba 2016: Wajumbe wa Kamati ya bunge ya Ujasusi walitangaza kuwa Urusi inafanya'' juhudi kubwa kuwa na ushawishi katika uchaguzi wa Marekani
  • Mei 2017: Naibu mwanasheria Mkuu wa Marekani alimteua Robert Muller kama mkuu wa baraza kuu la kuchunguza uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na madai yoyote kuhusu uratibu wa kampeni ya Trump
  • Disemba 2017: Mshauri wa zamani wa usalama wa taifa Michael Flynn alikiri kutoa taarifa za uongo kwa FBI kuhusu mikutano na balozi wa Urusi wiki kadhaa kabla ya rais Trump kuwa rais.
  • Agosti 2018: Mkuu wa zamani wa kampeni ya Trump Paul Manaford ilipatikana na hatia ya ufisadi. Alikubali kushirikiana na uchunguzi wa Mueller katika mwezi uliofuatia.
  • Novemba 2018: Rais Trump aliwasilisha majibu ya maandishi kujibu maswali ya baraza maalumu, siku kadhaa baada ya kumfuta kazi Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions
  • Disemaba 2018: Wakili binafsi wa Bwana Trump Michael Cohen alihukumiwa kifungo cha miezi 36 jela kwa kulidanganya baraza la congress, kukwepa kulipa kodi na kukiuka matumizi ya pesa za kampeni
  • Machi 2019: Mwanasheria Mkuu William Barr alipokea ripoti maalumu. Hakuitangaza moja kwa moja, lakini alitangaza muhtasari Robert Muller aliikosoa akiitaja kuwa yenye kutokuwa na ''dhana kamali''
  • Mei 2019: Robert Mueller alisema kuwa hotuba yake kwa umma kwamba ripoti yake hailaumu Trump, na akatangaza kujiuzulu kwake
  • Julai 2019: Muller alifika mbele ya baraza la Congress na akasisitiza kuwa ripoti yake haimtii hatiani Bwana Trump