Harvey Weinstein mzalishaji filamu wa New York akemewa na wanawake

Weinstein amekuwa kishutumiwa kwa makosa kadhaa ya unyanyasaji wa kingono, shutuma ambazo anakanusha

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Weinstein amekuwa kishutumiwa kwa makosa kadhaa ya unyanyasaji wa kingono, shutuma ambazo anakanusha

Wanawake kadhaa walizomewa na kuombwa waondoke walipokuwa wakilumbana na mzalishaji filamu mashuhuri wa muda mrefu Harvey Weinstein katika tukio moja mjini New York.

Gwiji huyo wa filamu alikuwa katika hadhira katika onyesho la vipaji vinavyoibukia wakati mchekeshaji Kelly Bachman alipomkosoa jukwani.

Weinstein amekuwa kishutumiwa kwa makosa kadhaa ya unyanyasaji wa kingono, shutuma ambazo anakanusha.

Bachman alijitambulisha kama "ndovu ndani ya chumba " na "Freddy Krueger" alipokuwa akizungumza katika tukio hilo.

Mwakilishi wake alisema kuwa tabia ya wanawake ilikuwa ni "ujeuri" na "isiyokubalika".

Unaweza pia kusoma:

"Sikujua kuwa lazima tulete filimbi za ubakaji katika muda wa Mchezaji filamu ," Bachman anaonekana katika picha ya video iliyotumwa kwenye mtandao wa Instagram.

Alizomewa na akaambiwa anyamaze kimya na hadhira, ambayo alijibu: "Samahani ,hilo liliuliwa katika kikundi cha usaidizi wa kisaikolojia kwa wahanga wa ubakaji ."

Hata hivyo, baadhi ya watu katika hadhira, walishangilia tena na kumpigia makofi.

Baada ya tukio hilo, Bachman aliliambia gazeti la Guardian kuwa "alihisi kana kwamba hapakuwa na pumzi ya kutosha katika chumba " alipozungumzia kumuhusu Weinstein jukwaani.

Unaweza pia kusoma:

Mchekeshaji mwenza Amber Rollo na mchezaji filamu Zoe Stuckles anaripotiwa kuelekea katika meza ya Weinstein wakati wa tukio upande wa mashariki mwa mji.

"Hakuna mtu yeyote atakayesema chochote?" Stuckles alipiga mayowe huku akiangalia upande wa mchezaji filamu- ambaye alikuwa ameketi na walinzi kabla ya yeye na Rollo kuamrishwa kuondoka.

Ukanda wa video wa malumbano hayo baadae ulitumwa kwenye ukurasa wa Facebook na kutolewa tena na gazeti la The Guardian.

Baadae Rollo alituma ujumbe wa twitter kwamba alimuita "jitu" na akamwambia anapaswa "kupotea".

Weinstein alikuwa ameonekana mara chache hadharani tangu kuenea kwa madai ya unyanyasaji wa kijinsia yalipotolewa dhidi yake, yaliyosababisha kuanza kwa vuguvu la #MeToo au #Mimi pia.

Katika taarifa yake, afisa matangazo wa mzalishaji Juda Engelmayer alisema : "Harvey Weinstein alikuwa amekwenda kuburudika na marafiki zake kwa muziki na kujaribu kupata faraja katika maisha yake ambayo imevurugwa.

"Tukio hili halikutarajiwa , ni la kikatili na mfano wa namna mchakato ulivyopingwa leo na umma, kujaribu kuupeleka mbali na mahakama pia ."

Harvey Weinstein mwenye umri wa miaka 67-kwa sasa amepewa dhamana na anatarajiwa kurudi mahakamani kwa ajili ya kesi dhidi yake mwezi Januari mjini New York kuhusu madai ya ubakaji