Boeing 787- 800 Dreamliner: Tanzania yapokea ndege ya pili aina ya Dreamliner

  • Abdalla Seif Dzungu
  • BBC Swahili
Ndege aina ya Dreamliner ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kutoka Marekani

Chanzo cha picha, Ikulu ya rais Tanzania

Tanzania imepokea ndege nyengine kubwa aina ya Boeing 787 Dreamliner kutoka nchini Marekani.

Ndege hiyo ilipokewa na rais John Pombe Magufuli aliyewaongoza mamia ya Watanziania katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere .

Ndege hiyo ni ya saba kati ya 11 zinazotarajiwa kununuliwa na serikali kufikia mwaka 2022.

Chanzo cha picha, Ikulu ya Tanzania

Uwezo wa ndege ya Dreamliner 787

Inabeba uwezo wa kubeba jumla ya abiria 262

Ndege hiyo pia ina uwezo wa kubeba uzito wa tani 227. Uzito huo unajumuisha chombo, mizigo na mafuta. Sifa yake ni kwamba ina uwezo wa kuhimili hali nzito ya hewa ikiwa kwenye umbali mrefu kwenda juu.

Inabeba Lita 101,000 za mafuta na ukubwa wa mita 56.72 sawa na nusu ya uwanja wa mpira wa miguu.

Vilvile ndege hiyo ina uwezo wa kutembea kilomita 13620 sawa na saa zaidi 12 hewani bila ya kusimamia

Chanzo cha picha, Ikulu ya Rais

Chanzo cha picha, Ikulu ya Tanzania

Akiwahutubia wananchi muda tu baada ya kutua kwa ndege hiyo , rais Magufuli ameelezea furaha yake ya kufanikiwa kwa mpango wa kuimarisha usafiri wa anga baada ya serikali hiyo ya awamu ya tano kununua ndege hizo.

Alisema: Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kuwa ndege hizo zimenunuliwa kutokana na fedha na kodi zao. kwa hivyo fedha zenu zinajulikana hadi kule marekani.

Magufuli Vilevile ameupongeza usimamizi wa shirika la ndege la ATCL kwa kazi nzuri.

Chanzo cha picha, Ikulu ya Tanzania

Awali katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi Dkt Leonard Chamuriho amesema kwamba shirika hilo linatarajia kuwa na ndege mpya tisa zikiwemo nne aina ya Bombadier Q400, ndege tatu za masafa ya kati ya Airbus A220-300 na nyengine mbili kubwa za masafa marefu ambazo ni Boeing 787 Dreamliner.

Ndege ambazo zimewasili nchini Tanzania kufikia sasa:

1. Ndege 2 aina ya Boeing 787-8

2. Ndege moja aina ya Forker 50

3. Ndege 3 aina ya Bombardier Dash 8-400

4. Ndege nyengine moja aina ya Bombardier Dash 8-300

5. Ndege 2 aina za Airbus A220-300 Zipo