Kanye West: 'Mimi ni msanii mkubwa kuliko wote'

Chanzo cha picha, Getty Images
Msanii Kanye west akitumbuiza jukwaani Coachella
Kama kuna kitu ambacho mwanamuziki wa Marekani wa miondoko ya Rap Kanye West anajivunia kuwa nacho ni kujiamini.
Aliwahi kujiita "mbunifu wa hali ya juu" na kuongeza kuwa "muziki wake ni bora", bila kusahau kutaja wakati mmoja alisema ana mpago wa kugombea kiti cha urais wa Marekani.
Katika mahojiano yake ya mwisho na mtangazaji wa, with Beats 1, Zane Lowe, aliangazia brand ya muziki wake.
Hakuzungumzia filamu za ngono tu, bali pia aligusia masuala ya kidini na kuongeza kuwa: "Anaamini yeye ndiye msanii bora zaidi duniani."
"Yaani hilo halina mjadala tena." alisema.
Anaagazia suala la dini katika kila nyimbo zake na pia kila Jumapili ,ameanzisha ibada yake binafsi ambayo inahudhuriwa na waalikwa pekee, na inayojumuisha mchanganyiko wa miziki tofauti ya injili na kwaya ya kidini.
Chanzo cha picha, Getty Images
Kanye akiimba katika Ibada ya Jumapili ya Tamasha la mwaka huu la Coachella
Albamu yake mpya-ambayo aliiachia siku ya Ijumaa - inafahamika kama Jesus is King, kumaanisha Yesu ni Mfalme na ameaahidi kutoa albamu nyingine kwa jina Jesus is Born-yaani Yesu Amezaliwa msimu wa Krismasi.
Kanye anasema kuwa amewashauri baadhi ya waanii wenzake wasijuhusishe na ngono kabla ya kuoa au kuolewa wakati wanapoanda albamu zao.
"Watu wengine wanajiingiza katika dawa za kulevya, na mimi nilizama katika uraibu wangu, ambao ulikuwa ngono," alisema akizungumzia jinsi alivyojiingiza katiaka uraibu wa filamu za ngono baada ya kupata jarida la ngono la Playboy la baba yake akiwa na umri mdogo.
Kando na muziki, moja ya biashara zake ni brand ya nguo ya Yeezy, ambayo ilijumuishwa katika wiki ya mitindo ya Paris.
Chanzo cha picha, Getty Images
Watu walivutiwa sana na ushirikiano wa mtindo wa mavazi kati ya Yeezy na Adidas
Kanye alizungumzia mpango wa kuleta "viwanda Amerika", kuwaajiri wafanyikazi katika kawanda chake cha Yeezy kupitia mfumo wa mageuzi katika idara ya magereza.
Alizidi kujigamba kuwa, "Mungu anamtumia yeye kujiunesha".
"Nebuchadnezzar alikuwa mfalme wa Babeli, na alitazama ufalme wake na kusema "Nilifanya hivi"
"Vinafanana, sivyo? Nimesimama juu ya mlima nikizungumzia Yeezus nikisema 'Nilibuni hiki. Mimi ni Mungu.'"
Mlima anaoashiria ni muundo wa jukwaa la jinsi Yeezus katika maonesho ya mwaka 2013/14, amabayo pia ilionesha mtu aliyefanana na Yesu akitokea jukwaani.
Chanzo cha picha, Getty Images
Kanye akitumbuiza katika tamasho moja nchi Australia
Alizungumzia gharama ya muundo wake wa ubunifu kwenye ziara, akisema kuwa "hakutengeza fedha zozote" kutoka kwa maonesho ya Yeezus, japo iliripotiwa kumuingizia takribani dola millioni 25, na kutajwa kuwa pato jumla la pili kwa ukubwa mwaka 2013, baada ya Paul McCartney.
Kanye pia alizungumzia uhasama wa zamani kati yake na msanii Drake akisema anataka kuangazia masuala yenye "nguvu chanya".
Aliendelea kusema kuwa wakati mwingine anamtembelea Drakes nyumbani kwake, lakini habishi mlango kwasababu hataki kumsumbua, badala yake anawaachia walinzi wa Drake nambari yake ya simu.
"Huwezo kumtumikia Mungu na kumwekea chuki ndugu yako."

Utajiri wa Jay-Z umetokana na nini?
Ni rasmi Jay-Z ndiye bilionea wa kwanza wa muziki wa hip hop ,limetangaza jarida la Forbes , baada ya kujijengea ufalme kutokana na muziki, mali, fasheni na uwekezaji