Tanzania kwa miaka mingi imekuwa katika ramani nzuri hasa kwenye uhuru wa kujieleza, lakini sasa hali ikoje?

Tanzania kwa miaka mingi imekuwa katika ramani nzuri hasa kwenye uhuru wa kujieleza, lakini sasa hali ikoje?

Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums Maxence Melo Mubyazi ameiambia BBC kuwa Tanzania kwa miaka mingi imekuwa katika ramani nzuri ya hasa kwenye uhuru wa kujieleza na suala la amani na uhuru wa demokrasia. Lakini kwa miaka mitano iliyopita, anasema katika kanda ya Afrika mashariki ilikuwa ikiongoza katika masuala ya uhuru wa kujieleza lakini sasa taifa hilo linaangalia Kenya kama mfano.