Mafuriko: Tahadhari za madhara yatokanayo na majanga ya mvua

Mafuriko: Tahadhari za madhara yatokanayo na majanga ya mvua

Mkoa wa Tanga, kaskazini mwa Tanzania ndio uliothirika zaidi na mvua za vuli ambazo zimenyesha kwa siku kadhaa katika ukanda wa Afrika mashariki.

Mvua hizo zimesababisha vifo vya vya watu kumi na tano mkoani humo na kukata mawasiliano ya barabara kwenda mikoa ya jirani kama Arusha Kilimanjaro na nchi jirani ya Kenya.

Je wananchi wanawezaje kuchukua tahadhari za madhara yatokanayo na majanga, kwa kutolea mfano mvua zinazoendelea kunyesha baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki zilivyoleta maafa na athari za kiuchumi na kijamii?

Mwandishi wa BBC Scolar Kisanga amezungumza na mtaalamu wa masuala ya Majanga nchini Tanzania James Mbatia.

wananchi wanavyoweza kuchukua tahadhari za madhara yatokanayo na majanga