Mfahamu mbwa wa kikosi maalum cha Marekani aliyesaidia kumuua Abu Bakr al-Baghdadi

Afisa wa jeshi maalum aliyesaidoia kuuawa kwa Abu bakr al-Baghdadi

Kiongozi mkuu wa Islamic State Abu Bakr al-Baghdadi, ameuawa kufuatia mashambulio katika eneo la kaskazini mwa Syria yaliotekelezwa na kikosi ,maalum cha Marekani kulingana na rais Donald Trump.

Rais huyo anasema kwamba Baghdadi alitorokea chini ya handaki baada ya wanajeshi kuingia katika nyumba nyake ambapo alidaiwa kuwachukua watoto watatu kabla ya kujilipua ndani ya handaki hilo.

Kulingana na rais Trump Abu Bakr al- Baghdadi ambaye alikuwa akisakwa sana na Marekani alifukuzwa na mbwa huyo wa jeshi la Marekani hadi mwisho wa handaki hilo .

Lakini je mbwa huyu alikuwa na jukumu gani katika operesheni hiyo?

Mbwa huyo ni afisa mwenye mafunzo na ana uwezo wa kubaini vilipuzi na vitu vingine.

Mwanajeshi mstaafu wa Marekani ambaye sasa ni kiongozi wa kampuni ya kufunza mbwa Ron Aiello , aliambia gazeti la The New York Times kwamba mbwa huyo bila shaka atavutia hamu ya wengi.

Baada ya uvamizi uliosababisha mauaji ya Osama bin laden 2011 utambulisho wa mbwa kwa jina Cairo aliyesaidia kundi la wanamaji walioingia katika eneo la nyumba ya kiongozi huyo wa al-Qaeda , mbwa huyo aina ya Belgian malinois, alivutia hamu ya wengi waliotaka kumjua.

Aiello, aliambia The New York Times kwamba mbwa huyo ana uwezo wa kubaini vilipuzi na anaweza kushiriki katika operesheni za vikosi vya makomando.

''Iwapo jeshi la Marekani linatekeleza operesheni, wanahitajika kunusa milipuko ili isifanyike'', alisema bwana Aiello.

Mbwa kama hao wana mafunzo ya hali ya juu , wanaweza kutekeleza mashambulizi mbali na kumuua mtu kwa dakika moja tu.

Rais Trump alizungumzia kuhusu mbwa huyo na kusema kwamba alifanya kazi ngumu ya kumnasa na kumuua Abu bakr al Baghdadi.

Gharama za mbwa huyo

Bei ya mbwa mmoja ambaye hana leseni inadaiwa kuwa zaidi ya $25,000 na kwamba wanaingiliana na vifaa vya kijeshi kama vile fulana zisizoweza kuingia maji, kamera na taa zinazomuelekeza mbwa wakati wa operesheni inayoendelea.

Gazeti la Bloomberg limeripoti kwamba mmoja ya mbwa waliofunzwa aina ya K-9 anamiliki vifaa vyenye thamani ya $ 283, 000.

Mbwa huyo ametajwa kuwa mrembo na mwenye kipaji na rais Trump.

Rais huyo alimpongeza mbwa huyo kwa ujasiri wake na kusema hakuna hata mwanajeshi mmoja aliumia wakati alipotangaza kifo cha kiongozi huyo wa IS siku ya Jumapili.

''Walitumia nguvu kuingia katika nyumba hiyo, ni vyema kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa''.

'Na ndio sababu mbwa huyo alifanya kitu kikubwa sana'.

Alijeruhiwa katika uvamizi huo

Mbwa huyo alijeruhiwa baada ya kiongozi huyo wa IS kujilipua pamoja na watoto watatu.

Rais Trump alisema kwamba Baghdadi alitoroka na kufika mwisho wa handaki alilokuwa akilia na kupiga mayowe, alipokuwa akifukuzwa na 'afisa' huyo wa kijeshi.

Jenerali Mark Milley , mwenyekiti wa majeshi yote alisema kwamba Malinois alijeruhiwa kidogo lakini anaendelea kupona, na kwamba mbwa huyo alifanya kazi nzuri sana.

Chanzo cha picha, UBALOZI WA MAREKANI TANZANIA

Ni mbwa jasiri

Kulingana na klabu ya Marekani ya Kennel , mbwa wa Malinois wana nguvu , ni werevu, na wanaweza kujifunza na kufanya mambo taofauti - swala ambalo ni muhimu sana wakati wa operesheni.

Hutumika sana na jeshi pamoja na maafisa wa polisi duniani ili kuelekeza na kuvilinda vikosi , kuwatafuta wanajeshi wapinzani, pamoja na vilipuzi kutokana na maadili ya kazi yao na weruvu.

Hii sio mara ya kwanza mbwa kama huyo amejiunga na jeshi la Marekani katika operesheni ya kiwango cha juu.

Pongezi za twitter

Picha ya mbwa huyo ilizua hsia kali katika mitandao.

Kampuni ya Twitter ilikuwa ya kwanza kujitokeza na kutoa pongezi hizo, huku baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Twitter wakitumia fursa hiyo nao kuwapongeza mbwa wao.