Ethiopia: Fahamu kijiji cha kale cha juu ya mlima

Kijiji cha Shonke ni eneo la makazi ya juu ya mlima ambalo limekuwepo kwa takribani miaka 900 katika jimbo la Amhara nchini Ethiopia.Wenyeji wanasema kuwa wanapendelea kujenga nyumba zao kwa mawe yanayopatikana hapo. Wanasema kuwa na wanapenda kuishi katika kijiji hicho badala ya maeneo ya mjini nchini humo.