Twitter yapiga marufuku matangazo ya kisiasa

Mkurugenzi wa Twitter Jack Dorsey akiwa katika kongamano la "Tech for Good" mjini Paris, Ufaransa Mei 15, 2019.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Jack Dorsey amesema maelezo zaidi yatatolewa mwezi Disemba

Twitter imepiga marufuku matangazo ya kisiasa kote duniani, ikisema kuwa ujumbe kama huo ''haustahili kununuliwa.''

"Japo matangazo ya kibishara ya interneti ndio njia bora zaidi ya kuwasilisha ujumbe , ambao unaweza kuwa na madhara kisiasa,"mkurugenzi wa kampuni hiyo Jack Dorsey aliandika kwenye Twitter.

Washindani wa mtandao wa kijamii wa Facebook hivi karibuni walifutilia mbali mpango wa kupiga marufuku matangazo ya siasa ya kibiashara.

Taarifa ya marufuku hiyo imeibua mgawanyiko katika kambi za kisiasa nchini Marekani zinapojiandaa katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Brad Parscale,meneja wa kampeni ya Raisi Donald Trump, kugombea muhula wa pili, amesema marufuku hiyo ni jaribio jingine la kumnyamazisha Trump na wahafidhina".

Lakini Bill Russo, msemaji wa kampeni ya mgombea mkuu wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden, amesema: "Wakati uamuzi wa kuchagua kati ya faida inayotokana na matangazo ya kibiashara na uadilifu wa demokrasia yetu, inatia moyo sana kuona kwamba, kwa mara ya kwanza pato la kibiashara halitashinda"

Akizungumzia hatua hiyo, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg alitetea sera ya kampuni yake.

"Katika ulimwengu wa demokrasia, nadhani ni sawa kwa kampuni binafsi kudhibiti wanasiasa au habari," alisema akizungumza na wanahabari.

Marufuku ya Twitter itaanza kutekelezwa kuanzia Novemba 22, huku maelezo zaidi kuhusu suala hilo ikitarajiwa kutolewa Novemba 15.

Bwamna Dorsey alielezea msimamo wake katika ujumbe wa Twitter

Matangazo ya biashara ya kisiasa, alisema yamekuja "na changamoto mpaya kuhusu suala la elimu kwa Umma".

Changamoto hizo ni pamoja na ''Mfumo wa kutoa mafunzo ya kutumia mashine kutuma ujumbe, kulenga kundi fulani, kuchunguza habari za kupotosha na habari ghushi",

"Sio ya uhakika," aliandika, "kwetu sisi kusema: 'Tunafanya kazi kwa bidii kukomesha watu kutumia mtandao wetu kusambaza taarifa za kupotosha, lakini ikiwa mtu atalipa tangazo ili tuwalazimishe watu kuona tangazo lao la kisiasa…basi...wanaweza kusema chochote watakacho!'"

Ili kukabiliana na hija kwamba sera hiyo mpya huenda ikaonekana kuwanufaisha viongozi ambao tayari wako ofisini , alisema kuwa, "Vugu vugu za kijamii hufikia watu wengi bila kutumia matangazo ya kibiashara".

Matangazo ya biashara yaliyo na ujumbe wa kuwahamasisha watu kujisajili kama wapiga kura hazitaathiriwa na marufuku hiyo,aliongeza.

Taarifa ya marufuku hiyo imepokelewaje?

Hillary Clinton, mgombe uraisi wa zamani wa Democratic ambaye alishindwa na Bw. Trump katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016, amekaribisha hatua hiyo ya Twitter na ameonekana kuishinikiza Facebook kutafakari msimamo wake kuhusu suala hilo.

Mchambuzi wa mitandao ya kijamii Carl Miller, amesema ni "ni mara ya kwanza kampuni hiyo kubwa ya teknolojia kurudi nyuma katika katika masuala mazito ambayo imekuwa ikifanyia makampuni mengine ambayo hayafuati mkondo wake".

Sera ya Facebook inasemaje?

Mapema mwezi huu, Mark Zuckerberg alifika mbele ya jopo la wanafunzi mjini Washington DC kutetea hatua ya kampuni hiyo kupiga marufuku matangazo ya biashara yaliyo na ujumbe wa uwongo.

Alikuwa ametafakari wazo la kupiga marufuku matangazo yote ya siasa katika mtandao lakini akabadili nia hiyo kwa kuamini kuwa hatua hiyo ingeliwafaidisha wanasiasa walio madarakani na mtu yeyote ambaye vyombo vya habari vitaamua kumuangazia.

Kampuni hiyo inastahili "kuangazia pakubwa suala la kujieleza", alisema.

Chanzo cha picha, Facebook

Maelezo ya picha,

Bw. Zuckerberg akizungumza na na wanafunzi katika Chuo kikuu cha Georgetown mjini Washington DC

Hatua hii itakuwa na athiri kwa uchaguzi wa Marekani?

Kampeini za Marekani zinatarajiwa kutumia karibu dola bilioni sita lakini nyingi ya fedha hizo zinatumiwa kwa matangazo ya kibiashara ya televisheni na zingine karibu 20% zikitumumiwa katika matangazo ya biashara ya kidigitali, kwa mujibu wa kampuni ya utafiti wa matangazo ya biashara ya Kantar.

Maelezo ya video,

VIDEO: Jinsi matangazo ya biashara ya itakavyoathiri kampeni za siasa