Mabilioni ya watu wanatumia WhatsApp, lakini je mtandao huu ni salama?

Watumiaji walioathirika na mashambulio dhidi ya WhatsApp walikuwa na namba za siku kutoka nchi mbalimbali, mkiwemo Bahrain, Muungano wa nchi za kiarabu na Mexico, kulingana na mashtaka

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Watumiaji walioathirika na mashambulio dhidi ya WhatsApp walikuwa na namba za siku kutoka nchi mbalimbali, mkiwemo Bahrain, Muungano wa nchi za kiarabu na Mexico, kulingana na mashtaka

Kampuni ya Facebook inayomiliki mtandao WhatsApp imewasilisha mashtaka dhidi ya kampuni ya Israel NSO Group, ikwamba kampuni hiyo ilitengeneza na kusambaza programu ya ujasusi kwa watumiaji wa mtandao huo billioni 1.5

WhatsApp inaishutumu kampuni hiyo kwa kutuma programu hiyo kwa simu za mkononi zipatazo 1,400 kwa lengo la kuzipeleleza.

Watumiaji walioathirika ni pamoja na waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binadamu, wanasiasa wa upinzani na wanadiplomasia.

NSO Group, kampuni ambayo hutengeneza programu za upelelezi, imekanusha madai hayo.

Unaweza pia kusoma:

Katika kesi iliyowasilishwa mahakamani, WhatsApp ilisema kuwa NSO Group "ilitengeneza programu yake ya hila ili kufikia ujumbe na mawasiliano baada ya kuziunganisha kwenye vifaa walivyolengwa".

Imesema kuwa NSO Group ilibuni akaunti kadhaa za WhatsApp na kuwezesha alama za siri kuuunganishwa na hifadhi ya jumbe za WhatsApp katika miezi ya Aprili na Mei.

"Tunaamini shambulio hili lililenga wajumbe 100 wa mashirika ya kiraia , jambo ambalo ni ukiukaji wa sheria," ilisema WhatsApp katika taarifa yake.

Watumiaji walioathirika walikuwa na namba za siku kutoka nchi mbalimbali, mkiwemo Bahrain, Muungano wa nchi za kiarabu na Mexico, kulingana na mashtaka.

WhatsApp imesema kuwa inataka marufuku ya kudumu dhidi ya NSO itolewe na mahakama kutumia huduma zake.

Chanzo cha picha, Getty Images

WhatsApp inajinadi kama programu yenye mawasiliano " yanayolindwa" kwasababu jumbe zake huwa zimeunganishwa baina ya watu wanaowasiliana pekee.

Hii ikimaanisha kuwa mawasiliano huwa yanaweza kuonekana baina ya kifaa, mfano simu ya mtumaji na mpokeaji.

Je unaweza kuepuka udukuzi wa kimtandao?

Kulingana na mwandishi wa habari wa BBC kitengo cha digitali, Basillioh Mutahi, udukuzi na upelelezi wa data katika mitandao ya kijamii umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

Mutahi anasema mtumiaji wa Whatsap na mitandao mingine ya kijamii anaweza kuepuka udukuzi wa mawasiliano yake kwa kuepuka kubofya au kubonyeza katika kila ujumbe unaotumwa au kusambazwa kwake, hususan pale unapokuwa na chanzo ambacho mtumiaji hakifahamu.

''Mara nyingi utapata unatumia ujumbe ambao unasema bonyeza hapa utapata data au bando za bure, au unatumiwa kiunganishi (link) kinachokupeleka kwenye ukurasa mwingine, unapaswa kuwa makini na ujumbe wa aina hii kwasababu unapopelekwa kwenye ukurasa mwingine inawezekana data za simu yako au kompyuta yako zinachukuliwa na mtu mwingine ambaye anaweza kuzitumia kuingilia mawasiliano yako'' anasema Mutahi.

Maelezo ya picha,

Maeneo ya huduma za data za WiFi zinazotolewa kwa umma si salama kwa taarifa ama data za kibinafsi

Mutahi anasema njia nyingine ya kuepukana na udukuzi wa taarifa zako mtandaoni ni kuhakikisha unapokuwa na tarakimu mbili za siri (log in) za kuingia kwenye kurasa zako za mtandao, mtu anaweza kujiwekea mwenyewe kwenye kifaa chake cha mawasiliano.

Unapoweka mpango huu, mfano mtu anaweza kutaka kuingia kwenye mtandao wako kwa kutumia tarakimu yako ya siri (password), lakini kama umeweka mpango wako wa password mbili itakua ni vigumu kwani mpango wa pili utatuma tarakimu za siri kwenye simu yako ya mkononi kwa hiyo itakuwa ni vigumu kwa mdukuzi kuingia kwenye akaunti yako, anasema Mutahi.

Bwana Mutahi ambaye ni mwandishi wa taarifa za Kidigitali kwa muda mrefu anasema maeneo ya huduma za data za WiFi zinazotolewa bure kwa umma pia si salama kwa taarifa ama data za kibinafsi kwani mtoaji huduma hiyo huenda anatazama taarifa za watu walioingia kwenye mitandao.

Matumizi ya kompyuta zinazotumiwa na kampuni au na watu wengi kwa pamoja pia si salama anasema Mutahi, na kuongeza kuwa mtu mwingine anaweza kuingia katika akaunti yako ya WhatsApp kupitia kompyuta unayoitumia kupitia desktop.

''Kuna njia mtu anaweza kutumia kuingia kwa WhatsApp kupitia desktop''. Anasisitiza

Mtu anakutumia link inayokulazimu kubadili na wanakwambia imeexpire na kubadili password na unabadilisha na unakosa akaunti yako...Nilibadilisha nikapata sina link ya kupata.