Bilionea Mo Dewji azungumza na BBC kuhusu kutekwa kwake Tanzania

Bilionea Mo Dewji azungumza na BBC kuhusu kutekwa kwake Tanzania

Bilionea kijana barani Afrika na mfanya biashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu sakata lake la kutekwa nyara mwaka jana na kuelezea jinsi alivyotishiwa maisha yake.

Katika mahojiano maalum, Dewji, almaarufu Mo, amemueleza mtangazaji wa BBC Salim Kikeke kuwa kwa kipindi kizima, alihisi kwamba kuna uwezekano mkubwa hatoweza kutoka salama na kuwa mwisho wa maisha yake ulikua umekaribia.