Wanaume watano wameachiliwa baada ya 'kumbaka msichana aliyepoteza fahamu' Uhispania

Waandamanaji katika mji wa Malaga wanabeba mabango wakiunga mkono mwantiriwa wa Manresa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Waandamanaji katika mji wa Malaga wanabeba mabango wakiunga mkono mwantiriwa wa Manresa

Mahakama moja nchini Barcelona imewaachilia huru wanaume watano waliotuhumiwa kumbaka kwa zamu msichana wa miaka 14 kufuatia mashtaka ya unyanyasaji huo wa kingono.

Wanaume hao walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo jela kwa uhalifu wa unyanyasaji wa kingono.

Chini ya sheria za Uhispania , shtaka linaweza kuwa la ubakaji iwapo utumiaji nguvu ama vitisho vilitumika.

Mahakama iliamua kwamba hawakutekeleza ubakaji kwa kuwa mwathiriwa alikua katika hali ya kupoteza fahamu na kwamba hawakulazimika kutumia nguvu.

Uamuzi huo unajiri licha ya mahakama ya Uhispania kubadilisha uamuzi kama huo mapema mwaka huu. Pia kuna harakati ya kuirekebisha sheria hiyo.

Watu sita walikuwa wameshtakiwa wakati huo.

Watano waliokuwa wameshtakiwa walipatikana na hatia na kuhukumiwa kati ya miaka 15 hadi 20. Makundi ya haki za kibinadamu yametoa hisia kali na hasira kufutaia uamuzi huo.

Onyo: Baadhi ya wasomaji wanaweza kuona maelezo ya habari hii kuwa ya kuogofya.

Wanaume hao walipatikana na hatia ya kumnyanyasa msichana huyo katika kile kinachojulikana kuwa 'unywaji wa Bottelon' katika magofu ya kiwanda kimoja huko Manresa, mji uliopo kaskazini mashariki mwa jimbo la Catalonia mnamo mwezi Oktoba 2016.

Kesi hiyo ilijulikana kama 'Manada de Manresa' - Bustani ya Mbwa mwitu wa Manresa - ikilinganishwa na kesi nyingine ya 2016 ambapo msichana mmoja alibakwa kwa zamu hatua iliozua pingamizi huku sheria hiyo ikitarajiwa kuangazia upya.

Ni nini kilichotokea?

Waendesha mashtaka waliambia mahakama kwamba wanaume hao walimnyanyasa kwa zamu msichana huyo ambaye alikuwa ametumia dawa za kulevya na pombe.

Mmoja ya walalamishi , kwa jina Bryan Andes M alidaiwa kuwaambia wenzake : ''Ni zamu yako na kila mmoja atachukua dakika 15 bila kuchelewa''.

Awali katika kipindi cha kusikilizwa kwa kesi hiyo , msichana huyo alisema kwamba alikumbuka kidogo yaliofanyika na kwamba mmoja ya wanaume hao alikuwa akishikilia bunduki.

Washukiwa wote walikana madai hayo, licha ya kwamba vinasaba vya mmoja ya wanaume hao vilipatikana katika nguo ya ndani ya msichana huyo.

Mahakama iliamuru kwamba mwathiriwa hakujua kile alichokuwa akifanya na kila ambacho hakuweza kufanya, hivyobasi hakuwa na uwezo wa kukubali ama kukataa uhusiano wa kingono ambao alikua nao na washukiwa hao, kulingana na gazeti la El Paris.

Liliongezea kwamba washukiwa hao waliweza kushiriki naye ngono bila kutumia nguvu ama vitisho. Mahakama ilimfidia mwathiriwa pauni elfu 10,300.

Ni nini kilichotokea katika kesi ya bustani asili ya mbwa mwitu?

Mahakama katika mji wa Navarra iliwafunga watu watano kwa unyanyasaji wa kingono katika eneo la Pamplona dhidi ya mwanamke mwenye umri wa miaka 18 ambaye alipewa dawa za kulevya katika jumba moja.

Kwa kuwa alionekana kama mtu aliyekosa fahamu , kulingana na ripoti ya polisi, mahakama iliamua kwamba hakuna vitisho wala nguvu zilizotumika.

Mwezi Juni, mahakama ya Uhispania ilibadili uamuzi wake ikiamua kwamba lilikuwa kosa la unyanyasaji wa kingono na kwamba wanaume hao walikuwa wabakaji.

Watano hao waliongezewa hukumu yao ya miaka tisa hadi 15 .

Waziri mkuu wa Uhispania mwaka uliopita alibuni jopo la kuangazia upya sheria za ubakaji.