Mazungumzo yanayoongozwa na Marekani juu ya mto Nile si ya upatanishi, yasema Ethiopia

Bwawa hilo linalojengwa kaskazini mwa Ethiopia, litakuwa kituo kikubwa kabisa cha kuzalisha umeme barani Afrika. Haki miliki ya picha Getty Images

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Misri, Ethiopia na Sudan wako nchini Marekani mjini Washington DC kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ujenzi wa bwawa kubwa la maji kando ya mto Nile.

Bwawa hilo linalojengwa kaskazini mwa Ethiopia, litakuwa kituo kikubwa kabisa cha kuzalisha umeme barani Afrika.

Lakini Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa 80%, ina hofu kuwa bwawa hilo litaathiri mfumo wa usambazaji maji ambao nao una changamoto kadhaa.

Mazungumzo haya yatasimamiwa na Marekani kama msuluhishi baada ya msimamo uliotolewa na Misri na Ethiopia kwenye mazungumzo yaliyopita mazungumzo ambayo hayakuzaa matunda.

katikati ya mzozo huo ni mpango wa kujaza bwawa hilo kuu, Ethiopia inataka kutekeleza mpango huo kwa kipindi cha miaka sita, Misri ikipendekeza muda wa miaka kumi ikihofu mradi huo utafanya Ethiopia kudhibiti maji ya mto Nile.

Wiki iliyopita waziri wa Mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry alisema kuwa yanalenga kuvunja " mkwamo katika mazungumzo yanayoendelea ", liliripotishi shirika la habari la AFP.

Lakini Ethiopia hauutazami mkutano wa Washingoton kwa mtizamo huo . " Huu sio uwaja wa mazungumzo ya kiufundi ," Alisema msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeniya Ethiopia Nebiat Getachew katika mazungumzo na BBC.

"Lakini tutakwenda kule ... na pande zote husika katika mazungumzo zitaelezea msimamo wao. Haya sio mazungumzo na Marekani haifanyi upatanishi. Hiyo haiwezi kuwa lugha sawa."

Bwana Nebiat alisema kuwa mazungumzo ya upatanishi yanafanyika baina ya ''mawaziri wa maj'', ankiongeza kuwa suluhu la kiufundi linaweza kupatikana kwa ajili ya hofu za Misri

Mwezi uliopita Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliliambia bunge mjini Addis Ababa kwamba "hakuna msukumo unaoweza kuisimamisha Ethiopia" kuacha kujenga bwawa

"Ethiopia haina nia ya kuwadhuru watu wa Misri, wanahitaji kupata faida tu kutokana na bwawa'' aliongeza.

Unaweza pia kusoma

Mara baada ya kukamilika, bwawa hilo litakalokuwa na uwezo wa megawatt 6000 litakalogharimu pauni bilioni tatu, lakini ujenzi huo umeathiriwa na ucheleweshaji na haijafahamika kama litaanza kufanya kazi baada ya muda wa mwisho uliowekwa na serikali mwaka 2021.

Kutiwa saini kwa mkataba kuhusu ugavi wa maji

Misri, Ethiopia na Sudan zilitia saini mkataba wa kwanza kuhusu ugavi wa maji katika mto Nile unaopitia mataifa hayo yote matatu.

Mkataba huo unafuatia ujenzi unaoendelea wa bwawa kubwa linalojengwa na Ethiopia katika mto Nile.

Ujenzi huo ulizua mzozo mkali wa kidiplomasia kati ya Misri na Ethiopia.

Unaweza pia kusoma:

Viongozi wa mataifa hayo matatu,walikutana jijini Khartoum Sudan kwa sherehe ya kutia saini mkataba huo ambao umetajwa kama hatua ya kwanza katika kutatua mzozo huo.

Ethiopia inasema itaisaidia katika kuzalisha nguvu za umeme kwa ajili ya viwanda vyake na pia inatarajia kuuza kawi kwa mataifa jirani.

Mara kwa mara Misri imepinga mradi huo ikisema huenda bwawa la Rennaissance likapunguza viwango vya maji kwa raia wake.

Misri kwa upande wake inaamini kuwa ina haki za kihistoria za mto huo kufuatia mikataba ya mwaka 1929 na 1959, inayoipa asilimia 87 ya maji ya mto huo, na pia uwezo wa kupinga miradi yoyote inayojengwa katika mto Nile.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Wasiwasi wa Ethiopia na majirani kwa kujenga bwawa mto Nile

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii