Zaidi ya watu milioni 52 wanakabiliwa na baa la njaa Afrika

Mafuriko Somalia Haki miliki ya picha NRC.SMUGMUG.COM
Image caption Nchi 18 zimeathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi Afrika

Zaidi ya watu milioni 52 katika nchi 18 barani Afrika wanakabiliwa na baa kubwa la njaa, sababu ikiwa hali mbaya ya hewa, umasikini na migogoro kwa mujibu wa Oxfam.

Baadhi ya maeneo yana ukame kwa kipindi cha miaka minne huku nchi nyingine, ukame umefuatiwa na mafuriko makubwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na mabadiliko ya vipindi vya hali ya hewa vya kawaida.

Sehemu kadhaa za Zimbabwe walikuwa na mvua kidogo tangu waka 1981 hatua ambayo ilisababisha watu milioni 5.5 kukumbwa na baa kubwa la njaa.

Zambia ambayo ni mzalishaji mkubwa wa mahindi pia ilikumbwa na njaa hatua ambayo serikali ilichukua ni kuzuia uuzaji wa mahindi nje ili kusaidia watu milioni 2.3 waliokuwa wakikabiliwa na njaa.

Unaweza pia kutazama:

Nchi zilizoathirika

Hali hii ni mbaya kwa nchi kama Angola, Malawi,Msumbiji, Madagascar, Namibia na Zimbabwe.

Ukame umeathiri mashariki na eneo la pembe ya Afrika hasa Ethiopia,Kenya na Somalia, ikiharibu mazao na mifugo. Mazao ya nafaka katika baadhi ya maeneo yamepanda bei, gharama ambazo watu walio masikini wa vipato wanashindwa kumudu.

Karibu watu milioni saba barani Afrika wanaishi katika hatari kubwa zaidi ya kukumbwa na baa la njaa.

Wakati huohuo, joto la juu katika bahari ya Hindi imesababisha mvua kubwa nchini Kenya na Sudani Kusini, na kusabisha mafuriko makubwa.

Sudani Kusini ilitangaza hali dharura baada ya watu zaidi ya 900,000 kukumbwa na mafuriko.

Haki miliki ya picha NRC.SMUGMUG.COM
Image caption Somalia ni moja ya nchi zilizoathiriwa na baa la njaa

Oxfam imesema nini?

Kiri Hanks, Mkuu wa sera za masuala ya hali ya hewa wa shirikika la Oxfam amesema: ''Mamilioni ya watu ambao tayari ni masikini wanakumbwa na baa kubwa la njaa kutokana na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa ambayo huathiri jamii hizo ambazo ziko vibaya. Sehemu za Zimbabwe zimekuwa na kiwango kidogo cha mvua kwa miaka 38 wakati Sudani Kusini ikikabiliwa na mafuriko.''

Wanaoathirika zaidi na athari zake zaidi ni wanawake, wasichana na inawawia vigumu kurejea kwenye hali yao ya kawaida.

Oxfam inasema kuwa nchi 18 imeingia hasara zaidi ya dola milioni 700 kutokana na madhara yaliyotokana na hali ya hewa kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Jitihada zinazofanyika kujikwamua.

Hata hivyo inaelezwa kuwa kuna maendeleo hafifu kwenye zoezi la kuchangisha fedha ili kuzisaidia nchi ziweze kukabiliana na athari zilizotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Afrika inachangia chini ya asilimia tano ya uchafuzi wa hali ya hewa lakini inaathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.

Wakati maafisa wakikusanyika kuelekea kwenye mkutano wa mawaziri kuhusu masuala ya mazingira mjini Durban Afrika Kusini unaofanyika mwezi wa Novemba, Oxfam imewataka mawaziri wa nchi za kiafrika, kudai nchi za kiviwanda kutimiza ahadi zao kuepuka gharama zinazoongezeka za kukabiliana na madhara.

Oxfam kwa sasa inawasaidia watu zaidi ya milioni saba katika nchi 10 zilizoathiriwa zaidi kwa kuwapa chakula na maji, na mradi huu wa muda mrefu ni kwa ajili ya kuwasaidia watu waweze kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa. Inajaribu kuchangisha pauni milioni 50 kwa ajili ya mradi huo.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Mafuriko: wataalamu washauri

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii