Gereza kubwa zaidi Afghanistan lina wafungwa wa Taliban karibu 2000

Wfungwa wa Taliban
Image caption Wapiganaji 2,000 wa Taliban wanashikiliwa kwenye gereza kubwa zaidi nchini Afghanistan

BBC ilipata fursa nadra kuingia kwenye gereza kubwa zaidi nchini Afghanistan, ambalo linawashikilia wapiganaji 2,000 wa Taliban katika upande mmoja wa gereza. Maisha ya Taliban ndani ya gereza kubwa Afghanistan

Je wapiganaji hawa wa Jihad ni nani, na wanafikiria nini kuhusu mustakabali wa Afghanistan?

Gereza la Pul-e-Charkhi, nje ya mji mkuu Kabul, limezungukwa na ukuta mgumu wa mawe na waya wa seng'enge, na pia linalindwa na nguzo ndefu za walinzi na mageti ya mbao makubwa. Kati ya wafungwa Maisha ya Taliban ndani ya gereza kubwa Afghanistan10,000, karibu moja ya tano ya wafungwa hao ni wapiganaji wa Taliban.

Mfungwa mmoja Mawlawi Fazel Bari anasema hakuzaliwa kuwa mpiganaji, lakini baada ya miaka mitano gerezani, anasema hakujisikia kama yuko tayari kufa.

''Nimekuwa mtu mwenye msongo wa mawazo. Sikufikiria kama nitaweza kujitoa muhanga, lakini sasa, kwa jina la Mungu ninaapa nitafanya hivyo,'' alieleza.

Mpango wa muda mrefu wa Taliban ni kurejesha utawala wa serikali ya kiislamu nchini Afghanistan - mfumo wake wa uongozi kati ya mwaka 1996 na 2001- ambao uliweka utawala wa Sharia. Kwa kuwapiga marufuku wanawake kuishi maisha ya kuonekana mbele ya umma na kuweka adhabu ya kuchapwa viboko na kukatwa viungo vya mwili.

Maelfu ya watu wamepoteza maisha Afghanistan tangu vikosi vya Marekani vilipouangusha utawala wa Taliban mwaka 2001, ikiwemo maelfu ya raia.

Wafungwa wa Taliban walikuwa wazi kuhusu hamasa zao na malalamiko yao, lakini walikataa kuzungumzia shughuli wanazozifanya. Lakini tunafahamu Mawlawo Fazel Bari alijiunga na Taliban miaka 15 iliyopita na kuwa kamanda wa kundi hilo katika jimbo la Helmand, wakipambana na vikosi vya Afghanistan na vikosi vya kijeshi kwenye eneo hilo.

Image caption Chumba cha jela cha Bari kina wanaume, wote wafuasi wa Taliban.

Chumba cha jela cha Bari kina wanaume, wote wafuasi wa Taliban. Kuna idadi ya watu wakiwa wamesimama kwenye mstari kwenye ushoroba - baadhi yao walikua wamekaa chini, wafungwa watu wazima wakiwa wamekaa sakafuni, kimya kimya wakisali kwa tasbihi.

Wafungwa hawa wamevipamba vyumba vya jela kubadili mazingira na kuyafanya kuwa kama peponi, wakiwa na imani kuwa watakapouawa watengwa moja kwa moja peponi.

Pembeni ya ukuta kuna maktaba ya vitabu kuhusu dini ya kiislamu na Koran.

Image caption Kuta za vyumba wanamolala wapiganaji wa Taliban vimepambwa wakiwa na imani ya kwenda peponi watakapokufa

Bari alianza kuhubiri na macho yote yalimuangalia. Pia ni mwanazuoni, hivyo wafungwa wenzake wanamtazama kama mtu muhimu.

''Nakwambia, ''alisema ''kama kuna mwanajeshi mmoja wa kigeni nchini Afghanistan, kupatikana kwa amani ni ndoto.''

Wanamgambo wa Taliban walikuwa wakishutumiwa kutoa hifadhi kwa Osama Bin Laden, wakishutumiwa kuratibu mashambulizi ya kigaidi ya mwezi Septemba nchini Marekani mwaka 2001. Baada ya miaka 19 ya vita kati ya Taliban na vikosi vilivyoongozwa na Marekani, mgogoro wa Afghanistan hivi sasa ni historia iliyopita muda mrefu nchini Marekani.

Marekani inasema ina wanajeshi karibu 13,000 nchini Afghanistan. Ikatangaza kupunguza na kuwabakisha 8,600 ndani ya kipindi cha miezi mitano baada ya makubaliano kutiwa saini.

Trump aliahidi wakati wa kampeni za mwaka 2016 kuwa atavimaliza vita vya Marekani nchini Afghanistan.

Lakini wakosoaji wanaamini kuwa bila kuishirikisha serikali ya Afghanistan-ambayo kwa sasa haihusiki kwenye mazungumzo ya amani-kuondoshwa kwa wanajeshi kunaweza kukazaa vurugu.

Ukitembea kwenye jengo la sita unaweza ukafikiri kama umeingia kwenye utawala wa Taliban. Ukumbi mkubwa ulikua umejaa wafungwa wa Taliban wakitembea kwa uhuru, wakinyoa nywele, kuoga na kupika.

Wafungwa wenzake Bari wametoka katika maisha tofauti. Kuna waliokuwa walimu, wakulima, wafanyabiashara na madereva ambao wamehukumiwa kwa kuwa wafuasi wa Taliban - wakiwa wamekutwa na makosa mbalimbali kama kukusanya kodi, na kufanya doria kama wanajeshi wa mguu, na kutega mabomu.

Image caption Wafungwa wengi wanasema kuwa sababu ya kujiunga na Taliban ni kutaka kulipa kisasi

Wengi wanasema kuwa awali walichochea kujiunga na Taliban kwa ajili ya kulipiza kisasi, hasa dhidi ya mashambulizi ya anga.

''Wakati majeshi ya Marekani yalipofanya mashambulizi ya anga kwenye kijiji changu (miaka 15 iliyopita) jirani yangu na wake zangu wawili walikufa, lakini mtoto wao mdogo aitwaye Rahmatullah, alinusurika,'' alisema Bari.

''Nilimuasili mtoto na nikamsaidia kupata elimu. Lakini kila wakati aliposikia sauti za helikopta juu, alikuwa akinikimbilia huku akipiga kelele: 'Wamekuja kuniua.''

Mfungwa mwingine wa Taliban kwenye jela hiyo, Mullah Sultan, pia anasema alitaka kulipiza kisasi kuhusu ''vitendo vya kinyama''.

Hatahivyo vikosi Taliban pia walishutumiwa kusababisha vifo vya raia katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kwa mujibu wa Umoja wa mataifa.

Viongozi kama Bari wanaaminika kupata maelekezo kutoka kwa wakuu wao wa juu, na hata kutoka kwa Sheikh Hibatullah Akhundzada, kiongozi wa juu wa Taliban, na kupeleka elimu moja kwa moja kwa wafungwa.

Habari za mazungumzo ya amani, yalipokua yanaendelea walikua wakipatiwa taarifa.

Image caption Ni mpango wa muda mrefu wa Taliban ni kurejesha utawala wa serikali ya kiislamu nchini Afghanistan

Na umoja wao na ngazi za uongozi zimewafanya kuwa na ushawishi mkubwa sana gerezani. Na kumudu kuwawakilisha wengine ndani ya gereza ili kupata huduma nzuri.

Walinzi wa gereza wanasema mahusiano kati yao na wafungwa wa Taliban ni mazuri.

''Ushirikiano una nguvu kati yetu na viongozi wa wafungwa wa Taliban'', anaeleza mlinzi Rahmudin kamanda wa jengo hilo mwenye miaka 28.

''Wako kama wafungwa 2,000 wa Taliban sasa tunahitaji kushirikiana ili waweze kushirikiana kutatua matatizo yao.''

Wafungwa wameiambia BBC kuwa mara nyingi hugoma kula kwa kufunga midomo yao kugomea hali mbaya ndani ya gereza kama vile dawa na kutendewa vibaya na walinzi.

Pia kuna ripoti kuhusu wafungwa wa Taliban kuwashambulia walinzi wa gereza, na hata kuchukua mamlaka za sehemu ya gereza.

BBC iliwasiliana na wizara ya mambo ya ndani kuthibitisha kuhusu taarifa hizo lakini hakupatikana.

Image caption Walinzi wa gereza wanasema mahusiano kati yao na wafungwa wa Taliban ni mazuri.

Serikali ya Afghanistan inasema watakutana na Taliban pale tu ikiwa mkataba wa kukomesha mapigano kwa muda wa mwezi mmoja utakapokubalika na pande zote. Katika kulijibu hilo, Taliban wamesema watakaa na serikali baada ya kuondoshwa kwa vikosi vya kigeni kutoka nchini humo.

Lakini watu wana maoni tofauti kuhusu hilo, wengine hawana imani kama amani inaweza kurejea kwa maana kila upande unavutia kwake, na ni vigumu kutofautisha kati ya rafiki na adui.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii