Misri,Sudan,Misri wakubaliana kuhusu ujenzi wa bwawa mto Nile

nile
Image caption Ujenzi wa bwawa hili unatarajiwa kukamilika mwaka 2021 kama hakutakua na pingamizi lolote

Misri, Ethiopia na Sudan wamekubaliana katika maamuzi ya mwisho kutumia maji ya mto nile kwa pamoja kuanzia Januari 2020.

Hii inafuatia baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu huko Washington DC Marekani siku ya jumatano, katika harakati ya kutatua mzozo wa nchi hizo kutokana na Bwawa linalojengwa kaskazini mwa Ethiopia, ambalo litakuwa kituo kikubwa kabisa cha kuzalisha umeme barani Afrika.

Lakini Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa 80%, ina hofu kuwa bwawa hilo litaathiri mfumo wa usambazaji maji ambao nao una changamoto kadhaa.

Unaweza pia kusoma:

Mkutano huo umeamua kuwa hakuna upande wowote baina ya nchi hizo utakaosimamisha ujenzi wa mradi huo, lakini pia Marekani na Benki ya Dunia watakua wasimamizi katika makubalino ya baadae.

Mapema mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zote tatu walikutana na rais wa Marekani Donald Trump.

Ethiopia imeshaanza ujenzi wa bwawa hilo kwa asilimia sabini na wamesisitiza kuwa hakuna atakayezuia ujenzi kuendelea , lakini Misri ina wasiwasi na matokeo ya ujenzi huo kwa maji yake na kiasi gani cha maji kitatumika.

Mradi huu mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme ukikamilika utakua mradi mkubwa zaidi barani Afrika , mradi utakaogharimu dola bilioni nne.

Mawaziri wa mambo ya nje waliafikiana makubaliano hayo, na kuahidi ushirikiano katika kumalisha mradi huo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mto nile unatiririka kupitia mji wa Aswan kusini mwa mji wa Cairo

Watakutana tena mwezi disemba mwaka huu nchini Marekani na januari 2020 kufatilia maendelo ya makubaliano yao.

Mara baada ya kukamilika, bwawa hilo litakalokuwa na uwezo wa megawatt 6000, lakini ujenzi huo umeathiriwa na ucheleweshaji na haijafahamika kama litaanza kufanya kazi baada ya muda wa mwisho uliowekwa na serikali mwaka 2021.

Viongozi hao wa mataifa matatu, walikutana jijini Khartoum Sudan katika ghafla ya kutia saini mkataba huo ambao umetajwa kama hatua ya kwanza katika kutatua mzozo huo.

Mara kwa mara Misri imepinga mradi huo ikisema huenda bwawa la Rennaissance likapunguza viwango vya maji kwa raia wake.

Misri kwa upande wake inaamini kuwa ina haki za kihistoria za mto huo kufuatia mikataba ya mwaka 1929 na 1959, inayoipa asilimia 87 ya maji ya mto , na pia uwezo wa kupinga miradi yoyote inayojengwa katika mto Nile.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii