Tupike
Huwezi kusikiliza tena

Aacha kazi ya benki kuwa mpishi

Pamellah Oduor ni muanzilishi wa kundi la Lets Cook nchini Kenya ambalo linaangazia mapishi ya jamii tofauti.

Alianza kundi hilo miaka mitatu iliyopita baada ya kuamua kuacha kazi ya benki ili kuangazia kitu anachopenda, upishi.

Bi Pamela alikua miongoni mwa majina 100 ya watu walio na mashabiki wengi katika mtandao wa kijamii wa Facebook mwaka jana.