Dwight Ritchie: Bondia wa Australia afariki baada ya kufanya mazoezi

Dwight Richie during his fight against Tim Tszyu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ritchie (kushoto) katika mapambano yake ya mwisho na Tim Tszyu mwezi Agosti

Bondia mmoja wa nchini Australia, Dwight Ritchie amefariki mara baada ya kutoka kwenye mazoezi.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 27, na baba wa watoto watatu alikuwa ana mapambano na Michael Zerafa huko Melbourne.

"Ni maskitiko makubwa kutangaza kifo cha mwanamisumbwi Dwight Ritchie ambaye amefariki akiwa anafanya kitu ambacho anakipenda," alisema promota wake Jake Ellis.

Ritchie alishindwa mara mbili katika mapambano 21, Hivi karibuni alipigana na Tim Tszyu wakiwa wanawania michuano ya uzito wa juu nchini Australia mnamo mwezi Agosti.

Kifo cha bondia huyo kimetokea mwezi mmoja baada ya kifo cha bondia wa Marekani kutokea.

Bondia wa Marekani alikufa baada ya kupata jeraha kwenye ubongo mara baada ya kupigana na bondia Charles Conwell.

"Dwight atakumbukwa katika ulimwengu wa ndondi kutokana na kipaji chake na jinsi alivyokuwa akishiriki mchezo huo kwa namna ya kipekee na hata mfumo wake wa maisha."

Ritchie aliposhindwa mchezo uliopita ndio sababu iliyomfanya kurejea kupambana na Tommy Browne.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kifo chake kimepokelewa na salamu nyingi katika mitandao ya kijamii wakieleza sifa zake na kuonyesha majonzi yao.

Tazama pia

Huwezi kusikiliza tena
Lulu Kayage,bondia muuza matunda

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii