Jinsi waandamanaji wa Iran walivyokabiliana na hali ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya mtandao

Zaidi ya waandamanaji 100 na vikosi vya usalama wameuawa kutokana maandamano Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zaidi ya waandamanaji 100 na vikosi vya usalama wameuawa kutokana maandamano

Kuna tofauti gani kuhusu wimbi la maandamano ya hivi karibuni nchini Iran?

Kilichoanza tarehe 15 mwezi Novemba kama mfululizo wa maandamano ni kupinga kupanda kwa gharama za mafuta yaliyosababisha mashinikizo ya kubadili utawala.

Watu nchini Iran waliingia mitaani wakiwa wamebeba mabango ya kiongozi wa juu wa nchi hiyo, wakimuita dikteta.

Siku sita za maandamano katika miji mbalimbali ya nchi, kufungwa kwa mawasiliano ya intaneti kulisababisha watu 106 kuuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na Shirika la mnesty International, ingawa vyanzo vingine vimesema idadi ya waliopoteza maisha inaweza kuwa kubwa zaidi.

Iran imethibitisha kuwepo kwa madhara kadhaa, na kuwashutumu watu waliowaita ''wanyang'anyi'' ikiwahusisha na maadui wa kigeni.

Ingawa maafisa wa Umoja wa Mataifa umezitaka mamlaka za Iran kutotumia silaha dhidi ya waandamanaji, picha za video zilionesha vikosi vya usalama vikiwafyatulia riasai waandamanaji.

Tarehe 20 mwezi Novemba, baada ya mapambano, rais wa Iran Hassan Rouhani alidai kupata ushindi dhidi ya mpango wa''adui''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption 20 Novemba 2019, mwanamke akitembea mbele ya jengo la benki lililoharibiwa

Kwa mujibu wa BBC nchini Iran, kilichofanya maandamano haya kuwa ya kipekee ni ''machafuko, vitendo vya unyang'anyi vilivyokithiri na njia kali za kudhibiti maandamano zilizochukuliwa na mamlaka.''

Wafuatiliaji wa masuala hayo wamesema kuwa amri ya kudhibiti maandamano haikuwa na chembe ya huruma ambayo ilisababisha si tu mauaji na majeruhi lakini pia maelfu walikamatwa.

Wataalamu wameeleza kuwa maandamano haya hayakuwa tu mjini Tehran, bali nchi nzima, miji kadhaa midogo na mikubwa ilihusika.

Maandamano ''haya hayakuwa na kiongozi na kwa mara ya kwanza katika miaka ya karibuni, yamewahusisha raia wa kipato cha kati.''

Ni nani anayeandamana?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wakisubiri kujaza matangi yao ya mafuta mjini Tehran

''Tuna matatizo mengi ya kiuchumi.Nyama ni ghali, kuku ni ghali, mayai ghali...na sasa mafuta,'' Muandamanaji wa kike aliiambia BBC.

Na wachambuzi wa BBC wanakubali: ''haki ya kukata tamaa ni chachu ya maandamano haya.''

Iran imekuwa kwenye changamoto ya kiuchumi tangu Marekani ilipoiwekea vikwazo mwaka 2018.

Gharama za maisha zimepanda kwa 40% na ukosefu wa ajira karibu 15%.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vitendo vya unyang'anyi vimeshamiri kutokana na maandamano

Matokeo yake, rais Rouhani ''ameshindwa kutimiza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni, hali iliyosababisha ghadhabu na fadhaa kubwa kutokana na hali ya uchumi na kutokuwepo kwa mabadiliko ya kisiasa,'' kwa mujibu wa wafuatiliaji wa siasa za Iran.

Na sasa watu wenye kipato cha kati wamekuwa watu wa ghadhabu na hasira wamejiunga na maandamano hayo,'' anaeleza mchambuzi wa BBC.

Misuguano kati ya jamii za makabila madogo na serikali kuu pia imesababisha kuwepo kwa vurugu katika miji ambayo ingependa kujitenga na Iran.

Huwezi kusikiliza tena
Nini kinachoondelea Iran?

Kuzimwa kwa mtandao wa Intaneti

Kuzimwa kwa mtandao wa Intaneti tangu siku ya Jumamosi kulifanya kushindwa kupatikana kwa picha halisi kuhusu ukubwa wa maandamano na matokeo ya udhibiti wa maandamano.

Lakini kwa mujibu wa Madyar Saminejad,kutoka shirika la Amnesty International,utafiti wao ulionesha'' kuwa wimbi la mauaji linaendelea nchini Iran ambapo mpaka sasa takribani watu 106 wamepoteza maisha katika miji 21''.

Pia imewawia vigumu waandamanaji kuwasiliana , ''mawasiliano yaliathiriwa vibaya, hakuna uratibu na kuna taarifa kidogo kuhusu nani aliyeratibu maandamano,'' wanaelezwa wafuatiliaji wa matukio hayo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Simu inayoonyesha kuwa hakuna mawasiliano ya intaneti

''Baadhi ya watu hutumia VPN, mtandao binafsi ambao hauna uhusiano mtandao wa Umma, ili kuepuka udhibiti wa serikali na kuweza kutuma na kupokea data binafsi, bila kupitia mitambo ya mawasiliano ya Umma,''

''Hakuna mtandao wa kijamii wa WhatsApp, Telegram ilifungwa miaka miwili iliyopita.Hali hii inamaanisha kuwa ''watu wamerejea katika nyakati zile za kupokea ujumbe kwa njia ya makaratasi na majarida''.

Mustakabali wa Iran ni upi ?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raisi Hassan Rouhani (katikati) anasema maadui wa Iran wamedhibitiwa

Baada tu ya kuwasambaratisha waandamanaji, Serikali iliwapeleka watu wanaowaunga mkono kuandamana kwenye mitaa hiyohiyo.

Rais Rouhani alisema ''Hii ina maana kuwa maadui zetu, ambao walikuwa wakipanga haya kwa miaka miwili na zaidi wamedhibitiwa.''

Bado haijfahamika nani yuko nyuma ya maandamano haya, ingawa rais amewashutumu ''watu wenye njama za kuharibu utawala wake'' wanaoungwa mkono na Marekani,Israel na Saudi Arabia.

Katika vyombo vya habari vya Iran kinachozungumzwa ni kuwa kila kitu kiko sawa hivi sasa, lakini ripoti kutoka katika maeneo hayo zinasema maandamano bado hayajakoma.

Na kwa hali ya uchumi ilivyo, Hasira ya watu haitaondoka hivi karibuni.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii