Ripoti ya BBI Kenya: Rais mwenye mamlaka kuchagua baraza la mawaziri na waziri mkuu

Viongozi nchini kenya katika uzinduzi wa ripoti ya kamati ya BBI kenya
Image caption Viongozi nchini kenya katika uzinduzi wa ripoti ya kamati ya BBI kenya

Rais aliyechaguliwa na wengi atahitaji washirika wengi bungeni kuhakikisha kwamba kuna upitishwaji wa haraka wa miswada mbali na kuidhinishwa maswala muhimu ya biashara za serikali iwapo mapendekezo ya BBI yatakubalika.

Kamati ya BBI inapendekeza kwamba rais atamchagua waziri mkuu, mawaziri na manaibu wao kutoka kwa wabunge waliochaguliwa kinyume na serikali ya sasa ilivyo ambapo mawaziri wanachaguliwa kutoka nje.

Fursa pia imetolewa kwa rais kuwachagua watu binafsi ambao sio wabunge lakini ambao watakauwa wabunge wa zamani, ikimaanisha kwamba wataruhusiwa bungeni lakini hawatakuwa na uwezo wa kupiga kura ili kuidhinisha miswada.

Kulingana na ripoti hiyo waziri mkuu atachaguliwa miongoni mwa wabunge na lazima atoke kutoka chama chenye wanachama wengi katika bunge ama mtu aliye na ufuasi mkubwa iwapo kutakuwa na serikali ya muungano.

Rais mwenye mamlaka:

Rais atasalia kiongozi wa taifa na serikali mbali na kuwa kamanda mkuu wa jeshi. Yeye atakuwa kiunganisha cha umoja wa taifa.

Rais atasimamia baraza la mawaziri , ambalo litakuwa na naibu wa rais , waziri mkuu na baraza la mawaziri.

Rais mwenye mamlaka atakuwa na uwezo wa kubaini sera za serikali kwa jumla huku mawaziri chini ya uongozi wa waziri mkuu watakuwa na jukumu la kuendesha biashara za serikali bungeni.

Rais ataongoza kwa awamu mbili kama ilivyo katika katiba. na naibu wa rais atakuwa mgombea mwenza wa rais . Naibu huyo wa rais atakuwa akimsaidia rais.

Jukumu la waziri mkuu:

Waziri mkuu atakuwa na jukumu la kuwasimamia mawaziri na kuhakikisha kuwa ajenda ya serikali inaeleweka ndani ya bunge na nje.

Kulingana na mapendekezo hayo mawaziri watakaokuwa na manaibu mawaziri pia watatarajiwa kutoka katika chama tawala ama muungano.

Kiongozi huyo ataendelea kupokea mshahara wake kama mbunge na kwamba hakutakuwa nyongeza ya mshahara kwa jukumu lake jipya

Kufutwa kazi kwa waziri mkuu:

Waziri mkuu atafutwa kazi na rais ama kupitia kura isiokuwa na imani naye bungeni.

Kiongozi rasmi wa upinzani:

Atakayeibuka katika nafasi ya pili katika uchaguzi huo wa urais atakuwa kiongozi rasmi wa upinzani iwapo chama chake hakitawakilisha serikalini kulingana na ripoti hiyo ya maridhiano.

Kamati hiyo ilipendekeza kwamba kuna umuhimu wa kuwepo kwa upinzani ulio dhabiti hivyobasi chama ama muungano wa vyama ambao haupo serikalini utakuwa upinzani rasmi.

Mawaziri kivuli:

Kiongozi rasmi wa upinzani bungeni ataruhusiwa kuwa na baraza kivuli la mawaziri.

Wakati wa maswali bungeni - Upinzani utakuwa na jukumu muhimu wakati wa maswali ya waziri mkuu Bungeni.

Baraza la mawaziri ni kiungo muhimu cha uogozi wa serikali.

Hatahivyo kuna hofu katika mfumo wa serikali uliopo , kulingana na jinsi Wakenya walivyoliambia jopo kazi la BBI.

Rais ataliteuwa baraza la mawaziri baada ya kushauriana na waziri mkuu. Mawaziri watawajibikia afisi zao zilizoundwa na rais kulingana na katiba.

Vilevile jopo hilo limependekeza kwamba makatibu katika baraza la mawaziri wapewe jina la Mawaziri.

Ili kuhakikisha kuwa kuna uwajibikaji bungeni kutakuwa na nafasi ya waziri atayechaguliwa kutoka kwa wabunge na watakuwa wakifanya kazi kama mawaziri wengine katika baraza la mawaziri.

Mawaziri hawa watenedela kupokea mhshahara wao kama wabunge na hakutakuwa na nyongeza yoyote ya mshahara katika majukumu yao mapya.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii