Watu wamehalalisha kutumia nguvu wakifanya ngono

Anna
Image caption Anna anasema kuwa alichukia kuvutwa nywele zake na kupigwa vibao na mpenzi wake wakati wanafanya mapenzi

Kutumia nguvu wakati wa kufanya mapenzi kwa watu walioridhia limekuwa jambo la kawaida lakini wanaharakati wameonya juu ya tabia hiyo.

Onyo hilo limekuja baada ya wanawake zaidi ya nusu wenye umri chini ya miaka 40 kukutana na vitendo hivyo kwa kupigwa vibao, kubana pumzi , kokojolewa mdomoni au kukabwa na hata kushindwa kuongea, utafiti uliofanywa na BBC Radio 5.

Kwa wanawake ambao walipitia na vitendo hivyo kwa kutaka au kwa kutotaka, asilimia ishirini wanasema kuwa walichukia kufanyiwa hivyo.

Anna mwenye umri wa miaka 23, alisema kuwa alifanyiwa vitendo vya vurugu ambavyo hakuridhia wakati alipofanya mapenzi kwa ridhaa yake na wanaume watatu tofauti kwa wakati tofauti.

Kwa upande wake, ilianza na kuvutwa nywele na kupigwa vibao.

Na mwanaume alijaribu kuweka mkono wake kwenye shingo na kama kutaka kumkaba.

" Nilishtuka," alisema, "Nilijihisi vibaya na nilihisi kama nilitishwa.

Kama mtu anakupiga kibao bila kutarajia, niliona kudhalilishwa".

Anna alipowasimulia rafiki zake ndio akagundua kuwa hivyo vitendo huwa vinafanyika mara nyingi..

"Wanaume wengi huwa wanajaribu kufanya hivyo hata mara moja, kama sio jambo ambalo analofanya mara nyingi."

Alisema mara nyingine alikabwa na mpenzi wake wakiwa wanafanya mapenzi bila ya kutaarifiwa.

Anna,ambaye amemaliza chuo kikuu mwaka huu, anasema kuwa alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa anatumia nguvu wanapokutana na kumuacha na majeraha anayougulia maumivu kwa siku kadhaa.

"Ninajua kuwa kuna wanawake ambao watasema kuwa wanapenda kufanyiwa vitendo hivyo.

Shida inakuja kuwa wanaume kudhani kuwa kila mwanamke anapenda kufanyiwa vitendo hivyo."

Kampuni ya utafiti ya Savanta ComRes iliwahoji wanawake 2,002 nchini Uingereza wenye umri wa kati ya miaka 18 na 39 kama waliwahi kupigwa vibao, kukabwa na kufanyiwa vitendo vya kinyanyasaji wakati wanapofanya mapenzi.

Matokeo yake yalikuwa ni zaidi ya robo tatu walikutana na vitendo hivyo kwa kuwa walikuwa hawataki 38% na huku mbili ya tatu walidai kuwa hawakuwahi kukutana na hali jiyo kwa 31% na asilimia 31 nyingine hawakutaka kuzungumzia suala hilo.

Kituo cha haki za wanawake imeiambia BBC kuwa msukumo mkubwa kutoka kwa wanawake wadogo kuwa wanafanyiwa vitendo vya hatari na wapenzi wao.

"Tabia hii inakuwa kutokana na urahisi wa upatikanaji wa filamu za ngono ambazo zinaonyesha uhalali wa kutumia fujo wakati wa ngono."

Waliongeza pia kuwa:

"Mtu kuridhia kufanya mapenzi na mtu haimpi ruhusa ya kumfanyia vitendo vya unyanyasaji kama kumpiga mwanamke vibao na kumkaba."

'Niliogopa sana'

'Emma' ni mtu mwingine ambaye anasimulia jinsi alivyojisikia siku alipokutana na vitendo hivyo.

Anasema kuwa alipokuwa na miaka 30 alikuwa katika mahusiano ya muda mrefu na aliwahi kukutana na mpenzi wa mapenzi ya usiku mmoja.

"Tulishtukia tu tuko kitandani- bila kutarajia - alianza kunikaba. Nilishtuka sana na kuogopa mno. Sikusema chochote wakati huo , nilihisi kuwa atanidhuru."

Msichana huyo alihusisha tabia ya mwanaume huyo kuwa amepata ushawishi mkubwa na filamu za ngono.

"Nilihisi kuwa ni vitu ameviona kwenye mtandao na anataka kuviweka katika uhalisia wa maisha ya kawaida."

Utafiti umebainisha kuwa asilimia 42 wanafanya vitendo hivyo kutokana na msukumo fulani.

Fujo inachukuliwa kuwa kitu cha kawaida

Steven Pope ni mwanasaikolojia katika masuala ya mahusiano na ngono.i

Yeye anasemakuwa hilo tatizo ambalo linaumiza watu kimyakimya, anadhani kuwa ni vitendo vyenye madhara makubwa. Si sahihi kwa fujo kukubalika kuwa ndio mapenzi yenyewe.

Anadhani watu wanaofanya vitendo hivyo hawana ueleo wa athari za vitendo hivyo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii