Orodha mpya ya Fifa: Kenya na Uganda zapanda Tanzania yashuka

Majirani wa Kenya katika eneo la Afrika mashariki Tanzania hatahivyo wameshuka nafasi moja chini katika orodha hiyo hadi nafasi ya 134 kutoka 133 huku nayo Burundi ikishuka nafasi nane chini hadi nafasi ya 151. Haki miliki ya picha TFF/TWITTER
Image caption Majirani wa Kenya katika eneo la Afrika mashariki Tanzania hatahivyo wameshuka nafasi moja chini katika orodha hiyo hadi nafasi ya 134 kutoka 133 huku nayo Burundi ikishuka nafasi nane chini hadi nafasi ya 151.

Sare 1-1 dhidi ya Misri katika michuano ya kufuzu kwa kombe la mataifa mabingwa Afrika 2021 imeisaidia Kenya kupanda nafasi mbili juu katika orodha mpya za shirika hilo la kandanda duniani iliotolewa siku ya Alhamisi.

Majirani wa Kenya katika eneo la Afrika mashariki Tanzania hatahivyo wameshuka nafasi moja chini katika orodha hiyo hadi nafasi ya 134 kutoka 133 huku nayo Burundi ikishuka nafasi nane chini hadi nafasi ya 151.

Kushuka kwa Tanzania kunajiri baada ya taifa hilo kupoteza 2-1 kwa Libya katia kundi J

Harambee Stars ya Kenya sasa ipo katika nafasi ya 106 duniani ikiwa ni nafasi mbili juu kutoka nafasi ya 108 ambayo ilikuwa ikishikilia wakati wa orodha ya miwsho iliofanyika Oktoba 24.

Timu hiyo ingepanda juu zaidi katika orodha hiyo iwapo wangepata matokeo mazuri dhidi ya Togo nyumbani katika mechi yao ya pili ya kufuzu.

Majirano Uganda hatahivyo wamepanda juu nafasi mbili zaidi hadi nafasi 77 na inasalia timu inayoorodheshwa juu zaidi huku Kenya ikiwa ya pili.

Ethiopia wakati huohuo imepanda nafasi tano juu kufuatia ushindi mzuri wa 2-1 dhidi ya Ivory Coast mjini Bahir Dar katika mchuno wa kufuzu na sasa wameorodheshwa katika nafasi ya 146.

Image caption Mashabiki katika mojawapo ya mechi za kombe la mataifa barani Afrika

Senegal wakati huohuo inasalia kuwa timu inayoorodheshwa katika nafasi ya kwanza kutoka Afrika huku ikishikilia nafasi yake ya 20 duniani huku Tunisia ikipanda juu nafasi mbili hadi nafasi ya 27 , nafasi nne juu ya Nigeria ambayo pia imepanda nafasi nne juu.

Mabingwa wa Afrika Algeria wamepanda nafasi tatu juu hadi katika nafasi ya 35 na sasa wako nambari nne katika orodha ya bara Afrika huku nayo Morocco ikishuka hadi nafasi ya tano na nambari 43 kwa jumla duniani.

Ubelgiji, Ufaransa na Brazil zimeshikilia nafasi zao katika nafasi tatu bora za kwanza duniani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii