Zimbabwe iko kwenye janga kubwa la njaa linalosababishwa na binaadamu

Mama akiwa amembeba mtoto wake mgongoni Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ukame, kukosekana kwa mvua ya kutosha na majanga ya asili vinachangia tatizo la ukosefu wa chakula

Umoja wa mataifa umeonya kuwa Zimbabwe ipo katika hatari ya kupatwa na janga la njaa linalosababishwa na binaadamu.

Utafiti umeonesha zaidi ya asilimia 60 ya watu milioni 14 nchini humo wanaelezwa kuwa na ukosefu wa chakula.

Sababu kuu ya tatizo hilo ni pamoja na mfumuko wa bei, umaskini, majanga ya asili na vikwazo vya uchumi.

Watoto na akina mama wamekuwa wahanga wa janga hilo, huku asilimia 90 ya watoto kuanzia umri wa miezi sita hadi miaka miwili kutokula chakula cha kutosha.

Msemaji wa Umoja wa mataifa Hilal Elver, kuhusu haki ya kupata chakula alichapisha matokeo hayo baada ya kutembelea nchi hiyo kwa siku 11.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zimbabwe iko katika hali mbaya kiuchumi

Bi Hilal Amesema kuwa ''siwezi kusisitiza vya kutosha kuhusu hali halisi ilivyo nchini Zimbabwe'' na kuendelea kusema kuwa hali inazidi kuwa mbaya.

Ameelezea kuwa watu wengi aliokutana nao walimudu kununua mlo mmoja kwa siku tu, na watoto wengi aliokutana nao walikuwa wamedumaa na kuwa na uzito mdogo sana.

''Simulizi za kuogofya nilizosikia kutoka kwa bibi, kina mama au mashangazi wanaojaribu kuwaokoa watoto wao kutoka kwenye janga la njaa katikati ya matatizo mengine zitasalia na mimi.''

Utapia mlo sugu ni ugonjwa ambao upo nchi nzima, kote vijijini na mijini.

Ukame na hali ya hewa mbaya vimeharibu uzalishaji wa mazao, vile vile mfumuko wa bei umefanya hali kuwa mbaya zaidi.

Unaweza pia kutazama

Huwezi kusikiliza tena
Zimbabwe imekabiliwa na ukamwe kwa miaka 40

Bi Elver amesema raia wa Zimbabwe aliozungumza nao ''walieleza kuwa hata kama vyakula vinapatikana madukani, kuporomoka kwa mapato yao ukijumlisha na mfumuko wa bei kuongezeka zaidi ya asilimia 490, umewafanya kuwa na wasiwasi wa kutopata chakula.''

Ameonyesha pia sababu nyingine zinazochangia kwenye tatizo zikiwemo matatizo ya rushwa na vikwazo vya kiuchumi.

Na pia aliongeza na kusema Zimbabwe ni moja ya nchi nne zinazoongoza kwa matatizo ya ukosefu wa chakula pamoja na nchi zenye mizozo mikali.

''Hatua zinaweza kuchukuliwa kitaifa kuheshimu, kulinda na kutimiza wajibu wa haki za kibinadam za serikali na za kimataifa, kwa kusitisha vikwazo vyote vya uchumi.''

''Na kumalizia kwa kusema ''watu wa Zimbabwe wana ujasiri na hawastahili mateso kama hayo.''

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii