Kipande cha zizi alimowekwa Yesu baada ya kuzaliwa charejea Bethlehem

A nun kisses the relic during a procession in Bethlehem, 30 November 2019 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kurejea kwa kifaa hiki kunakuja wakati wa mwanzo wa sherehe za krismasi mjini Bethlehem

Kipande cha ubao kinachoaminiwa kuwa sehemu ya vifaa vilivyotumiwa na Yesu kimerejeshwa mjini Bethlehem baada ya miaka zaidi ya 1,000 barani Ulaya.

Papa Francis aliagiza kurejeshwa kwa kifaa hicho cha kale chenye ukubwa wa mkono wa binadamu kutoka kanisa la Roma la Basilica ya Santa Maria Maggiore kama zawadi.

Kipande hicho cha ubao kimekuwa Roma tangu karne ya saba.

Kiliwekwa kwa muda mfupi kwenye eneo la umma mjini Jerusalem kabla ya kuendelea na safari yake hadi mjini Bethlehem wakati wa mwanzo wa sherehe za Krismasi mjini humo.

Kifaa hicho kilipokelewa Mjini Bethlehem siku ya Jumapili na Bendi ya gwaride na kuchukuliwa katika kanisa la Mt. Catherine, karibu na Kanisa la Nativity ambako wataalamu wa masuala ya utamaduni wanasema Yesu alizaliwa.

Ni upi umuhimu wa kifaa hiki cha kale cha kidini?

Baadhi ya Wakristo wanaamini kipande hicho kidogo cha ubao ni sehemu ya mahali ambamo Yesu alilazwa baada ya kuzaliwa.

Wasimamizi wa Custodia Terrae Sanctae,maeneo matakatifu ya dini za kikatoliki katika Ardhi Takatifu wanasema Kipande hicho kilitolewa kama msaada na wasimamizi wa eneo takatifu la St Sophronius kwa Papa Theodore 1 katika karne ya 7.

Wanasema kipande hiki kimekuwa kikitunzwa kwenye eneo la maonyesho ya umma katika kanisa dogo la Roma la Santa Maria Maggiore, ambako "idadi kubwa ya mahujaji kutoka kote duniani " walikiheshimu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kifaa hiki cha kale kilionyeshwa kwa umma kwa muda mfupi mjini Jerusalem kabla ya kuhamishiwa katika eneo alikozaliwa Yesu

Huku sehemu kubwa ya kifaa hiki ikisalia Roma, kurejea kwa kipande kidogo kulishangiliwa na Wakristo katika kanda hiyo ya mashariki ya kati

"Moyo wangu unapiga. Kusema ukweli ninalia kwa furaha kutokana na tukio hili na ninamshukuru Papa, kwa ukarimu hii ambao ameuleta Bethlehem," Louisa Fleckenstein, mlinzi wa mahujaji wanaotembelea Ardhi takatifu, aliliambia shirika la habari la AP.

Lakini baadhi hawakuridhika.

"Tuliposikia kwamba ubao wa zizi unakuja tulifikiri kuwa litakuwa ni zizi zima, lakini tukaona kipande tu ," Sandy Shahin Hijazeen aliliambia shirika la habari la Reuters.

Kwanini ubao huu unapelekwa Bethlehem sasa?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waumini wakiomba huku wakitazama kipande cha zizi ambamoinaamin iwa kuwa Yesu kristo alilazwa baada ya kuzaliwa

Vatican imeelezea kurejea kwa kipande hiki kama zawadi kutoka kwa papa Francis.

Meya wa Bethlehem, Anton Salman, ameliambia shirika la habari la Wapalestina -Wafa kwamba kurejeshwa kwake kumefuatia ombi kutoka kwa rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas d wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mjini Vatican.

Kurejeshwa kwake kumekuja wakati wakristo Wakatoliki wakianza kipindi cha kujiandaa kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo kinachofahamika katika kanisa hilo lama Adventi- ,ambacho huwa ni majuma manne ya kuelekea sikukuu ya Krismasi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Umati wa watu ukisherehekea kurejea kwa kipande cha zizi alimoweka Yesu baada ya kuzaliwa kulichorejeshwa mjini Bethlehem

Wakristo wanakadiriwa kuwa 1% ya Watu wa Palestina katika eneo la Ukanda wa magharibi (West Bank), Gaza na Jerusalem Mashariki , lakini Bethlehem ni eneo maarufu kwa mamahujaji wa Kikristo kutoka maeneo mbali mbali ya dunia hususan wakati wa Krismasi.

Maelfu kw amaelfu ya mahujaji wa kikristo wanatarajia kufanya hija mwezi huu, kwamujibu wa Wafa.

"Kuadhimisha Krismasi huku kukiwa na kipande cha zizi ambamo Yesu kristo alizaliwa ni jambo zuri sana na ni tukio kubwa " alisema Amira Hanania, mjumbe wa kamati ya ngazi ya juu ya rais Abbas ya masuala ya Makanisa.

Unaweza pia kusoma:

Je hiki ni kitu kisicho cha kawaida?

Dkt. Yisca Harani, Mtaalamu wa msuala ya Kikristo wa Israeli ,ameelezea kuwa kurejea kwa kipande cha zizi alimozaliwa Yesu kama "mabadiliko ya kihistoria".

"Miaka elfu moja iliyopita , Roma ilikuwa nakusanya zana za kidini kutoka masharki kujijenga kama Jerusalemu mbadala . Sasa ,Rome ni thabiti vya kutosha kiasi kwamba inaweza kurejesha vitu hivi Jerusalem na Bethlehem ," aliliambia gazeti Israeli Haaretz.

Kipande cha zizi sio kifaa cha kwanza cha kidini ambacho kimerejeshwa na Papa.

Mapema mwaka huu, aliwapatia viongozi wa kanisa la Orthodox Mashariki vipande vya mifupa ya Mtakatifu Peter.

Baadae alisema kuwa hatua hiyo ililenga kuyaleta pamoja makanisa ya Orthodox na Katoliki.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Mtoto amvua kofia Papa Francis

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii