'Mfalme wa kondomu Kenya' anayekabiliana na maambukizi ya Ukimwi
Huwezi kusikiliza tena

'Kenya inahitaji wafalme na malkia wengi zaidi wa mipira ya kondomu'

Stanley Ngara, maarufu mfalme wa kondomu wa Kenya, amekuwa akisambaza mipira ya kondomu katika jiji la Nairobi, kwa lengo la kuhamasisha watu umuhimu wa kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

"Mipira ya kondomu imehusishwa na uasherati kwa sababu watu hufikiria kuwa mtu akiwa ameathirika na ugonjwa huo basi yeye ni kahaba au anashiriki ngono na zaidi ya mtu mmoja," anasema Mfalme huyo wa miaka 47 ambaye anajaribu kukabiliana na dhana hiyo potofu kuhusu matumizi ya kandomu inayochangia unyanyapaa. Amezungumza na BBC.

Video na Anthony Irungu

Mada zinazohusiana