Ripoti ya BBI: Je Kenya inajenga daraja lisilo na mwelekeo?

Mfuasi wa upinzani akiwakabili maafisa wa polisi wakati a maandamano ya uchaguzi w Oktoba 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ghasia zilizuka wakati matokeo ya uchaguzi wa 2017 yalipotangazwa

Katika msururu wa barua za waandishi kutoka Afrika, Mwandishi Waihiga Mwaura anauliza iwapo tofauti za kikabila na migawanyika ya kisiasa inaweza 'kutibiwa'.

Miezi 21 iliopita , kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga na mpinzani wake rais Uhuru Kenyatta walikumbatiana na kuamua kufanya kazi pamoja.

Ukweli ni kwamba walisalimiana mbele ya Kamera katika kile ambacho baadaye kilijulikana kuwa maamkuzi ya kihistoria yani 'Handshake'.

Huwezi kusikiliza tena
Waziri wa maswala ya Kigeni Tanzania Paramagamba Kabudi awataka Wakenya kuiga mfano wa Wat
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maamkuzi ya handshake kati ya rais Uhuru Kenyatta (kushoto) na Raila Odinga (kulia) yalisitisha mkwamo wa kisiasa

Hatua hiyo ilimaliza wasiwasi wa miezi kadhaa kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata , ambao mara kwa mara husababisha migawanyiko na kusababisha ghasia nchini Kenya.

Viongozi hao wawili walikubaliana kuunda kamati itakayotafuta njia ya kumaliza hali hiyo ya ukosefu wa uthabiti.

Jopo hilo lililojulikana kama Building Bridges Initiative BBI lilipaswa kuangazia maswala tisa ikiwemo ukabila, ufisadi na ugatuzi - ikiwa ni miongoni mwa changamoto kuu tangu taifa hilo lilijipatie Uhuru mwaka 1963.

'Kuwafunza wazazi'

Baada ya miezi 18 ya kutembea ndani ya taifa hilo la Afrika mashariki , Jopo hilo la BBI hatimaye limewasilisha matokeo yake na kupongezwa sana.

Bwana Odinga aliwaambia wale waliokongamana katika uzinduzi wake kwamba kabla ya mchakato huo kuanza , taifa hilo lilikuwa katika hatari ya kutumbukia katika ghasia.

Rais huyo aliongezea: Hatukuwepo katika hali nzuri kama taifa. Tulikuwa tumegawanyika. Ulikuwa huwezi kweda katika jamii nyengine.

Wawili hao waliungana wakikumbatia mapendekezo ya BBI.

Baadhi ya mapendekezo muhimu ni:

  • Kubuni wadhfa wa waziri mkuu kama njia ya kupunguza uwezo wa rais.
  • Kuwapatia Wakenya kaunti 47 zilizo na bajeti kubwa ili kutekeleza mipango iliowekwa.
  • Kuwa na baraza dogo la mawaziri na uwakilishi zaidi wa taifa.
  • Kuwapatia wafichuzi wa ufisadi asilimia 5 ya pato litakalopatikana

Pendekezo jingine katika ripoti hiyo yenye kurasa 156 linalenga kubuni madarasa ya watu wazima kwa wazazi wote wapya ili wajue jinsi kutoa maagizo, kurekebisha , kukemea na kuwasaidia wanao

Baadhi ya raia wameipongeza ripoti hiyo wakiitaja kama inayounganisha , kama ilivyoangaziwa matatizo yao mbali na kuwa mwanzo wa mchakato wa kulijenga upya taifa.

Pia wamelisifu jopo hilo kwa kutowaongezea kodi Wakenya kufuatia uvumi kwamba mapendekezo hayo yangefanyika.

'Saa nyingi za kufanya kazi'

Lakini nakala hiyo inakabiliwa na upinzani hata iwapo sio wa haja.

Baadhi ya wakosoaji wanasema kwamba baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 , kuikuwa na ripoti tofauti na kamati ambazo ziliangazia sababu ya ghasia hizo ambazo zilitokana na upeanaji wa ardhi na uhalifu mwengine wa kiuchumi pamoja na unyanyasaji wa haki za kibinadamu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wafanyakazi wa Kenya kama wale wa mabawabu kutoka seta ya kibinafsi , hufanya kazi kwa saa nyingi licha ya kupata mishahara duni

Kwa nini tusizitoe faili hizo badala ya kutumia fedha ambazo kulingana na mbunge Patrick Munene zitagharimu takriban bilioni 10 za Kenya ili kuziangazia.

Ripoti hiyo inajiri wakati ambapo serikali inakabiliwa na changamoto ya kifedha - baada ya waziri wa fedha kuweka mikakati ya kuzuia matumizi zaidi serikalini.

Niliguswa sana na matamshi ya bawabu mmoja siku ambayo ripoti hiyo ilitolewa.

Aliniuliza kuhusu yaliomo na nikamuelezea kwa kifupi.

Baadaye alilalamika kwamba kile ambacho alikuwa amesikia kufikia sasa hakijaangazia changamoto anazokumbana nazo - masaa marefu ya kufanya kazi { saa 12 , siku sita kwa wiki na mshahara duni katika kazi ambapo mshahara wa chini ni dola 131 mfanyakazi hathaminiwi na hupigwa faini kwa kukosa kuripoti kazi hata iwapo wewe ni mgonjwa, alitumai kwamba ripoti hiyo itaangazia hali yake ya kikazi mbali na ile ya maelfu ya wenzake katika sekta ya usalama.

Je upinzani unasmaje?

Wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo wengine waliwachwa midomo wazi wakihoji kuhusu hali ya kidemokrasia nchini Kenya.

Rais alionekana akijihusisha sana na waziri mkuu Raila Odinga zaidi ya wanachama wa chama chake hatua inayozua maswali ya iwapo upinzani wa Kenya umepoteza sauti yake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ripoti ya BBI ilizinduliwa kufuatia hisia tofauti

Katika mwaka uliojaa ufichuzi kuhusu maswala ya kifisadi katika sekta ya umma , upinzani tangu maamkuzi hayo ya kihistoria , ulionekana kusahau majukumu yake ya kuiweka serikali katika ratili.

Kwa mfano umeendelea kunyamaza kuhusu kashfa kama ile iliogunduliwa na gavana wa benki kuu , ambaye aliwashutumu maafisa wa zamani wa benki hiyo kwa kutumia miujiza ili kupotosha kuhusu matumizi ya serikali.

Wakati jaji mkuu aliposhutumu serikali mapema mwaka huu kwa kujaribu kulemaza idara ya mahakama , kupitia kukata matumizi yake, kutosikika kwa sauti ya upinzani kuliwashangaza wengi.

Katika wakati ambapo hifadhi ya damu inakabiliwa na uhaba - kukiwa na madai kwamba damu inauzwa kwengineko , wanasiasa wanaonekana kutoingilia kati swala kama hilo ili kuchunguza.

Mapendekezo ya BBI yana kipindi kirefu kuidhinishwa na huenda yakapitia kura ya maoni iwapo katiba itabadilishwa.

Lakini kwa wananchi - mchakato huo una dalili ya kundi la kisiasa kutotaka kuvuka daraja kutoka upande wao wa upendeleo kuona jinsi watu wanavyopambana upande wa pili.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii