Rais wa Yoweri Museveni wa Uganda apania kuumaliza ufisadi

Rais Museveni awakosoa maafisa wa serikali ya Uganda kwa kujihusisha na ulaji rushwa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Museveni awakosoa maafisa wa serikali ya Uganda kwa kujihusisha na ulaji rushwa

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema wakati umewadia wa kukomesha vitendo vya kifisadi kwani anawatambua wale wanaofanya vitendo hivyo.

Rais Museveni alisema hayo baada ya kuongoza matembezi ya kilomita nne dhidi ya ufisadi, yaliyofanyika katika jiji la Kampala hadi kwenye uwanja wa uhuru Kololo.

Pia aliwakosoa maafisa wa serikali ya Uganda kwa kujihusisha na ulaji rushwa.

''Watu wananifahamisha...wale wanaotua rushwa kwa watu wenu wwanakuja na kunijulisha, ila sina ushahidi wa kutosha kuwakamata, lakini nawafahamu wengi wao kwamba ni mafisadi... kama unaona sijakukamata usifikiri kwamba uko salama bali nasubiri kupata ushahidi wa kutosha '' alisema bwana Museveni.

Image caption Hafla ya kampeini dhi ya Ufisadi Uganda

Aliwambia waliohudhuria matembezi hayo kuwa yeye mwenyewe ni tajiri kakini hajawahi kuiba mali ya umma.

Msongamano mkubwa wa magari ulishuhudiwa jijini huo baada ya barabara kuu nyingi kufungwa kwa ajili ya matembezi hayo.

Baadhi ya walioshiriki waliitaka serikali kushiriki kikamilifu vita dhidi ya ufisadi siyo matembezi ya ya kujionyesha na kuishia hapo.

Unaweza pia kusoma:

''Matembezi kama haya yasitumike kama hafla ya watu kujuana bali kuwe na ufuatiliaji'', mmoja wao alisema.

Vyombo vya habari na na watu katika mitandao ya kijamii wanasema hatua hiyo ni ya kujipatia umaarufu na kwamba serikali haijo tayari kukabiliana na tatizo la ufisadi.

''Kwa kweli serikali nyingi za Afrika zimekuwa zikipambana na hali hizo... niu ugonjwa ambao umefanya wanainchi wengi wa nchi za Kiafrika kutopata maendeleo'' mwingine ambayea hakutaka jina lake litajwe aliiambia BBC.

Mawaziri kadhaa wa ngazi ya juu na baadhi ya jamaa wa familia yake wametuhumiwa kwa ulaji rushwa lakini ni nadra sana wafunguliwe mashitaka au kufungwa.

Wakati wa matembezi hayo hakuna magari ya uchukuzi wa umma yaliruhuhusiwa kuingia jijini, hali ambayo iliwafanya watu wengi kukwama katika vizuizi vya muda vya barabarani.

Wengine waliamua kutembea hadi kazini huku baadhi yao wakiamua kusalia majumbani.

Matembezi hayo yameshirikisha watu mbali mbali wakiwemo mabalozi wa mataifa mbali mbali wanaowakilisha mataifa yao nchini Uganda.

''Haya matembezi ni muhimu kwa sababu yanato elimu na kuwahamasisha wananchi wasitoe au kuchukua rushwa, kwa hivyo sio kwa wananchi wa Uganda pekee yake bali hili ni suala la kupiga vita ufisadi katika Jumuiya nzima ya Afrika Mashariki'' alisemaBalozi wa Tanzania nchini Uganda, Dkt Aziz Mlima.

Lakini baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanahoji matembezi hayo wakisema ni ishara ya serikali ya bwana Museveni kushindwa kupambana na vitendo vya ufisadi.

Upinzani ukiongozwa na Dkt Kiza Besigye ulipanga kufanya matembezi yao, lakini Besiyge alikamatwa mapema na polisi na kurudishwa nyumbani kwake kabla ya kufanya matembezi yao.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii