Ripoti ya uchunguzi wa madai dhidi ya Trump uko kwenye hatua za mwisho

Ripoti ya madai dhidi ya rais Donald Trump kutolewa 03 Desemba Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ripoti ya madai dhidi ya rais Donald Trump kutolewa 03 Desemba 2019

Ushahidi dhidi ya madai yanayomuhusu rais wa Marekani Donald Trump ya kutumia madaraka vibaya bado 'yanaungwa mkono na wengi', kwa mujibu wa kamati inayoongoza majadiliano ya tuhuma hizo .

Rais aliweka maslahi yake binafsi katika siasa "chini ya maslahi ya taifa la Marekani", ripoti hiyo imeeleza .

Ni namna gani alijaribu kuhusisha utawala wa Marekani na Ukraine, ili aweze kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Ripoti hiyo iliandaliwa kama mbinu ya kumuondoa Trump madarakani kutokana na kesi inayomhusu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Spika wa bunge la congress kutoka chama cha Democrat Nancy Pelosi (kushoto)amesema kuwa rais Trump "lazima awajibike''

Trump amekanusha kuhusika na madai yote dhidi yake na kudai kuwa wanaomtuhumu ni waongo na wanafanya uhaini mkubwa.

Kabla ya ripoti hiyo kutolewa, chama cha Democrat kilimshutumu vikali Trump na kuongoza uchunguzi dhidi yake, shutuma ambazo zilidaiwa kuwa ni za uongo.

Baada ya chapisho hilo, msemaji wa ikulu wa White House Stephanie Grisham alisema kuwa chama cha Democrats kimeshindwa kabisa kutoa ushahidi dhidi ya shutuma zinazomkabili Trump na hiyo inaashiria wazi kushindwa kwao.

Ripoti hiyo sasa ipo katika kamati kuu ya baraza la hukumu hii leo ambayo itaweza kuangazia hukumu ambayo itatolewa dhidi ya Trump.

Ripoti hiyo inasema nini?

Madai ya shutuma za Trump nchini Ukraine yaliwekwa wazi siku ya Jumanne na kamati kuu ya uchunguzi.

Shutuma dhidi ya rais Trump ambayo inaweza kumuondoa madarakani ,zimechukua miezi kadhaa ya uchunguzi kuhusu Trump kumhusisha na kashfa ya rushwa na nchi jirani kwa manufaa yake binafsi ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump anashutumiwa kuwashinikiza viongozi wa Ukraine kumchunguza hasimu wake kisiasa Joe Biden(kulia)

Shutuma dhidi ya rais Trump ambayo inaweza kumuondoa madarakani ,inakuja baada ya mazungumzo ya simu kati ya rais Trump na kiongozi wa Ukraine .

Katika mazungumzo hayo ya simu, Trump alimshinikiza rais wa Ukraine kufanya uchunguzi wa kashfa za rushwa dhidi ya mpinzani wake Joe Biden na mtoto wake, ambaye anafanya kazi katika kiwanda cha gesi nchini Ukraine.

Lengo la uchunguzi huo uweze kumsaidia katika kampeni yake ya urais kwa mwaka 2020.

"Rais alimtaka rais, Volodymyr Zelensky, kutangaza hadharani kashfa hiyo.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa ushaidi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Trump bado ni kipingamizi kikubwa kwa wanachama wa chama chake.

Trump anashutumiwa nini?

Katika mawasiliano ya simu, Trump alimtaka Bwana Zelensky amchunguze Joe Biden, ambaye kwa sasa ndiye mgombea aliye mstari wa mbele kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais mwaka ujao, na mtoto wake wa kiume Hunter Biden, ambaye awali alifanyia kazi kampuni ya nishati ya Ukraine Burisma.

Uchunguzi unataka kubaini ikiwa Bwana Trump alitumia kitisho kuzuia msaada wa jeshi la Marekani kwa Ukraine ili kuifanya imchunguze Biden na mwanae. Rais Trump amekana kufanya kosa lolote na ameutaja uchunguzi kuwa ni "hila".

Wiki iliyopita, Kamati ya masuala ya ujasusi ilikamilisha wiki mbili za kusikiliza kesi hiyo , kufuatia wiki kadhaa za vikao vya faragha ambapo waliwahoji mashahidi.

Adam Schiff, mwenyekiti wa kamati ya ujasusi, anayeongoza uchunguzi huo alisema kamati za masuala ya kigeni na intelijensia - ilitoa ripoti hiyo tarehe 3 Disemba.

Huwezi kusikiliza tena
Je inawezekana kumvua madaraka rais wa Marekani?

Ni nini kitakachofuata?

Majadiliano ya madai yataanza kwa kusikiliza katiba nne ambazo zitaeleza ni namna gani madai hayo yanaweza kufanyiwa kazi.

Ikulu ya Marekani imekataa kuhudhuria kesi hiyo kwa madai kuwa imeshughulikiwa bila kuwepo usawa.

Baada ya kura ya bunge linalodhibitiwa na Democratic , kesi itaendeshwa katika bunge la seneti linalodhibitiwa na Republican.

Kama bwana Trump atapatikana na hatia kwa theluthi mbili ya wabunge- matokeo ambayo yanaonekana huenda kutopatikana- atakuwa ni rais wa kwanza wa Marekani kung'olewa madarakani kupitia mashtaka ya aina hii.

Image caption Shutuma za Trump

Trump and impeachment

Chama cha Republican kinasema nini?

Kabla ya toleo la kwanza la ripoti kutolewa hadharani, Republican walitoa chapisho lenye kurasa 123 kupinga urasimu ambao umetuhumiwa kwa watu ambao wametoa ushaidi.

Inasema kuwa hawakubaliani kabisa na namna Trump anavyofanya maamuzi na jinsi dunia inavyomtazama.

Nakala hiyo inadai kuwa Democrats wanajaribu kuondoa matakwa ya raia wa Marekani kwa kumfanyia hila rais tangu aingie madarakani.

"Hakuna mwanachama/kiongozi wa Democrat aliyeshuhudia rushwa, uhalifu wa hali ya juu," na kuwa ushahidi ambao unaweza kuwa kigezo cha kumuondoa Trump madarakani.

Kamati ya kiintelijensia inayoongozwa na mwenyekiti Adam Schiff imepuuzia madai ya Republican na kusema kuwa wanategemea ushaidi ambao utakuwa na vigezo vya kumuondoa Trump madarakani.

Katika kongamano linaloendelea mjini London, la maadhimisho ya miaka 70 ya Nato, bwana Trump alimdhihaki bwana Schiff kwa kumuita asiye na akili.

Ni namna gani kashfa zinaweza kumuondoa kiongozi?

Sehemu ya kwanza ya shutuma hizo - maamuzi yatakuwa ni kumuondoa rais madarakani.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa, mawakilishi wakiweza kupitisha kura za ripoti ya madai dhidi ya Trump, basi seneta atalazimika kusimamisha kesi hiyo.

Kura ya seneta inawataka robo tatu ya watakaopiga kura ili impe fursa ya kumuondoa rais katika madaraka.

Ni marais wawili tu katika historia ya Marekani - Bill Clinton na Andrew Johnson - walipata shutuma za madai ambayo yaliwaweka njia panda kuondolewa madarakani lakini haikufikia huko.

Rais Richard Nixon alijiuzulu kabla ya madai ya kashfa dhidi yake kusikilizwa

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii