Picha 20 za Rais Putin aliyeingia madarakani kama rais mwaka 1999

Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza wakati wa kampeni Machi 2018

Vladimir Putin anakaribia kuadhimisha miaka 20 tangu alipochukua uongozi kama rais na waziri mkuu, Je unakumbuka nini kuhusu hatua za kisiasa alizopiga na matukio maarufu ya michezo aliyohudhuria?

Bill Clinton alikuwa katika Ikulu ya Marekani wakati aliyekuwa afisa wa usalama wa taifa anaingia madarakani kama rais Desemba 31, 1999.

Katika kipindi cha miaka 20, Marekani imefanikiwa kuwa na marais watatu huku Uingereza ikiwa na mawaziri wakuu watatu.

Kuanzia migogoro duniani, kashfa za ndani ya nchi hadi ushindi katika nyanja ya spoti na picha zinazosemekana kuwa propaganda tu, tunaangazia twasira inayomueleza Putin katika kipindi cha miaka 20 madarakani.

Maelezo ya picha,

Vladimir Putin alichaguliwa kama waziri mkuu Agosti 1999 kabla kuchukua hatamu kutoka kwa mtangulizi wake Boris Yeltsin kama rais Desemba 31

Putin tayari alikuwa amechaguliwa kama waziri mkuu wakati Urusi ilianzisha vita vya pili vya Chechen Oktoba 1999, ikijibu msururu wa mashambulizi ya mabomu katika maeneo ya makazi.

Awali, uongozi wake ulighubikwa na mgogoro katika eneo la kusini. Vikosi vya Urusi vilizingira na kuvamia mji mkuu wa Chechen, Grozny. Mwaka 2003, Umoja wa Mataifa ukaelezea Grozny kama mji ulioharibiwa vibaya baada ya uvamizi huo.

Maelezo ya picha,

Putin alizuru Chechnya Machi 2000, miezi kadhaa baada ya kuanzisha vita vya Chechen

Kwa miaka mingi Urusi imekuwa ikikumbwa na mashambulio ya kijeshi mfano, 2004 shule ya Beslan ilivamiwa ambapo watu 330 walipoteza maisha yao wengi wao wakiwa watoto.

Rais Putin hakumaliza oparesheni hiyo hadi mwaka 2009.

Maelezo ya picha,

Baraza la mawaziri Urusi wakikaa kimya kwa dakika moja Septemba 2004 baada ya shule ya Beslan kuvamiwa ambapo wanamgambo walitekeleza mauaji ya watu zaidi ya 330.

Bwana Putin alithibitishwa kuwa rais baada ya uchaguzi wa Machi 2000, na ndani ya miezi kadhaa akajikuta akiwa katika ya mgogoro wa kiuongozi.

Kukatokea janga baada ya nyambizi ya Kursk kuzama majini na kusababisha vifo vya watu 118.

Maelezo ya picha,

Putin alikutana na familia ya nahonda wa nyambizi ya Kursk lakini alikosolewa vikali kwa hatua alizochukua wakati janga hilo linatokea.

Nyambizi ya Kursk ilipozama mwaka 2000, serikali ya Urusi ilichukua muda mrefu kufahamisha jamaa za wahusika na pia rais hakurejea mara moja kama ilivyotarajiwa na wengi kutoka Bahari nyeusi alikokuwa mapumzikoni.

Maelezo ya picha,

Rais wa Marekani W Bush alimwalika rais Putin katika Ikulu ya rais mwaka 2001. Wawili hao waliandamana hadi katika makazi ya Bush Texas wakati wa ziara yake

Katika kipindi cha miaka kumi ya kwanza madarakani, Vladimir Putin alikuwa na uhusiano mzuri na viongozi wa nchi za magharibi licha ya kwamba alikosoa sana sera zao.

Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi (kulia) alitembelea Urusi 2003 kujadili hali ilivyo Iraq

Maelezo ya picha,

Malkia alimwalika Putin mwaka 2003 - hiyo ikiwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi wa Urusi mwaka tangu 1874

Urusi ilikuwa mwenyeji wa mkutano wake wa kwanza wa G8 mwaka 2006, na kuthibitisha uanachama wake.

Maelezo ya picha,

Angela Merkel, Tony Blair, Jacques Chirac, Vladimir Putin na George W Bush wakipigwa picha katika mkutano wa G8 mwaka 2006, St Petersburg

Chini ya katiba ya Urusi, Bwana Putin hangeweza kugombea urais kwa awamu ya tatu mfululizo, hivyo basi mwaka 2008, akawa waziri mkuu kwa kindi cha miaka minne.

Kuna wachache waliomuona Rais Dmitry Medvedev kama kibaraka wa Putin aliyefanyakazi kwa niaba ya mkuu wake.

Maelezo ya picha,

Kama waziri mkuu, Putin alitembelea waliojeruhiwa baada ya kutokea kwa vita na Georgia

Wakati Georgia ilipotuma vikosi vyake ili kuchukua tena udhibiti wa eneo la kusini mwa Ossetia 2008, Urusi iliendelea kuvamia Georgia.

Hatua hiyo ilikwa kama onyo kwa mataifa ya magharibi lakini uamuzi wa Urusi wa kuvamia mashariki mwa Ukraine ulizidisha kuzorota kwa uhusiano kati ya Putin na viongozi wa nchi za Magharibi.

Hatua ya Urusi ya kutwa eneo la Krimea kutoka kwa Ukraine ilisababisha Umoja wa Ulaya na Marekani kuiwekea Urusi vikwazo na kusitisha uanachama wa nchi hiyo katika muungano wa G8.

Maelezo ya picha,

Rais Putin akizungumzia hatua ya kutwaa rasi ya Krimea mwaka 2014 ambako kulifanya aendele kuwa maarufu kulingana na kura ya maoni.

Maelezo ya picha,

Agosti 2-19, Putin alihudhuria mashindano ya pikipiki katika eneo la Krimea alilolitwaa. Ukraine ilisema huo ulikuwa ni ukuikwaji mkubwa wa kujitawala

Maelezo ya picha,

Mazungumzo yalianza tena mwezi huu na rais Volodymyr Zelensky, miaka mitano baada ya kutokea kwa mapigano Ukraine lengo likiwa ni kumaliza mapigano

Wakati Syria ikiwa imeendelea kushuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka minne, Urusi iliingilia kati na kumuunga mkono mshirika wake, Rais Bashar al-Assad, ambaye serikali yake ilikuwa inakaribia kuanguka.

Uamuzi wa Putin wa kutuma ndege za Urusi na mavazi ya kijeshi Syria, kulibadilisha hali iliyokuwa inaendelea.

Maelezo ya picha,

hatua ya rais Putin kumuunga mkono rais wa Syria Bashar al-Assad kulibadilisha mkondo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria

Baada ya ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa Urais wa Marekani 2016, Idara ya ujasusi ya Marekani ilithibitisha kwamba Urusi iliingilia kampeni za uchaguzi.

Maelezo ya picha,

Idara ya ujasusi ya Marekani ilisema kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa urais mwaka 2016

Pia unaweza kusoma:

Mwaka 2018, Uingereza iliishutumu Urusi kwa kumtilia sumu afisa aliyekuwa jasusi wa nchi hiyo Sergei Skripal huko Salisbury.

Maelezo ya picha,

Uhusiano na aliyekuwa Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, ulianza kuyumba baada ya Sergei Skripal kutiliwa sumu

Katika kipindi chake chote madarakani, Rais wa Urusi amekuwa akijaribu kudhibiti picha zake na za Urusi kama nchi kwa ujumla. Picha kadhaa zilizotolewa na kiongozi huyo kwa miaka kadhaa zimekuwa zikijaribu kumuonesha kama kiongozi imara.

Maelezo ya picha,

Vladimir Putin akiwa amebeba bunduki karibu na mpaka wa Mongolia mwaka 2007

Maelezo ya picha,

Putin alitoa picha zinazoonesha upande wake wa pili, 2013. Anacheza katika barafu msimu wa baridi akiwa na mbwa wake Buffy na Yume

Maelezo ya picha,

Pia akiwa kama Rais, Putin ameonesha uwezo wake kimchezo na kushiriki katika mchezo wa magongo msimu wa baridi pamoja na Judo

Pia amejitahidi katika kuimarisha michezo nchini Urusi kwa kuwa mwenyeji wa mshindano ya Olimpiki msimu wa Baridi mwaka 2014 na mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018.

Mashindano ya dunia yaliofanyika Sochi yalikuwa ya mafanikio makubwa lakini athari zake baada ya wanariadha wake kushtumiwa kwamba wametumia dawa za kuongeza nguvu bado yanaendelea kuonekana.

Shirika la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini duniani limepiga marufuku washiriki wa Urusi kushiriki michezo yote maarufu kwa miaka minne. 2015, ripoti yao ilisema kwamba Urusi ilikuwa imetekeleza kile kinachoweza kuchukuliwa kama mpango wa serikali wa kuongeza wanariadha wake nguvu. Na mwezi huu, ilibainika kwamba Urusi imeingilia data ya maabara iliyotolewa Januari kwa ajili ya utafiti.

Maelezo ya picha,

Rais Putin alikuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha Urusi inakuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018

Huku mashindano ya soka ya dunia yaliyofanyika Urusi 2018 yakichukuliwa kama mafanikio ya kimataifa, shutuma za wanariadha wake kutumia dawa za kuongeza nguvu kuna maanisha kwamba Urusi haitashiriki katika mashindano yajayo yatakayofanyika Qatar mwaka 2022.

Picha zote zina haki miliki.