Wajinga Nyinyi: Jinsi wasanii wa Afrika Mashariki wanavyopambana kupitia vipaza sauti kuleta mabadiliko

Msanii Ney wa Mitego aliwahi kukamatwa na Basata ikapiga marufuku kabisa wimbo uliomkosoa rais Magufuli, lakini baadae rais aliagiza aachiliwe na wimbo wake uchezwe Haki miliki ya picha NEY WA MITEGO/FACEBOOK
Image caption Msanii Ney wa Mitego aliwahi kukamatwa na Basata ikapiga marufuku kabisa wimbo uongozi wa rais Magufuli, lakini baadae rais aliagiza aachiliwe na wimbo wake uchezwe

Miongoni mwa kazi za ya msanii ni kuielimisha, kuiburudisha, kuiliwaza na kuikosoa jamii na asipotekeleza hayo basi kazi yake haijakamilika.

Lakini je wasanii wa muziki wa Afrika Mashariki wameweza kuielimisha na kuikosoa jamii?.

Katika kile ambacho kilionekana kama njia ya kuikosoa na kuielimisha jamii King Kaka kwa jina lake halisi Kennedy Ombima, mwishoni mwa juma alitoa video tata ya wimbo aliouta 'Wajinga Nyinyi', akikosoa maovu miongoni mwa jamii ya Wakenya.

Katika wimbo huo amewatuhumu wazi wazi watu binafsi aliowataja majina moja kwa moja pamoja na wabunge na taasisi za umma kwa ufisadi, uliokithiri na maovu mengine katika jamii , huku akiwataka Wakenya kutafakari maovu hayo na kuyarekebisha.

Aliutumia wimbo huo huwatolea wito Wakenya kutafakari ujumbe wa video yake na kuchukua hatua.

Wimbo ulipokelewa kwa hisia tofauti

Tangu video ya wimbo huo kutoka, imekuwa ndio maarufu zaidi mitandaoni nchini Kenya .

Licha ya wimbo 'Wajinga nyinyi' ulioimbwa kwa mtindo wa rap kusifiwa na wengi kuwa maudhui yake yalikua ni ya kweli baadhi ya waliotajwa majina walimkosoa na kutishia kumshitaki.

Image caption Katika wimbo wake wenye utata 'Wajinga nyinyi' King Kaka aliwakosoa , wabunge na taasisi za umma kwa ufisadi

King kaka alidai anatishiwa maisha na kujisalimisha katika Ofisi ya Mwendeshamashitaka mkuu wa Serikali (DCI), akidai lakini ofisi hiyo ilisema haikumuita.

Mwanamuziki huyo ambaye alipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wasanii wenzake kwa kutoa ujumbe huo, pia aliahidiwa utetezi wa kisheria na mawakili maarufu iwapo atapelekwa mahakamani kwa kuimba wimbo 'Wajinga nyinyi' .

Mbali na mwanamuziki King Kaka wanamuziki wengine wa Kenya pia awali walitoa nyimbo zilizokosoa ufisadi katika jamii yao. Mfanyo ni mwanamuziki Erick wa mtindo wa Afrobit Wainanaina katika wimbo wake 'Nchi ya kitu kidogo' na mwanamuziki wa mtindo wa Hiphop Juliani katika wimbo wake 'Sitasimama maovu yakitawala'

Hali ikoje nchini Tanzania?

Kwa muda sasa wasanii wa muziki nchini Tanzania wamekuwa wakiwasilisha ujumbe wao hususan baada ya kuingia madarakani kwa rais John Pombe Magufuli. Ukosoaji wao umekua ni ukijibu yanayofanyika nchini mwao.

Haki miliki ya picha Nikki Mbishi/ Facebook
Image caption Katika wimbo wake 'Iam Sorry JK'' Nikki Mbishi aliongelea kuhusu namna baadhi ya Watanzania akiwemo yeye walimkosoa vibaya Kikwete alipokua mamlakani lakini sasa wanamkosa na kutamani angegombea awamu ya tatu mamlakani!.

Wa kwanza alikua ni wanamuziki ni mwanamuziki wa Hip hop Karama Masopud na wimbo wake 'Magufuli balaa ' , al maarufu Kalapina.

Hata hivyo kalapina ambaye alishindwa katika harakatii zake za kuwania ubunge, alitoa wimbo mwingine wa kumsifu rais Magufuli. Aliimba: 'Unaweza kudhani ni ni miujiza lakini ni picha halisi. Upinani uko kimya, hauna la kusema. Amefanya walichopanga kukifanya.''

Msanii mwingine aliyekuwa na ujumbe wa ukosoaji miongo ni mwa jamii, ni mwanamuziki wa mtindo wa rap, Nikki Mbishi ambapo Januari 2017 aliimba:''I'm Sorry JK.''

Mtangulizi wa rais John Pombe Magufuli , Jakaya Kikwete, alifahamika kama 'JK'.

''Itaeleweka ikiwa nitasema siku moja kwamba, hakuna rais kama JK. Watanzania wanakukosa sanana kwa niaba ya Watanzania ninasema wanakukosa sana na wanatamani ungegombea awamu ya tatu kama rais''

Katika wimbo huo, msanii aliongelea kuhusu namna baadhi ya Watanzania akiwemo yeye walimkosoa vibaya Kikwete alipokua mamlakani lakini sasa wanamkosa na kutamani angegombea awamu ya tatu mamlakani!.

Alisema kwa sasa hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Mikopo ya wanafunzi wa Chuo Kikuu haipatikani tena kwa urahisi, uchumi unadhoofika na benki zinakabiliwa na wakati mgumu, hakuna pesa mitaani na demokrasia imebanwa, miongoni mwa mambo mengine.

Haki miliki ya picha Nakaaya Sumari/ Instagram
Image caption Nakaaya Sumari aliachia wimbo wake 'Mr politician' wa rais Jakaya Kikwete.

Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) lilimuita msanii huyo wa muziki wa rap na kumhoji. Baadae aliandika taarifa katika kituo cha polisi jijini Dar es salaam, na wimbo wake ukapigwa marufuku mnamo mwezi wa Februari 2017.

Kufuatia kuvamiwa kwa kituo cha TV na mshirika wa karibu wa rais, John Magufuli Paul Makonda, wasanii wa Hip hop walipeleka hasira zao juu ya kile kilichokua kikiendelea.

Ney wa Mitego alitoa wimbo, 'Wapo'. Ingawa hakutaja moja kwa moja jina lolote la kiongozi katika wimbo wake ilikua wazi kuwa alikua akielezea maeneo ambayo rais Joh Pombe Magufuli ''ameshindwa'' kutekeleza wajibu wake.

Wimbo huo ulipata umaarufu sana. Alikamatwa mara moja na Basata ikapiga marufuku kabisa wimbo huo.

Hata hivyo Jumatatu iliyofuatia, rais Magufuli aliagiza Ney aachiliwe huru na wimbo wake uchezwe.

Nyimbo nyingine zilizokosoa utawala wa rais Magufuli ni pamoja na 'Dereva wa 5 hana leseni' wa Wagosi wa Kaya, 'Usinipangie' wa Baghdad na 'Madaraka ya kulevya' wa Weusi.

Usinipangie uliimbwa kujibu kauli ya rais Magufuli kusema kuwa hatoambiwa la kufanya.

Unaweza pia kusoma:

Madaraka ya kulevya ni wimbo ambao mistari yake iliandikwa kwa ustadi lakini yenye utata. Wimbio huo haukuwazungumzia moja kwa moja rais Magufuli au Makonda , lakini maneno yaliyotumiwa yanaonyesha kumuhusu kiongozi aliyelewa mamlaka kukiuka maadili yake ya kiuongozi.

Msanii wa muziki wa rap Profesa Jay katika wimbo wake 'Ndio, mzee aalikosoa utawala wa rais Mkapa miaka ya 2000, Nakaaya Sumari katika wimbo wake Mr politician na Mrisho Mpoto katika wimbo Mjomba ambao wengi wanaamini vilimlenga rais Jakaya Kikwete.

Uganda

Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wasanii nchini Uganda walijitokeza kukosoa maovu wanayodai yanatekelezwa na utawala wa rais wa muda mrefu yoweri Museveni, huku wengine wakimsifu.

Mwaka 2012 katika wimbo wake Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine katika wimbo wake 'By Far' aliashiria nia yake ya kujiunga na siasa akiukosoa utawala wa rais Museveni.

Aliimba : 'My father said there is more politics music industry than in the Parliement, they dont know who they are dealing with' akimaanisha 'Baba yangu aliniambia kuna siasa zaidi katika muziki kuliko bungeni, lakini hawajui ninani wanaekabiliana nae'.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bobi Wine amekua mkosoaji mkuu wa maovu katika jamii za Waganda ukosoaji wake ukiilenga zaidi serikali ya rais Museveni pamoja na viongozi wengine wa Uganda.

Katika wimbo huu alielezea kuwa wakazi wa vitongoji duni kikiwemo kitongoji cha ambako alikua akiishi hawaogopi vitisho, huku akiwatolea wito raia kuamka na kupigania haki zao.

Akiimba kwa kwa lugha ya Luganda Bibi Wine, mwaka 2016, alitoa wimbo 'Dembe' au 'Amani' Msanii Bobi Wine aliouimba Bobi Wine alikemea kile alichokiita ghasia miongoni mwa viongozi wa Uganda, huku akiwalaumu kwa kuchochea ghasia hususan wakati wa uchaguzi.

Aliitaka jamii ya Waganda kupiga kura kwa amani ili kuepuka ghasia zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita, akiwatuhumu viongozi waliopo madarakani kuchochea ghasia hizo.

Imekua vigumu kutumia muziki kuelimisha na kukosoa maovu Uganda:

Nyimbo zake zilizojaa ukosoaji wa rushwa na ukosefu wa haki za kijamii nchini Uganda zilichangia kwa kiasi kikubwa kuchaguliwa kwa Bobi Wine kama mbunge wa kyadondo Mashariki mwaka 2017.

Mnamo mwaka 2017 , msanii huyo aliimba: 'Ugandans need equal opportunity', Waganda wanahitaji fursa sawa'', akitaka serikali ifikishe huduma kwa usawa miongoni mwa raia mkiwemo ajira kwa vijana.

Hata hivyo juhudi zake za kuendelea kuukosoa utawala wa rais Museveni kupitia usanii wake wa muziki zimegonga mwamba baada ya maafisa wa usalama kuzuia matamasha yake yote ya muziki.

Haki miliki ya picha FACEBOOK / JOSE CHAMELEONE
Image caption Hivi karibuni jose Camelione (Kushoto) alitangaza kuingia siasa ili kukosoa maovu yanayofanyika Uganda, jambo lililosababisha kukosa ufuasi wa rais Yoweri Museveni katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Msanii wa muziki wa Hip hop na Afro bit Uganda ni Jose Chameleone kutoka nchini Uganda ambaye alifahamika kwa kutumbuiza nyimbo zake katika hafla za Chama tawala cha NRM pamoja na matukio mengine ya serikali ya rais Museveni sasa amegeuka kuwa mkosoaji wake.

Baada ya Chameleone Kutangaza nia yake ya kuingia siasa na kugombea kiti cha Meya wa Jiji Kuu Kampala ili kumaliza maovu yanayofanyika katika mji huo, rais Museveni ambaye alikua mfuasi wake katika ukurasa wa twitter alimua kuondoa ufuasi wake.

Kinyume na Bobi Wine pamoja na Jose' Chamilion, Msanii mwingine maarufu kwa jina la Bebe Cool amekua mstari wa mbele kuunga mkono utawala wa rais Yoweri Museveni, huku akiwakosoa wasanii wenzake kwa kuukosoa utawala.

Ni dhahiri kuwa wasanii wengi wa muziki katika nchi za Afrika Mashariki wamekua wakitumia kazi yao kuzielimisha na kuzikosoa jamii zao, japo katika mazingira magumu inapokuja katika ukosoaji wa kisiasa. Hata hivyo swali ni je ukosoaji huu wa wasanii unaleta tija?

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii