Vifo vyao vilikua ni pigo 2019

Mugabe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mugabe aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu

Ingawa taarifa hii inaangazia zaidi vifo vya watu maarufu was Afrika mashariki walifariki mwaka 2019, tunaanza na kiongozi wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye kifo chake kiliitikisa dunia :

Pigo la kwanza lilikua ni Kifo cha aliyekuwa rais wa zaman wa Zimbabwe Robert Mugabe kilichotokea tarehe 6 Juni, 2019.

Mugabe aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.

Taarifa ya kifo chake kwa mara ya kwanza ilithibitishwa na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kupitia mtandao wa twitter.

Viongozi mbali mbali wakiwemo wa kikanda na kimataifa walituma salamu zao za rambi rambi, huku wakimpongeza kwa kuwa mwanapinduzi shupavu.

Wazimbabwe walikumbuka 'mkombozi na mkandamizaji'

Unaweza pia Kusoma:

2. Reginald Mengi:

Chanzo cha picha, IPP

Maelezo ya picha,

Rais John pombe Magufuli alisema ataendelea kumkumbuka Mzee Mengi kwa mchango wake katika maendeleo ya taifa lake.

Lilikua ni pigo kubwa kwa Watanzania na dunia nzima baada ya kupokea taarifa ya mwenyekiti wa makampuni ya IPP na moja ya watu matajiri na mashuhuri nchini Tanzania Reginald Mengi aliyefariki dunia mapema mwezi Mei 2019.

Mzee Mengi alizaliwa mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro alifariki dunia akiwa mjini Dubai, Falme za Kiarabu baada ya kuugua kwa muda mfupi, kwa mujibu wa familia yake.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, aliwaongoza mamilioni ya Watanzania kutuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huo.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter Magufuli alisema ataendelea kumkumbuka Mzee Mengi kwa mchango wake katika maendeleo ya taifa lake.

Watu mbali mbali walijitokeza kuifariji familia yake na kumpumzisha kwao Machame,

Wengi walimsifu kwa kuwa mtu aliyekua mfano wa kuigwa katika sekta ya ujasiliamali, mpole, asiye na majivuno, mkarimu na mwenye huruma hususan juhudi zake za kuwasaidia watu wenye ulemavu na wengine wasiojiweza.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Mwili wa Reginald Abraham Mengi wawasili Dar es salaam

3. Bob Collymore:

Chanzo cha picha, CITIZEN TV

Maelezo ya picha,

Collymore alianza kuuiongoza kampuni ya afaricom mwaka 2010

Kifo cha Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni kubwa zaidi ya mawasialiano ya simu Afrika Mashariki Safaricom, Bob Collymore kililitikisa eneozima la Afrika Mashariki , huhusa ni kutokana na kifo hicho kutokea ghafla. Taarifa ya kifo chake ilitolewa na kampuni hiyo iliyosema kuwa aliaga dunia Juni Mosi 2019.

Kabla ya kifo chake Collymore, alichukua likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017 na kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu ya saratani .Alirejea Kenya mwezi Juni mwaka jana.

Collymore alianza kuuiongoza kampuni ya afaricom mwaka 2010.

Mwaka 2017 wanahisa walipiga kura kuongeza mkataba wa Bob Collymore kwa miaka miwili baada ya mkataba wake kuisha.

Mkataba aliokuwa akiufanyia kazi ulikuwa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mkurugenzi aliyekalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi kwenye historia ya kampuni hiyo.

Viongozi kadhaa wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta walituma salamu za rambirambi kwa familia kufuatia kifo hicho.

Uhuru amesema nchi imepoteza kiongozi ambaye mchango wake kwa Kenya utakumbukwa.

Unaweza pia kusoma:

4. Ruge Mtahaba:

Chanzo cha picha, Clouds Media Group Tanzania

Maelezo ya picha,

Ruge Mutahaba amefariki Afrika kusini alikokuwa akipokea matibabu

Watanzania pamoja na tasnia ya habari kwa ujumla hususan katika eneo la Afrika Mashariki haitasahau tarehe 26 Februari, mwaka 2019 siku ambayo Luge Mutahaba alifariki dunia nchini Afrika Kusini alikokua akipata matibabu.

Mutahaba alizaliwa Mwaka 1970 nchini Marekani.

Muasisi mwenza na Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga alielezea namna ambavyo Ruge atakumbukwa:

'Ruge ametutoka akiwa bado kijana mdogo kabisa, amefanya mambo mengi sana. Amepigana ameugua, amekuwa South Africa kwa muda tukipigania sana kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida, afya bora. 'Lakini Mungu amempenda na amemchukua siku ya leo, amueke mahali pema peponi'.

Ruge alikua moja kati ya watu wenye mchango mkubwa katika tasnia ya habari burudani, na ni mtu aliyekua mwenye juhudi za kujenga fikra za maendeleo ya vijana Tanzania.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, Rais Magufuli aliandika taarifa yake huku akitoa pole kwa familia , ndugu jamaa na marafiki zake wa karibu wakiwemo wasanii nchini Tanzania.

Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki nchini Tanzania waliomboleza kifo chake huku wengi wakisema watamkumbuka kama mtu aliyekua mkaribu, mchapakazi na ambaye aliwasaidia kimaisha.

Unaweza pia kusoma:

5.Binyavanga Wainaina:

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Maelezo ya picha,

Binyavanga Wainaina, alikuwa miongoni mwa Wakenya wa kwanza kujitokeza hadharani na kusema kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja

Kifo cha Mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja, kilikua ni kifo kilichozungumziwa sana Kenya Afrika mashariki, na hata nje ya mipaka ya Afrika hususan kutokana na hali yake ya kijinsia.

Mwanaharakati huyo alifariki akiwa na umri wa miaka amefariki mwezi Mei akiwa na umri wa miaka 48, baada ya kuugua.

Wainaina alikuwa mshindi wa tuzo ya Caine na aliorodheshwa na gazeti la Times magazine miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani 2014.

Binyavanga Wainaina, alikuwa miongoni mwa Wakenya wa kwanza kujitokeza hadharani na kusema kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Tangazo hilo lilimfanya Binyavanga kuwa mmoja wa waafrika mashuhuri kujitokeza hadharani.

Alifichua hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter iliowiana na siku ya kuzaliwa kwake.

Mwaka 2018 Binyavanga Wainaina ambaye ni mwandishi maarufu wa vitabu aliwashangaza Wakenya wengi alipotangaza atafunga ndoa na raia wa Nigeria.

Unaweza pia kusoma:

6. Ali Mufuruki:

Chanzo cha picha, NMG

Maelezo ya picha,

Ali Mufuruki aliaga dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa akipata matibabu.

Kifo cha hivi karibuni kilikuwa ni cha Ali Mufuruki, mfanyabiashara, muhisani na kocha wa masuala ya uongozi, ambaye alifariki dunia siku ya Jumamosi tarehe 07 mwezi huu wa Desemba akiwa na umri wa miaka 61.

Watu mbali mbali nchini Tanzania na nje ya taifa hilo watuma rambirambi zao hususan kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kifo cha Bwana Mufuruki.

Mwenyekiti wa jukwaa la CEO Roundtable la Tanzania Sanjay Rughani alinukuliwa akisema Mufuruki alifariki katika hospitali ya Morningside ya jijini Johannesburg Afrika Kusini ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Mtendaji Mkuu wa jukwaa la sekta binafsi nchini, Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Godfrey Simbeye alikitaja kifo cha Bwana Mufuruki kuwa ni pigo na pengo kubwa katika dira ya sekta binafsi nchini Tanzania.

Mufuruki alikuwa kiongozi aliyejali sana sekta binafsi nchini. Kila mara alikuwa tayari kutoa ushauri wake juu ya namna ya kuimarisha sekta hii. Tutazikosa sana busara zake.' Alisema Simbeye.