Operesheni ya Ufaransa dhidi ya wanamgambo wa kijihadi Afrika Magharibi bado haina matumani

Mwnajeshi wa Ufaransa katika eneo la Sahel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwnajeshi wa Ufaransa katika eneo la Sahel

Ongezeko la idadi ya mashambulio yanayofanywa na wanamgambo wa kijihadi Afrika Magharibi limeibua maswali kuhusu oparesheni ya kijeshi ya Ufaransa katika eneo hilo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezuru taifa la Niger wikendi hii kutoa heshima ya mwisho kwa wanajeshi wake na raia wa nchi hiyo waliouawa katika oparesheni ya kijeshi hivi karibuni.

Oparesheni ya sasa imekuwa ikiendelea tangu mwaka 2014 na Ufaransa imekuwa ikitoa usaidizi katika upande wa usalama katika nchi za Mali, Mauritania, Niger, Burkina Faso na Chad.

Mataifa hayo yamekuwa yakikabiliana na mtandao mkubwa wa makundi ya kijihadi ambayo rais wa Niger Mahamadou Issoufou amesema yamegeuka kuwa "wataalamu katika sanaa ya kivita".

Shambulio lililofanywa na wapiganaji wa kijihadi dhidi ya kambi ya kijeshi mapema mwezi huu lilisababisha vifo vya zaidi ya wanajeshi sabini wa Niger.

Mwezi Novemba, wanajeshi 13 wa Ufaransa walifariki baada ya helikopta kugongana wakati wa oparesheni dhidi ya wapiganaji wa kijihadi nchini Mali, ikiwa ni idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi wa Ufaransa tangu miaka ya 1980.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger

Viongozi wa kikanda wameomba msaada zaidi wa kimataifa kukabiliana na wanamgambo hao lakini pia kumekuwa na ongezeko la maandamano nchini Ufaransa dhidi ya waarabu huku maandamano yakishuhudiwa katika miji mingine katika kanda hiyo.

Mtandao sugu wa makundi ya kijihadi

Eneo la Sahel, ambalo ni jangwa kubwa katika eneo la Afrika Magharibi, linatajwa kuwa makazi ya makundi kadhaa yaliyo na ufungamano na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na Islamic State.

Pia kuna wanamgambo wa kikabila wanaopigana wenyewe kwa wenyewe na pia kupigana na vikosi vya kitaifa na vikosi vya Ufaransa

Juhudi za kupambana na zimefanikiwa kuwaondo wa kijihadi na kusambaratisha baadhi ya shughuli za wanamgambo hao.

Lakini hali bado haijaonesha dalili ya kuimarika.

Nchini Niger, kumekuwa na ongezeko kubwa la mashambulio ya wanamgambo mwaka huu.

Katika taifa jirani la Mali, oparesheni ya kukabiliana na makundi ya kigaidi ilizinduliwa mwaka 2014 kwa ushirikiano na vikosi vya Ufaransa, imesaidia kuleta hali ya utulivu.

Hatahivyo idadi ya vifo vilivyotokana na makabiliano kati ya vikosi vya Mali na makundi ya kijihadi vimeongezeka zaidi ya mara mbili katika kipindi cha mwaka mmoja, kwa mujibu wa takwimu za mradi wa kundi la linalochunguza ghasia za kisiasa, linalofahamika kama 'Armed Conflict Location and Event Data Project (Acled)'.

Makundi makuu ya kijihadi:

  • Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) - Muungano wa makundi ya kijihadi, ambayo yanaendesha shughuli zake katika eneo la Sahel
  • The Islamic State in the Greater Sahara (ISGS) - Mshirika wa kundi la kigaidi la IS, ambalo linakaliwa eneo la kaskazini mashariki mwa Mali
  • Ansarul Islam - Linapatikana kaskazini mwa Burkina Faso
  • Boko Haram - Linaendesha shughuli zake katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi za Nigeria, Niger, Chad na kaskazini mwa Cameroon

Jinsi makundi hayo yanavyofadhili operesheni zao

Utafiti uliofanywa na taasisi ya usalama katika kipindi cha miaka miwili iliopita unaonyesha uhusiano kati ya wapiganaji walio na itikadi kali pamoja na vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika maeneo ya mipakani mwa Liptako-Gourma.

Makundi hayo yanafaidika kutokana na watoa huduma na wadhibiti wa vitendo hivyo.

Ili kuendeleza vitendo hivyo watoa huduma hizo hutafuta fedha, chakula na uwezo wa kuendeleza operesheni hizo mbali na kuimarisha maeneo wanayotoka ikiwemo kupitia kusajili wapiganaji wapya.

Kundi hilo limeanzisha mikakati ya kuchangisha fedha , wizi wa mifugo mbali na uchimbaji wa madini.

Wizi wa mifugo unafanyika kwa wingi katika eneo hilo hususani katika mpaka wa Mali na Niger na katika maeneo mengine ya katikati ya taifa la Mali.

Mifugo iliombwa huchukuliwa na kuuzwa katika masoko ya karibu ama kuuzwa wachinjaji.

Katika maeneo mengine makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali wameanza kuwatoza wakulima kodi ya mifugo yao ili kupata usalama.

kitendo hicho kimeenea sana katika mpaka katika ya Mali na Niger.

Baadhi ya makundi pia yanaishi katika maeneo mashariki mwa Burkina Faso yenye dhahabu, huku lengo la ni kufanya biashara ya madini hayo.