Uvamizi wa Panama: Operesheni ya Marekani iliomng'oa madarakani Manuel Antonio Noriega

Wanajeshi wa Marekani wanakalia gari la kijeshi katika barabara ya mji wa Panama wakati wa opereshen Just Cause tarehe 23 mwezi Disemba 1989

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Zaidi ya wanajeshi 20,000 wa Marekani walipelekwa nchini Panama

Uvamizi huo ulifanyika kupitia baharini, angani na ardhini. Maelfu ya wanajeshi walivamia Panama wakiwa na lengo la kumng'oa madarakani kiongozi wa taifa hilo na kumpeleka Miami ili kufunguliwa mashtaka.

Ilikuwa tarehe 20 mwezi Disemba 1989 na uhusiano wa karibu uliokuwepo kati ya jenerali Manuel Noriega na Marekani ulikuwa umezorota.

Katika hotuba yake kwa taifa , Rais George H W Bush alisema kwamba amewaagiza wanajeshi kuelekea Panama ili kulinda maisha ya raia wa Marekani na kumfungulia mashtaka Noriega.

Tangazo hilo lilijiri siku chache baada ya wanajeshi wa Panama kuwaua maafisa wa Marekani. Wakati huo, Noriega alikwa pia anakabiliwa na mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Marekani mbali na madai kwamba alikuwa amefanya udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa 1989.

Operation Just Cause, kama ilivyojulikana ilishirikisha wanajeshi 20,000 wa Marekani ambao walivamia taifa hilo na kudhibti kambi muhimu za kijeshi.

Chanzo cha picha, AFP

Kirasmi wanajeshi 514 na raia waliuawa katika uvamizi huo lakini baadhi ya makundi yanasema kuwa idadi kamili inakaribia 1,000. Wanajeshi 23 wa Marekani waliuawa.

Uvamizi huo uliugeuza mji wa Panama kuwa eneo la vita.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Msako nje ya ubalozi wa Vatican nchini Panama

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Marekani wajipanga nje ya duka la jumla nchini panama tarehe 23 mwezi Disemba 1989

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Ndege za kijeshi za Marekani zikipepea ndani ya anga ya Panama

Wafuasi wa Noriega walikamatwa wakati wa ghasia hizo.

Chanzo cha picha, AFP

Mtu huyu aliepatikana akiiba wakati wa uvamizi huo, alifungwa macho na kuzuiliwa na wanajeshi wa Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Marekani wamkamata mtu ambaye alikuwa akiiba aawakati wa uvaizi huo nchini Panama

Raia wa Panama waliokuwa wakimpinga Noriega walisherehekea kung'atuliwa kwa kiongozi huyo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Idadi kubwa wa raia wa Panama waliokuwa wakimpinga Jenerali Antonio Noriega wapeperusha bendera za marekani nje ya kituo kimoja cha Jeshi tarehe 22 mwezi Disemba 1989.

Noriega alitafuta hifadhi katika ubalozi wa Vatican. Wanajeshi walisalia nje ya ubalozi huo katika kipindi cha Krisimasi na kucheza muziki wa sauti ya juu wa Rock ili kumshinikiza kutoka .

Nyimbo za Clash, Van Halen na U2 ni miongoni zilizochezwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Marekani wakijiandaa nje ya ubalozi wa vatican nchini Panama ambapo Jenerali Noriega alikuwa amepata hifadhi tarehe 25 Disemba 1989

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Marekani wanaweka ulinzi nje ya ubalozi wa Panama wakati wa Operesheni ya Just cause tarehe 25 Disemba 1989

Noriega alisalimu amri tarehe 3 mwezi Januari 1990 baada ya kuishi ndani ya ubalozi huo kwa takriban siku 11 .

Baadaye alikamatwa na kusafirishwa na kitengo cha kukabiliana na dawa za kulevya hadi Miami ili kufunguliwa mashtaka, kabla ya kupatikana na hatia ya ulanguzi wa mihadarati pamoja na ule wa kifedha.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jenerali Noriega katikati akiwa ndani ya ndege ya Marekani baada ya kukamatwa n kuingizwa katika ndege ya Marekani akielekea Miami ili kufunguliwa kesi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Picha ya Jenerali Manuel Antonio Noriega tarehe 30 mwezi Mei 2017

Unaweza pia kusoma:

Noriega alihudumu kipindi chote cha maisha yake kizuizini - kwanza Marekani , baadaye Ufaransa na mwisho katika kifungo cha nyumbani nchini Panama.

Alifariki 2017, akiwa na umri wa miaka 83, kutokana na upasuaji wa kutoa uvimbe katika ubongo wake.

Picha zote zina hatimiliki.