Kesi ya kumuondoa madarakani Trump: Rais ataka kesi yake kuwasilishwa seneti mara moja

Spika wa bunge la uwakilishi nchini Marekani nancy Pelosi na rais Donald Trump Kulia
Maelezo ya picha,

Spika wa bunge la uwakilishi nchini Marekani nancy Pelosi na rais Donald Trump Kulia

Rais wa Marekani Donald Trump ametaka kesi inayomkabili ya utumizi mbaya wa mamlaka kuwasilishwa katika bunge la seneti mara moja , huku kukiwa na mkwamo miongoni mwa Democrats na Republicans kuhusu siku ya ya kuanzishwa.

Siku ya Jumatano, bunge la wawawkilishi nchini Marekani lilipiga kura ya kutaka kumuondoa madarakani kwa madai ya utumizi mbaya wa mamlaka na kulizuia bunge la uwakilishi.

Lakini Democrats wamekataa kuanzisha kesi hiyo ,wakidai kwamba bunge la seneti linadhibitiwa na Republicans ambao wamekataa mashahidi na kwamba haliwezi kufanya kesi ya haki.

Pia unaweza kusoma:

Idadi ya wanachama wa bunge la seneti inaonyesha wazi kwamba bwana Trump huenda akaondolewa mashtaka hayo.

Mchakato wa kumuuondoa madarakani rais huyo umechochewa na migawanyiko ya mabunge hao mawili kulingana na vyama vyao.

Maelezo ya picha,

Kiongozi wa wabunge wa Republican katika bunge la seneti Mitch McConnell

Mashtaka yaliowasilishwa dhidi ya Trump yanafuatia madai kwamba rais huyo aliishinikiza Ukraine kuchunguza habari kuhusu mpinzani wake wa Democrats Joe Biden na mwanawe wa kiume Hunter, na baadaye akakataa kushirikiana na uchunguzi wa bunge kuhusu swala hilo.

Je Trump alisema nini?

Katika msururu wa jumbe za twitter, rais aliwashutumu wabunge wa Democrats kwa kukataa kuendelea na kesi hiyo kwa kuwa ''kesi yao ilikuwa mbaya''.

Alituma ujumbe wa twitter akisema; Baada ya Democrats kukataa kunipa haki yangu bungeni, bila kuwa na wakili bila mashahidi, sasa wanataka kuliambia bunge la seneti jinsi ya kuendesha kesi hiyo.

''Kwa kweli hawana thibitisho la chochote, Na pia hawatakuwepo .Nataka kesi hiyo kufanyika sasa hivi!''

Maelezo ya picha,

Rais Trump anataka kesi inayomkabilia kuanzishwa mara moja

Rais alisema Democrats hawamtaki Adam Schiff, ambaye aliongoza mchakato wa kesi hiyo , familia ya Biden na wala mfichuzi wa CIA ambaye alisababisha kufanyika kwa uchunguzi huo kutoa ushahidi.

Kwa nini kuna mkwamo kuhusu kuanza kwa kesi hiyo?

Ili kesi hiyo kuanza bunge la uwakilishi linalodhibitiwa na Democrats ni sharti liwasilishe nakala za kesi hiyo kwa bunge la seneti.

Lakini spika wa bunge la uwakilishi Nancy Pelosi amekataa kufanya hivyo hadi pale sheria za kesi hiyo za seneti zitakapokubaliwa na Democrats.

Kiongozi wa Republican katika bunge la seneti Mitch McConnell , ataamua masharti ya kesi hiyo na Democrats wanamtaka kutoa maelezo kuhusu mashahidi na ushahidi utakaoruhusiwa.

Bwana McConnel amekataa kukubaliana na Democrats: Tunasalia katika mkwamo, alisema, baada ya mkutano mfupi na kiongozi wa walio wachache wa Democrats Chuck Schumer.

Bwana McConnel ana idadi kubwa ya wabunge wa Republican katika bunge hilo .

Kuna wabunge 53 wa Republican katika bunge hilo lenye viti 100 na kwa kura hiyo kumuondoa madarakani rais Trump itahitaji kuungwa mkono na thuluthi mbili ya wabunge .

Bwana McConnell ameutaja mchakato wa kesi hiyo kuwa moja iloharakishwa na isio ya haki katika historia, ikitoa ishara ya jinsi watu watakavyogawanyika kulingana na chama wakati kesi hiyo itakapoanza.

Democrats wanatumai kwamba kuchelewa huko kutaongeza maoni ya umma na kumnyima bwana Trump - rais wa tatu kufungliwa kesi Marekani - kuondolewa mashtaka.

Democrats wanataka wafanyakazi wanne wa Ikulu ya Whitehouse walio na ufahamu kilichoendelea UKraine kutoa ushahidi.

Wanasema kwamba kesi hiyo lazima ifanyike kwa haki na kwamba matamshi ya bwana McConnel yanaonyesha hayuko tayari kufanya hivyo.

Trump anakabiliwa na shutuma gani?

Kama matokeo ya uchunguzi yatapatikana, chama cha Democratic kinasema Bw Trump alitoa misaada miwili ya kijeshi yenye thamani ya dola milioni 400 za Kimarekani ambazo tayari zilikuwa zimeshapangwa na bunge, na mkutano na rais Volodymyr Zelensky.

Chama cha Democrat kinasema shinikizo hili kwa mshirika wa Marekani linaonesha matumizi mabaya ya madaraka.

Uchunguzi wa kwanza ambao Bw Trump aliutaka kutoka kwa Ukraine ulikuwa unahusu makamu wa rais mstaafu Joe Biden, ambaye ni mpinzani wake mkubwa kutoka chama cha Democratic na mtoto wake Hunter.

Hunter Biden alijiunga na baraza la kampuni ya nishati la Ukraine, pale baba yake alipokuwa makamu wa rais mstaafu Barack Obama.

Kitu cha pili ambacho Trump alitaka ni Ukraine kujaribu kurekebisha njama zinaonyesha kuwa Ukraine na sio Urusi ndio walioingilia uchaguzi mkuu uliopita wa Marekani.

Nadharia hii ilikuwa dhaifu, na vyombo vya uchunguzi nchini Marekani vimeficha kusema kuwa Moscow ndio waliofanya udukuzi wa barua pepe mwaka wa 2016.

Je kuna namna yoyote ambayo rais atapatwa na hatia?

Ni viongozi wachache wa Marekani ndio walifikia katika hatua ya namna hii. Kwa kuwa chama cha upinzani cha Democratic kina wingi wa wawabunge, kuna uwezekano kuwa Trump ataondolewa mashtaka.

Democratic wanataka kura hiyo ipigwe kabla ya mwisho wa mwaka.