Simulizi ya bingwa wa mchezo wa 'surfing' iliyoanza mitaani

Simulizi ya bingwa wa mchezo wa 'surfing' iliyoanza mitaani

Ntando Msibi alianza kuishi mitaani akiwa na umri wa miaka 11 baada ya kuondoka nyumbani kutokana na maudhi ya bibi yake mlevi aliyekuwa anamnyanyasa.

Alihangaika sana na maisha ya kutukanwa na kupigwa lakini aliweza kupata msaada kwa kutoka kwa wachezaji wa kuteleza kwenye maji kwa mbao maarufu kama 'Surfers' ambao wanawasaidia watoto wa mtaani kuwa watoto mahiri wa mchezo wa mbao mjini Durban.

Sasa Ntando ni mchezaji maarufu anayeshiriki mashindano ya kimataifa.

BBC iliweza kukutana na mtoto huyo nchini Afrika Kusini.