Marcial Maciel: Mwanzilishi wa kanisa katoliki Mexico anayetumiwa 'kuwanyanyasa kingono watoto 60'

Marcial Maciel, katika picha mwaka 2005, akiwa anaongoza misa mjini Rome

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marcial Maciel, katika picha mwaka 2005, akiwa anaongoza misa mjini Rome

Uchunguzi umebainika kuwa watoto wapatao 60 walinyanyaswa kingono na padre Marcial Maciel, muasisi wa taasisi ya kikristo ya 'Legionaries of Christ 'na muanzilishi wa kanisa katoliki nchini Mexico.

Matokeo ya utafiti ambao ulichapishwa na kundi la wakatoliki, umesema kuwa mapadre 33 waliwanyanyasa watoto 175 tangu ilipoanzishwa mwaka 1941.

Mwaka 2006, Maciel alitakiwa kustaafu kazi ya upadre kufuatia madai ya miaka kadhaa ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto wadogo.

Miaka miwili baadaye alifariki akiwa na umri wa miaka 87 bila ya shutuma zilizomkabili kubainika kuwa na ukweli kisheria.

"Inawezekana alikuwa anakabiliana na kesi nyingine nyingi za unyanyasaji wa kingono ukiachilia mbali zile zilizoripotiwa katika utafiti huu, hivyo takwimu za makosa yake zitakuwa zinarekebishwa kila wakati," ripoti hiyo iliandika.

Ripoti hiyo aidha iliongeza kuwa mchakato wa fidia na maridhiano ulianza na waathirika 45.

Nini kitatokea kwa mapadre wengine wanaoshutumiwa na unyanyasaji?

Kwa mujibu wa ripoti hiyo , "Mapadre sita kati ya 33 walikufa hata kabla ya kushitakiwa.

Mmoja amekamatwa, mwingine anasubiri hukumu yake kwa sasa na ameondolewa katika utume wake".

Wengine 18 bado ni sehemu ya asasi, ingawa wameondolewa katika majukumu ya uchungaji yanayohusisha kuwasiliana na umma au watoto.

Ripoti iliongeza kusema kuwa kati ya mapadre 14 ya hao 33 walikuwa waathirika wao wenyewe, hivyo ilikuwa ni cheni ya unyanyasaji inayozunguka, yaani yule aliyeathiriwa anakuja kumfanyia mwingine mwingine baada ya muda.

Wanaume kadhaa walimshutumu Maciel kabla ya kifo chake kwa unyanyasaji wa kingono wakati walipokuwa wanasoma shule za seminari kuanzia miaka ya 1940 mpaka miaka ya 1960.

Wakati ambao alikuwa anakana shutuma hizo mwaka 2002: "Sijawahi kujihusisha na tuhuma hizo ambazo wanaume hawa wananishutumu kuhusika."

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Marcial Maciel, kushoto, akiwa anapewa baraka na Papa John Paul II mwaka 2004 - mara baada ya madai ya shutuma zinazomkabili kutajwa

Mwaka 2006, Papa Benedict XVI alitaka kiongozi wa asasi ya 'Legionaries of Christ' kuachia wadhifa wake kutokana na tuhuma ambazo zilikuwa zinamkabili, jambo a mbalo mtangulizi wake Papa John Paul II alilipuuzia wakati tuhuma hizo zilipoanza kuibuka.

Baada ya kifo cha Maciel mwaka 2008, ilibainika kuwa alikuwa baba wa watoto kadhaa.

Siku ya jumanne, Papa Francis alitangaza kuwa hakuna muongozo wa usiri ambao utaendelea kufanyika dhidi ya unyanyasaji wa kingono wa watoto wadogo.

Maelezo ya sauti,

Papa Francis ameondoa kiapo cha siri kwa visa vya unyanyasaji wa kingono

Kanisa halitaendelea kukabiliana na kesi za namna hiyo kwa usiri, jambo ambalo lilidaiwa kuwa linawalinda waathirika na wadhifa wa wanaoshutumiwa.

Hakuna kipingamizi ambacho kimewekwa katika utafiti huo wa unyanyasaji na hata wa waathirika.

Hii ikiwa ni hatua iliyobuniwa kuboresha uwazi na uwezo wa polisi kufanya kazi zao kiufasha wanapohitaji taarifa kutoka kanisani.