Jinsi wapiganaji wa Islamic State wanavyoimarika Iraq

IS militants in Anbar province (2014)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

IS waling'olewa baada ya mapigano ya muda mrefu nchini Iraq, lakini hawakushindwa kabisa.

Kuna ongezeko kubwa la ishara kwamba kundi la Islamic State (IS) linajipanga tena nchini Iraq, miaka miwili baada ya kupoteza eneo la mwisho lililokua linalidhibiti nchini humo. Wakurdi na maafisa wa ujasusi wa magharibi wameiambia BBC kwamba uwepo wa IS nchini Iraq ni uasi wa kisasa na mashambulio yao yanaongezeka.

Wanamgambo hao kwa sasa wana ujuzi zaidi na ni hatari zaidi kuliko al-Qaeda kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa Kikurdi wa masuala ya kupambana na ugaidi Lahur Talabany.

"Wana mbinu bora zaidi, mikakati bora, na pesa zaidi," alisema . " Wako tayari kununu magari, silaha, chakula na vifaa. Kiteknolojia wako mnbele zaidi. Ni vigumu zaidi kuwamaliza.

Kwahivyo wako kama al-Qaeda wanaotumia steroidi ."

Unaweza pia kusoma:

Afisa wa mkongwe wa ujasusi alitoa tathmini yake kwa lafudhi ya London - aliyoipata katika miaka kadhaa aliyoishi Uingereza baada ya familia yake kuutoroka utawala wa Saddam Hussein.

Katika ngome yake iliyopo eneo la Sulaimaniya, lililozingirwa na milima ya jimbo la Kurdistan kaskazini mwa Iraq,alitoa picha ya kundi hilo lililomaliza miezi 12 likijijenga baada ya kusambaratishwa.

"Tunashuhudia shughuli zikiongezeka sasa, na tunafikiri awamu ya kikijenga upya imekwisha ," alisema Bwana Talabany, ambaye ni mkuu wa kikundi cha Zanyari moja ya makundi ya ujasusi ya Iraqi katika Kurdistan

Aina tofauti ya IS imejitokeza , anasema, ambayo haitaki kudhibiti eneo lolote ili kuepuka kulengwa na mashmabulio. Badala yake kama ilivyokua kwa watangulizi wao al-Qaeda - wapiganaji hao wenye itikadi kali wamejificha katika katika milima ya Iraq ya Hamrin.

"Hiki ndio kitovu cha ISIS [Kundi la Islamic State ] kwa sasa," alisema Bwana Talabany. " Ni eneo lenye milima mingi, na ni eneo gumu sana kudhibitiwa na jeshi la Iraqi . Kuna maeneo mengi sana ya kujifichana mapango."

Maelezo ya picha,

Mapango (kushoto)ambamo wapiganaji wa IS wamekua wakijificha

Alionya kuwa IS watanawiri kufuatia ghasia zinazoendelea katika mji mkuu wa Iraq , Baghdad, watatumia fikra za kutengwa kwa wenzaoWaislamu wa madhehebu ya Sunni - ambao ni wachache nchini Iraq ,hili ni suala la familia na damu linalofahamika.

"Kama tuna mzozo wa kisiasa " alisema: "Hii ni Paradiso/Ahera au Krismasi ya mapema kwa ajili ya ISIS."

Kukua kwa vyeo

Wapiganbaji wa IS pia wananufaika na mahusiano mabaya baina ya serikali ya Baghdad na ya kijimbo ya Kurdistan , kufuatia kura ya uhuru wa Wakurdi ya mwaka 2017.

Kuna eneo pana zaidi sasa ambalo halikaliwi na watu kaskazini mwa Iraq baina ya vikozi vya Kikurdi vya Peshmerga na wenzao wa Iraqi. Kwamujibu wa Bwana Talabany, wanaofanya doria katika eneo hili tu ni IS.

Maelezo ya picha,

Mwanajeshi wa Peshmerga akitazama eneo lisilomilikiwa na binadamu yoyote ambako wapiganaji wa IS huzurura

Akiwa katika kilima juu ya mifuko ya michanga huku akiangalia mji wa Gwer, Meja Jenerali General Sirwan Barzani anaweza kutazama eneo lisilodhibitiwa na mtu yeyote, huku akionekana uwa mwenye wasiwasi . Kamanda wa Wakurdi wa Peshmerga canasema sasa IS wana eneo huru hapa ambalo halidhibitiwi na mtu yeyote.

" Katika eneo la bonde kati ya Great Zab na Tigris tunaweza kusema kuwa mito ipo pale daima ," alisema. " Kuna shughuli nyingi kupita kiasi za IS katika eneo lililopo karibu na Tigris. Siku hadi siku tunashuhudia harakati za ISIS, na shughuli zao."

Kwa mujibu wa ripoti za ujasusi za Peshmerga, hadhi ya IS katika eneo hilo imekua ikiimarishwa na wapiganaji 100 ambao walivuka mpaka kutoka Syria, wakiwemo baadhi ya wapiganaji wa kigeni baadhi yao wakiwa na mikanda ya vilipuzi vya kujitoa muhanga.

Maelezo ya picha,

"Kama hali itaendelea kama ilivyo, IS watakuwa ni kundi lililojipanga zaidi 2020," anaonya Meja Generali Gen Sirwan Barzani

Ilikuwa ni katika eneo la miinuka la Gwer ambako Peshmerga walianzisha mashambulio ya kwanza dhidi ya wapiganaji wa Islamic State ( IS) mwezi Agosti 2014. Meja Jenerali Serwan Barzan na wenzake wanasema kuwa historia inajirudia.

"Ninaweza kulinganisha yaliyotokea mwaka 2019 na mwaka 2012, " alisema, " wakati wapiganaji wa IS walipoanza , kujikusanya na kuanza kuchukua ushuru kutoka kwa watu. Kama hali itandelea kama ilivyo, mwaka 2020 watajikusanya tena na kujipanga zaidi, na kuwa imara na kufanya mashambulizi ."

Maafisa wa ujasusi wa Kikurdi wanakadiria kuwa IS wako 10,000 na imara ndani ya Iraq huku kati ya 4,000 na 5,000 wakiwa ni wapiganaji, na idadi sawa na hiyo ni ni wafuasi ambao ni raia

Jami ya kimataifa ina sababu ya kuhofia , kwa mujibu wa Lahur Talabany. " jinsi wanavyokuwa na urahisi kwao kufika hapa ," anasema , "watakua na mawazo ya kuendesha operesheni nje ya Iraq na Syria."

Wanaongeza shinikizo

Kamanda wa ngazi ya juu wa Marekani nchini Iraq anasema kuwa IS inajaribu kujiunda upya lakini inakabiliwa na mashambulio tofauti kutoka kwa Iraqi na vikosi vya usalama vya wakurdi wakati huu.

Kwa mujibu wa Brigadia Jeneral William Seely, kamanda wa kikosi cha nguvukazi nchini Iraq, vikosi hivi vilikua vimejiandaa vema kuliko vilivyokua mwaka 2014 wakati IS walipopata udhibiti wa theluthi moja ya Iraqna kuuteka mji wa Mosul, ambao ni mi wa pili kwa ukubwa, pila upinzani wowote.

"Vikosi vya Iraq (ISF) na vile vya Peshmerga sio vikosi sawa na vile vilivyokuwepo wakati mji wa Mosul ulipoanguka ," alisema Brigaria Jenerali Seely. "Tumekua hapa tukiwapatia mafunzo juu ya mafunzo waliyokuwa nayo. ISF wanaongeza juhudi kuhakikisha mapambano dhidi ya Daesh [IS] yanaendelea ."

Map: Map of Iraq and Syria

Alielezea kuhusu mwezi mmoja, kutoka -Octoba hadi November, ambapo SF ilifanya mashambulio 170 ya "kusafisha " na kuwaangamiza takriban wapiganaji 1,700 kwa kutumia vifaa vya kulipua vilipuzi vya kutegwa.

Anasema wapiganaji wa IS kwa sasa wamejifisha katika mapango na jangwani "katika hali ambazo hakuna mtu anaweza kuzivumilia kwa muda mrefu sana ", na hawawezi kujiunda katka makundi makubwa . "Kundi kubwa zaidi nililolishuhudia katika kipindi cha miezi sita hapa ni la watu 15, anasema, na kuongeza kuwa hata mpiganaji mmoja wa ISIS ni wengi''.

Kwa sasa wapiganaji wenye itikadi kali wamesalia mafichoni - wakijitokeza usiku kufanya wakishambulia- na kukimbia.

Lakini Iraqimeshuhudia tisho liliongeza tangu kundi hili lilipoanza, na baadhi wanahofia tisho jipya linakuja, kutoka kanda hiyo na Magharibi..