Kutana na Mani Love, mchezaji wa mpira wa kikapu mwenye urefu wa mita 1.34

Kutana na Mani Love, mchezaji wa mpira wa kikapu mwenye urefu wa mita 1.34

Jahmani Swanson, anayefahamika kwa jina Mani Love, anacheza mpira wa kikapu katika timu ya Harlem Globetrotters ya New York na amekua maarufu sana katika mtandao wa intaneti baada ya kufikia ndoto yake ya kuwa nyota wa mpira wa kikapu, licha ya kuzaliwa na hali ya kimo kifupi (mbilikimo) . Hapa anatembelea shule nchini Uingereza kuwatia moyo wanafunzi kuwa na "ndoto kubwa" na kujivunia tofauti zao.