Janga la utoro wa shule Japan 'Futoko' lashika kasi

Children playing in Tamagawa Free School Haki miliki ya picha Stephane Bureau du Colombier

Nchini Japan, watoto wengi zaidi wameanza kukataa kwenda shule, mtindo ambao unafahamika kama "futoko". Kadri idadi inavyoongezeka , watu huwa wanajiuliza kuhusu mfumo wa shule kuliko tatizo la watoto wenyewe.

Mtoto mwenye miaka 10 Yuta Itoalikuwa anasubiri likizo yake kwa hamu ili aweze kuwaambia wazazi wake jinsi wanavyojisikia kuwa hajisikii tena kwenda shule.

Kwa miezi kadhaa amekuwa akihudhuria shule ya msingi kwa kulazimishwa sana, mara nyingi huwa anakataa kabisa.

Anasema kuwa alikuwa ananyanyaswa na alikuwa anagombana na wanafunzi wenzie darasani.

Wazazi wake wakati huo walikuwa na mambo matatu ya kuchagua: Kumfanya Yuta aweze kuhudhuria shule kwa kumueleza umuhimu na vitu ambavyo angeweza kuvipata kama akiweza kwenda shule kwa matumaini kuwa hali itabadilika.

Miongoni mwa mambo waliyokuwa wakimueleza ni pamoja na kumfundisha nyumbani na kumpeleka shule bila gharama au kubaki nyumbani, naye akachagua namba tatu.

Na sasa Yuta anatumia muda wake ambao alipaswa kwenda shule kufanya kile anachojisikia kufanya na ana furaha zaidi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shule ya msingi ya Japan

Yuta ni miongoni mwa wanafunzi wanaotumia mtindo wa futoko, inayomaanisha kwa wizara ya elimu Japan kuwa ni wanafunzi ambao wanaacha kwenda shule kwa zaidi ya siku 30, kwa sababu ambazo hazina uhusiano na matatizo ya masuala ya kiafya au kifedha.

Kutohudhuria huko kwa wanafunzi shuleni huwa kunatajwa kuwa ni utoro, uoga wa shule au mtoto kugoma tu kusoma.

Tabia za mtindo wa futoko zimeweza kubadilika kwa miongo kadhaa.

Mpaka mwaka 1992 watoto walianza kukataa kuhudhuria shule na wengi wakadhani ni ugonjwa wa akili.

Lakini mwaka 1997 jina liliadilika na kuwa watoto wasiohudhuria shuleni.

Tarehe 17 Oktoba, serikali ilitangaza kuwa idadi ya wanafunzi watoro shuleni imeongezeka kwa kiwango cha juu, kati ya wanafunzi 164,528 watoto 30 hawahudhurii shule kwa muda wa siku 30 au wanafunzi zaidi walitega shule mwaka 2018, huku mwaka 2017 watoto 144,031 walitega.

Haki miliki ya picha Stephane Bureau du Colombier
Image caption Mbwa akiwa amehudhuria shule ya bure ya Tamagawa

Mvutano wa kuwa na shule za bure ulianza Japan mwaka 1980, na kufanya idadi ya utoro shuleni kukua zaidi.

Kuna shule nyingine ambazo zinawapa uhuru wa kujiamulia.

Huwa wanakubali mtu kuchagua masomo ya ulazima pamoja na kujifunza ukiwa nyumbani ingawa hawawezi kutambua masomo hayo ambayo wanapata nyumbani.

Idadi ya wanafunzi wanaohudhuria shule ya bure au shule inayompa mwanafunzi uhuru wa kuchagua masomo badala ya kufuata mfumo wa kawaida zimefungwa miaka kadhaa iliyopita kuanzia ilipoanza kuwa 7,424 mwaka 1992 mpaka 20,346 mwaka 2017 .

Utoro mashuleni umeweza kusababisha athari za muda mrefu, na kuna hatari kuwa kuwa vijana wanaweza kujitenga na jamii kabisa na kutaka kujifungia katika vyumba vyao tu tabia inayojulikana kama hikikomori.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption wanafunzi wa shule ya bure

Inacholeta hofu zaidi ni idadi ya wanafunzi ambao huwa wanajiua. Mwaka 2018, idadi ya watoto waliojiua ni kubwa zaidi ya miaka 30 iliyopita kwa kuwa na kesi 332 .

Mwaka 2016 idadi ya wanafunzi wanaojiua iliongezeka na kufanya serikali ya Japan kupitisha sheria ya kuzuia hualifu huo kwa kutoa mapendekezo kadha katika shule.

Haki miliki ya picha Stephane Bureau du Colombier
Image caption Shule za bure ziliweka sheria zao wenyewe

Kwa nini watoto wengi wanakataa kwenda shule Japan?

Masuala ya kifamilia, ya mtu binafsi na masuala ya kirafiki, na kuoneana shuleni ni miongoni mwa sababu zinazowapelekea kuacha shule kwa mujibu wa utafiti wa wizara ya elimu nchini umo.

Kwa ujumla, wanafunzi walioacha shule waliripoti kuwa walikuwa hawapatani na wanafunzi wengine shuleni na mara nyingine na walimu.

Hii ilikuwa kesi ya Tomoe Morihashi.

"Yeye alikuwa hajioni kuwa yuko huru shuleni na watu wengi ," alisema mtoto wa miaka 12. "Alisema maisha ya shule yalikuwa ya maumivu makubwa sana."

Tomoe alikuwa ana matatizo ya utindio wa ubongo, hivyo alisumbuka sana akiwa katika mazingira ya umma.

"Nilikuwa siwezi kuzungumza nkiwa nje ya nyumbani na watu ambao sio familia yangu," alisema.

Haki miliki ya picha Getty Images

Shule nyingi za Japan huwa zinaangalia muonekano wa wanafunzi, huwa zinawalazimisha wanafunzi wenye nywele za brown kuweka rangi, vilevile huwa hawawaruhusu kuvaa koti wakati wa baridi

Mara nyingine wanawachagulia hata rangi za nguo ya ndani ambazo wanapaswa kuvaa.

Shule zenye misimamo hiyo zilianzishwa mwaka 1970s na 1980s na kudaiwa kuwa ni uonevu.

Shule hizo zilipunguza makali mwaka 1990s lakini zimeanza kuwa na sheria kali tena miaka ya hivi karibuni.

Haki miliki ya picha Stephane Bureau du Colombier
Image caption Watoto huwa wanapewa mwanya wa kufanya kile wanachojisikia shuleni

Utaratibu wake hauko katika mpangilio kama nyumba ya familia kubwa. Wanafunzi huwa wanakutana sehemu na kupiga soga na kucheza pamoja.

" Lengo la shule ni kukuza ujuzi wa mtu binafsi ," alisemaTakashi Yoshikawa, Mwalimu mkuu wa shule.

Kufanya mazoezi , kucheza michezo mbalimbali au kusoma ni miongoni mambo muhimu kujifunza .

Haki miliki ya picha Stephane Bureau du Colombier
Image caption Watoto wapatao 10 huwa wanahudhuria kila siku shule ya bure ya Tamagawa
Haki miliki ya picha Stephane Bureau du Colombier
Image caption Children playing in Tamagawa Free School

Mtaalamu wa masuala ya elimu , Profesa Uchida anasema kuwa wanafunzi wengi wanaotega shuleni wamefanya kama mtindo wa maisha sasa.

Vilevile shule zimeshindwa kutoa mazingira rafiki katika mfumo wa elimu wanaoutoa.

Takribani vijana nusu milioni wanaacha kuhudhuria shule nchini Japan na wanadaiwa kujitenga na jamii kwa kukataa kutoka vyumbani mwao.

Vijana hawa wanafahamika kama hikikomori.

Familia zao huwa wanakuwa katika wakati mgumu na kushindwa nini cha kufanya.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii