Je kufutwa kazi kwa Mkuu wa Boeing afutwa kazi, ndio suluhu ya matatizo ya 737?

Dennis Muilenburg

Chanzo cha picha, Getty Images

Boeing imemfuta kazi mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, Dennis Muilenburg, katika hatua ya kurejesha imani ya kampuni hiyo baada ya ajali mbili mbaya zilizohusisha ndege yake ya 737 Max.

Zaidi ya watu 340 walikufa katika mkasa uliochochea shutuma kwamba Boeing iliweka mbele faida zaidi ya usalama.

Familia za waathiriwa zimeafiki hatua ya kujiuzulu kwa Bwana Muilenberg.

Lakini walisema uamuzi wa Boeing kumuondoa mamlakani na badala yake kumpatia nafasi hiyo mjumbe wa zamani wa bodi yake kunaacha maswali juu ya wajibu wa kuleta mabadiliko.

Boeing ilimtaja David Calhoun, ambaye alihudumu katika bodi ya kampuni hiyo 2009 na mwenyekiti wake wa sasa kama Mkurugenzi mkuu mtendaji na rais.

"Huku kujiuzulu kwa Bwana Muilenburg ikiwa ni hatua nzuri, ni wazi kwamba kampuni ya Boeing inahitaji kufanya mabadiliko ya utawala wake wa kampuni ," alisema Paul Njoroge, ambaye alimpoteza mke wake, watoto watatu na mama mkwe wake wakati ndege ya Ethiopian Airlines chapa 302 ilipoanguka mwezi Machi.

Bwana Calhoun "si mtu sahihi kwa kazi ", aliongeza.

Zipporah Kuria, ambaye baba yake aliuawa katika ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines , alisema kuwa Bwana Muilenburg angepaswa kuwa ameondolewa mamlakani "zamani " lakini uwajibikaji wa ajali unawahusu wengi.

"Ninajihisi ni kama watu wengi zaidi wangepaswa kujiuzulu ikiwemo mtu ambaye anachukua nafasi ya Bwana Muilenburg ,"aliiambia BBC.

Mabadiliko 'Muhimu'

Boeing imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la uchunguzi mkali dhidi ya ndege za 737 Max kufuatia ajali zake zilizotokea katika kipindi cha miezi mitano, ya kwanza ikiwa ni ya Indonesia na baadaye ya Ethjiopia.

Safari za ndege za za 737 zimepigwa marufuku kusafiri kote duniani tanu mwezi Machi.

Huku kampuni hiyo ikiwa na matumaini ya kurejesha angani ndege zake ambazo ndizo zinazouzwa zaidi duniani kufikia mwishoni mwa mwaka huu , wakaguzi wa viwango vya ndege nchini Marekani wamesema wazi kuwa haitapata kibali cha kurejea angani haraka.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Eneo la ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines chapa 302

Wiki iliyopita Boeing ilisema kuwa itasitisha uzalishaji wa ndege zake.

Halafu Ijumaa sifa ya kampuni ilipata pigo jingine wakati chombo chake cha anga za juu kilipopata matatizo ya kiufundi yaliokizuwia kutumia njia sahihi katika kituo cha kimataifa cha anga za juu.

Bodi ya Boeing ilisema "imeamua kuwa mabadiliko ya uongozi wake ni muhimu ili kurejesha imani katika kampuni inapojaribu kusafisha uhusiano wake na wasimamizi wa viwango vya safari za anga, wateja na wadau wote ".

Bwana Calhoun, mkurugenzi mtendaji wa masuala ya usalawa, atachukua wadhfa wake kuanzia Januari 13.

Unaweza pia kusoma:

Lawrence Kellner, mjumbe wa bodi tangu 2011, atakua mwenyekiti ambaye si mtendaji mara moja.

"Chini ya uongozi mpya, Boeing itafanya kazi kwa uwajibikaji wenye uwazi kamili, ikiwemo mawasiliano thabiti na Shirikisho la utawala wa safari za anga FAA [Federal Aviation Administration], waangalizi wengine wa dunia na wateja wake ," ilisema.

Licha ya kufanya mabadiliko, wakosoaji wakuu wa kampuni hiyo mjini Washington walisema kuwa bado wana maswali juu ya mabadiliko ya uwajibikaji ndani ya kampuni hiyo.

Seneta Richard Bumenthal alisema: " Kampuni inahitaji utawala mpya katika bodi na waweke watu watakaochukulia usalama kwa umakini."

Michael Stumo, ambaye alimpoteza binti yake Samya Rose katika ndege ya Ethiopian Airlines na ambaye amezikusanya familia dhidi ya Boeing, alisema kujiuzulu ni "hatua ya kwanza nzuri kuelekea kuifanya Boeing kuwa kampuni ambayo inatoa kipaumbele kwa usalama na uvumbuzi ".

"Hatua inayofuatia ni ya wajumbe kadhaa ambao hawafanyi kazi kwa viwango vinavyotakikikana na wasio na ujuzi kujiuzulu,"alisema.

'Tatizo la mfumo'

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Dennis Muilenburg alikabiliwa na miito ya kujiuzulu

Maafisa wa usalama wa ndege wanaochunguza mikasa wamebaini mfumo wa uongozaji wa ndege unaofahamika kama MCAS, kuwa ndio chanzo cha ajali zote mbili.

Boeing imesema kuwa mfumo wa MCAS , ulioendeshwa kwa kutegemea taarifa moja, ulipokea data, ambazo ziliusababishia kuvuruga mawasiliano ya rubani.

Imesema kuwa inautengeneza mfumo huo na imeboresha mchakato wake wa mawasiliano.

Lakini wabunge wa Marekani, ambao wanachunguza kampuni wamesema kuwa ilifahamu fika kwamba mfumo wake wa uongozaji wa ndege ulikua sio wa kutegemewa.

Wameishutumu kampuni hiyo kwa kuficha hatari na kukimbilia kuirejesha ndege kutoa huduma ya usafiri.